WEKA TAREHE KAMILI NI LINI UNAKUSUDIA KUMILIKI PESA UNAZOTAMANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WEKA TAREHE KAMILI NI LINI UNAKUSUDIA KUMILIKI PESA UNAZOTAMANI





Inatoka sehemu ya i kama hukuisoma isome hapa.

Asubuhi moja baada ya moto mkubwa wa Chicago, kundi la wafanyibiashara walisimama kwenye barabara ya umma, wakitazama mabaki ya moshi wa yaliyokuwa maduka yao. Walifanya mkutano kuamua ikiwa kama wangejaribu kujenga tena upya, au kuhama Chicago na kwenda kuanza tena katika eneo jingine la nchi ambalo lingekuwa na matumaini zaidi.Wote isipokuwa mmoja wao, walifikia uamuzi wa kuondoka Chicago.

Mfanyabiashara aliyeamua kubaki na kujenga upya, alinyosha kidole kwenye mabaki ya lile duka lake, na kusema, “Mabwana, juu ya eneo lilelile nitajenga duka kubwa kuliko yote Duniani, pasipokujali ni mara ngapi litaungua”. Duka lilijengwa, na mpaka leo hii lipo jengo refu la ukumbusho kwa nguvu ya ile hali ya akili iitwayo Shauku kuu.

Kitu rahisi kwa jemadari mkuu kufanya kingeweza kuwa sawasawa na kile wafanyabiashara wenzake walichofanya. Safari ilipokuwa ngumu na majaaliwa ya baadae kuonekana ni yenye majonzi, walisita na kuelekea kule walikoona mambo ni rahisi.

Kumbuka vyema tofauti hii kati ya Jemadari na Wafanyabiashara wenzake, kwasababu ni tofauti hiyohiyo inayomtofautisha Edwin C. Barnes na maelfu ya vijana wengine waliowahi kufanya kazi katika kampuni ya Edison. Ni tofauti hiyohiyo ambayo hutofautisha kivitendo wale wote wanaofanikiwa na wale wanaofeli.

Kila binadamu anayefahamu makusudi ya pesa, hutamani kuzipata. Kutamani peke yake hakutaleta utajiri. Lakini kutamani utajiri huku ukiwa na hali ya akili iliyokuwa na utayari, kisha ukapanga mipango dhahiri na njia za kuufikia utajiri, na ukaisaidia hiyo mipango kwa uvumilivu usiotambua anguko(kufeli) kutaleta utajiri.

Njia ambayo shauku ya utajiri inaweza kubadilishwa na kugeuka kuwa katika kipimo cha pesa imegawanyika katika hatua sita kamili za kivitendo,
1.  Jenga picha akilini mwako ya kiasi kamili cha pesa unachotamani, haitoshi tu kusema, “Nataka kiasi kikubwa cha pesa”, kuwa muwazi ni kiasi gani (Kuna sababu za kisaikolojia kutaja kiasi kamili, ambazo zitaelezwa katika sura inayofuata.

2.  Tambua hasa ni kitu gani unachokusudia kurudisha kama malipo kwa fedha unazotamani(Ukweli ni kwamba, hakuna kitu cha bure)


3.  Weka tarehe kamili ni lini unakusudia kumiliki pesa unazotamani.

4.  Tengeneza mpango kamili wa kutekeleza tamanio lako, na anza mara moja pasipo kujali kama upo tayari kuuweka mpango huo katika vitendo ama la.


5.  Andika sentensi fupi na inayoeleweka ya kiasi cha pesa unachokusudia kupata. Taja muda wa mwisho wa kuzipata. Eleza kile unachokusudia kutoa kama malipo kwa pesa utakazopata, na elezea kwa ufasaha mpango ambao kwa kupitia huo umekusudia kuzikusanya.

6.  Soma sentensi yako uliyoandika kwa sauti mara mbili kwa siku, mara moja punde kabla hujalala usiku, na mara moja baada ya kuamka asubuhi. WAKATI UKISOMA, ONA NA HISI NA AMINI WEWE MWENYEWE TAYARI UKIWA UNAMILIKI HIZO PESA.

Ni muhimu kwamba unafuata maelezo yaliyoelezwa katika hizi hatua sita. Ni muhimu zaidi kwamba unazingatia na kufuata maelekezo katika aya ya sita .

Unaweza ukalalamika kwamba, haiwezekani kwa wewe, “kuona mwenyewe ukimiliki pesa kabla hujawa nazo kiukweli. Hapa ndipo shauku kuu inapoanza kufanya kazi. Ikiwa kweli unatamani sana pesa kiasi ambacho tamaa yako umeijaza akilini, hautapata ugumu katika kujishawishi mwenyewe kwamba utazipata.

Ni wale tu wenye utambuzi wa pesa wanaoweza kulimbikiza utajiri mkubwa. Utambuzi wa pesa maana yake ni kwamba akili imejawa mno na hamu ya pesa kiasi kwamba mtu anaweza kujihisi mwenyewe kuwa tayari anazimiliki.

Kwa wale ambao hawajapata elimu ya jinsi akili ya binadamu inavyofanya kazi, maelekezo haya yanaweza yakawa hayatekelezeki kivitendo. Yanaweza yakawa msaada, kwa wale wote wanaoshindwa kutambua mantiki ya zile hatua sita, kujua kwamba taarifa wanazopata zilitoka kwa Andrew Carnegie ambaye alianza kama kibarua wa kawaida tu kwenye kiwanda cha chuma.

Licha ya mwanzo wake duni Carnegie aliweza kuzifanya kanuni hizi kumpatia utajiri unaokadiriwa kuwa zaidi ya dolla million 100. Yaweza kuwa msaada zaidi kujua kwamba hatua sita zilizopendekezwa hapa zilichunguzwa kwa makini na Thomas A. Edison.
Aligonga mhuri wa kibali juu yake kuashiria siyo tu kwamba hatua hizo ni kwa ajili ya kujichumia pesa peke yake, bali pia ni kwa ajili ya kulifikia lengo lolote lililokuwa dhahiri. Hatua hizo hazihitaji “kufanya kazi ngumu” Hazihitaji kujitoa mhanga. Hazihitaji mtu kuwa na dharau, au kuwa mjinga. Ili kuzitumia hauhitaji kuwa na kiwango kikubwa cha elimu.

Lakini matumizi yenye tija ya hizi hatua sita yanahitaji ubunifu wa kutosha kumuwezesha mtu kuona na kuelewa, kwamba utajiri hauwezi ukatokea tu kwa bahati na sibu. Mtu anapaswa kutambua  yakwamba, wale wote ambao wamewahi kujilimbikizia utajiri mkubwa, kitu cha kwanza kabisa kufanya kabla hawajapata pesa, kwa kiasi fulani waliota ndoto, kuwa na matumaini, kuwa na matamanio, shauku na mipango.

 ---------------------------------------------------------------------------------------

Usikose sehemu ya (iii) kesho,tutaendelea kuwa pamoja na tunakutakia safari njema kuelekea mafanikio katika shughuli zako.

Ngugu msomaji kama kuna chochote ambacho ungependa tuboreshe katika blogu hii au una maoni yeyote tafadhali yaweke hapo chini sehemu ya kutoa maoni na si lazima ujitambulishe. Pia tunapenda kuwajulisha kwamba vitabu vyote vya Self Help Books, "Mifereji ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa", "Siri ya mafanikio Biashara ya rejareja" na "Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali", sasa vyote vimekamilika.

Ukiwa Dar es salaam unaweza kuvipata kwa mawakala wetu au katika duka lililopo nje ya ofisi zetu Buguruni sokoni stendi mbele kidogo ya Benki ya Akiba simu zetu ni '0712 202244'/ '0765 553030'. Na kama uko mikoani, mkoa wowote ule tutakutumia kwa njia ya Mabasi au unaweza ukamuagizia mtu/jamaa yako anayefika Dar akuchukulie.



0 Response to "WEKA TAREHE KAMILI NI LINI UNAKUSUDIA KUMILIKI PESA UNAZOTAMANI"

Post a Comment