HATUA 6 + KANUNI YA KUINGIZA KIASI CHOCHOTE CHA PESA UNAZOTAKA MAISHANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATUA 6 + KANUNI YA KUINGIZA KIASI CHOCHOTE CHA PESA UNAZOTAKA MAISHANI


KUJISHAURI BINAFSI
NJIA YA KUSHAWISHI AKILI YA NDANI.
(Hatua ya tatu kuelekea utajiri)
Kujiashauri binafsi ni neno linalotumika kwa mawazo yote na vichocheo vyote vinavyosimamiwa binafsi ambavyo hufika katika akili ya mtu kupitia milango mitano ya fahamu. Kwa lugha nyingine, kujishauribinafsi ni kujiingizia mawazo akilini  mwenyewe.

Ni wakala wa mawasiliano kati ya ile sehemu ya akili ambapo fikra za fahamu hutokea na ambayo huhudumu kama kiti cha vitendo kwa ajili ya akili ya ndani. Kupitia mawazo yanayotawala, mtu huruhusu kubakia katika ufahamu(iwe mawazo hayo ni hasi au chanya haijalishi), kanuni ya kujishauribinafsi kwa hiyari huifikia akili ya ndani na kuiathiri kwa mawazo hayo.

Ukiacha fikra(mawazo) yanayochukuliwa kutoka angani(ether), hakuna mawazo yawe ni chanya ama hasi, YANAYOWEZA KUINGIA AKILI YA NDANI BILA MSAADA WA KANUNI HII YA KUJISHAURIBINAFSI. Kwa maneno mengine, maono yote ya fahamu ambayo hutambuliwa kupitia milango mitano ya fahamu huzuiliwa na akili ya kawaida ya kufikiria na yanaweza, aidha kupitishwa kwenda katika akili ya ndani au kukataliwa kwa hiyari. Kwa hiyo kitivo cha akili ya nje ya kawaida  huhudumu kama mlinzi wa nje dhidi ya kuikaribia akili ya ndani.

Hivyo asili imetujenga sisi kwamba tunao udhibiti wote juu ya kitu kinachoingia katika akili yetu ya ndani kupitia milango 5 ya fahamu ingawa hii haina maana kutafsiriwa kama kauli kwamba kila mara tunatekeleza udhibiti huu. Kwa upande mwingine mara nyingi sana huwa hatuitekelezi na hiyo ndiyo sababu kwanini watu wengi kiasi hicho hupitia maisha ya umasikini.

Kumbuka kile kilichokwisha semwa juu ya akili ya ndani kufanana na bustani yenye rutuba ambayo magugu yataota kwa wingi ikiwa mbegu za mazao mazuri hazitapandwa pale. Kujishauri binafsi ni wakala wa uthibiti ambaye kupitia yeye  mtu kwa hiyari huilisha akili ya ndani fikra zenye asii ya kujenga au kwa kutokujali, kuruhusu fikra zenye asili ya kubomoa kuingia katika bustani hii tajiri ya akili.

Ulifundishwa katika hatua ya mwisho ya hatua sita zilizoelezwa katika sura ya 2, kusoma kwa sauti mara mbili kwa siku kauli iliyoandikwa ya shauku yako kwa pesa, na kuona na kuhisi mwenyewe tayari ukiwa unamiliki hizo pesa. Kwa kufuata maelekezo haya, unawasilisha nia ya shauku yako moja kwa moja kwenye akili ya ndani katika roho ya imani kamilifu. Kupitia kurudiarudia kwa njia hii kwa hiyari unatengeneza tabia za mawazo zinazoendana na juhudi zako kubadilisha shauku kuwa katika kiasi cha fedha kinacholingana nayo.

Rudi katika hatua hizi sita zilizoelezwa katika sura ya 2, na uzisome tena kwa uangalifu kabla hujaendelea zaidi. Kisha (utakapoikuta), soma kwa makini sana hatua nne kwa ajili ya kuunganisha kundi lako la kushauriana(mastermind group) zilizoelezwa katika sura ya 7. Kwa kulinganisha hatua hizi mbili za mafunzo na zile zilizoelezwa kwenye kujishauri binafsi, utaona kwamba mafundisho huhusisha  matumizi ya kujishauribinafsi.

Kwahiyo kumbuka , wakati unaposoma kwa sauti ile kauli ya shauku(ambayo kupitia hiyo unajitahidi kukuza “ufahamu wa pesa”), kwamba kusoma tu peke yake hakuleti matunda yeyote ikiwa hautachanganya mhemko wa hisia na maneno yako. Ikiwa utarudia mara elfu kanuni maarufu ya Emil Coue isemayo, “Siku baada ya siku, katika kila hali, naendelea kuwa bora zaidi”, pasipo kuchanganya mhemko wa imani na maneno hayo, hautapata matokeo mazuri.

Akili yako ya ndani hutambua na kufanyia kazi tu yale mawazo yanayochanganywa na mhemko wa hisia. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa kuhalalisha kitendo cha kurudiarudia katika kila sura. Ukosefu wa uelewa wa hili ndiyo sababu kubwa ya watu wengi wanaojaribu kutumia kanuni ya kujishauribinafsi kutopata matokeo mazuri.

Maneno matupu yasiyokuwa na hisia hayawezi kushawishi akilli ya ndani. Hutapata matokeo makubwa, mpaka utakapojifunza kuifikia akili yako ya ndani na mawazo au maneno yaliyotamkwa vizuri kwa hisia na imani. Usikatishwe tamaa kama huwezi kudhibiti na kuongoza hisia zako mara ya kwanza unapojaribu kufanya  hivyo. Kumbuka hakuna uwezekano kama huo wa kupata kitu pasipo kutoa kitu chochote, uwezo wa kuifikia na kuishawishi akili yako ya ndani una gharama yake na ni lazima ulipe gharama hiyo. Hauwezi ukadanganya , hata kama unatamani kufanya hivyo. 

Gharama ya uwezo wa kuishawishi akili yako ya ndani ni msimamo usiokuwa na kikomo katika kuzitumia kanuni zilizoelezwa hapa. Huwezi ukatengeneza uwezo unaotarajiwa kwa gharama ya chini. Wewe na ni wewe mwenyewe unayepaswa kuamua ikiwa malipo kwa kile unachohangaikia(utambuzi wa pesa) yanalingana au hayalingani na gharama ya nguvu unayolazimika kulipa katika jitihada.

Busara na ujanja peke yake havitavuta na kutunza pesa isipokuwa katika nyakati chache sana ambapo kanuni ya wastani(kadiri) huegemea upande wa kuvuta pesa kupitia vyanzo hivi. Njia ya kuvuta pesa iliyoelezwa hapa haitegemei sheria ya kadiri. Zaidi njia hiyo huwa haina upendeleo. Itafanya kazi vizuri kwa mtu mmoja  kama itakavyofanya kazi kwa mtu mwingine. Pale kushindwa kunapotokea, ni mtu mwenyewe, na siyo njia iliyomuangusha. Kama utajaribu na kushindwa, fanya jitihada nyingine na nyingine tena, mpaka umeshinda.

Uwezo wako wa kuitumia kanuni ya kujishauri binafsi utategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wako wa kuelekeza nguvu zote pamoja(concentration) kwenye shauku mpaka pale shauku hiyo inapogeuka kuwa jukumu muhimu zaidi. Unapoanza kuchukua mafunzo kuhusiana na hatua sita zilizoelezwa katika sura ya pili, itakuwa ni muhimu kwako kufanya matumizi ya sheria ya kuweka nguvu zote pamoja.

Ngoja hapa tutoe ushauri wa matumizi bora ya kukusanya nguvu zote pamoja(concentration). ‘Unapoanza kufanya hatua ya kwanza ya zile hatua sita ambazo zinakuelekeza wewe’ “kukazia” katika akili yako mwenyewe kiasi kamili cha pesa unazotamani,’ endelea kushika mawazo yako juu ya kiasi hicho cha pesa kwa kuelekezea nguvu zote pamoja, au mkazo wa usikivu ukiwa umefumba macho yako, mpaka kweli utakapoona umbo halisi la pesa. Fanya hivyo angalao mara moja kila siku. Kadri utakavyokuwa ukipitia zoezi hili, fuata maelekezo yaliyotolewa katika sura ya Imani na kuona wewe mwenyewe kweli ukiwa unamiliki hizo pesa.

Huu ni ukweli dhahiri zaidi-akili ya ndani huchukua maelekezo yeyote inayopewa katia roho ya imani kamili na kufanyia kazi maelekezo hayo ingawa maelekezo mara nyingi yanapaswa kupewa tena na tena, kupitia kurudiwarudiwa, kabla hayajatafsiriwa na akili ya ndani. Zingatia uwezekano wa kucheza “mbinu” halali kamilifu kwenye akili yako ya ndani kwa kuifanya iamini- kwa kuwa unaiamini - kwamba ni lazima uwe na kiasi cha fedha  unachokiona akilini, kwamba fedha hizi tayari zinakusubiri uzichukue, kwamba akili ya ndani ni lazima  ikupe mipango ya kivitendo kwa ajili ya kupata pesa ambazo ni za kwako. Kabidhi wazo hili kwa akili yako ya ubunifu, na kuona ni nini ubunifu wako unachoweza  au utakaofanya kutengeneza mipango ya kivitendo kwa ajili ya kupata fedha kupitia mageuzi ya shauku yako.

Usisubirie mpango kamili ambao kupitia huo ndio unaokusudia kubadilisha huduma ama bidhaa kwa malipo ya fedha unazozifikiria akilini. Anza mara moja kujiona mwenyewe ukimiliki hizo pesa, ukihitaji na kutegemea wakati huohuo kuwa akili yako ya ndani itakabidhi mpango au mipango unayohitaji, kaa macho kwa hii mipango, na wakati itakapotokea, itie katika vitendo mara moja. Yamkini itamulika ghafla katika akili yako kupitia mlango fahamu wa sita, katika umbile la “wahyi”(ufunuo), ufunuo huu unaweza ukachukuliwa kama ujumbe wa moja kwa moja kutoka nguvu isiyokuwa na mipaka(Mungu). Itendee kwa heshima, na ifanyie kazi haraka mara unapoipokea. Kukosa kufanya hivi, mafanikio yako yatakuwa kazi bure.

Katika hatua ya nne kati ya sita ulifundishwa “kutengeneza mpango kamili kwa ajili ya kutekeleza shauku yako, na anza mara moja kuuweka mpango katika vitendo, unapaswa kufuata haya maelekezo katika mtindo ulioelezwa kwenye aya zilizotangulia. Usije ukaziamini fikra zako unapotengeneza mpango wako. Fikra zako zina makosa. Na zaidi kitivo chako cha kufikiri kinaweza kuwa kivivu, na ikiwa utakitegemea moja kwa moja kukuhudumia, kinaweza kikakukatisha tamaa.

Unapowaza akilini fedha unayokusudia kuipata(ukiwa umefumba macho), jione mwenyewe ukitoa huduma, au ukiuza bidhaa unazokusudia kutoa kama malipo ya hizo feha. Hii ni muhimu!.
   
Muhtasari wa mafundisho(maelekezo)
Ukweli kwamba unasoma kitabu hiki ni ishara kuwa unatafuta maarifa kwa moyo wako wote. Pia ni ishara kwamba wewe ni mwanafunzi wa somo hili. Ikiwa wewe ni mwanafunzi tu, kuna uwezekano unaweza ukajifunza mengi, lakini utajifunza tu kwa kujijengea tabia ya unyenyekevu. Ikiwa unachagua kufuata baadhi ya mafundisho lakini ukadharau ama kukataa kufuata mengine, utafeli. Ili kupata matokeo ya kuridhisha ni lazima ufuate mafundisho yote katika roho ya imani

Mafundisho yanayotolewa yakihusishwa na hatua sita kwenye sura ya 2 sasa yatafupishwa na kuchanganywa na kanuni zilizoelezwa katika sura hii.
1. Nenda katika eneo lililokuwa kimya(inapendekezwa kitandani wakati wa usiku) ambapo hautabugudhiwa au kukatishwa. Fumba macho yako na rudia wa sauti (kiasi unachoweza kusikia maneno yako mwenyewe) kauli iliyoandikwa ya kiasi cha pesa unachokusudia kukipata na maelezo ya huduma au bidhaa unazokusudia kutoa kubadilishana na pesa.

Utakapokuwa ukitekeleza haya mafunzo, jione mwenyewe ukiwa tayari unamiliki hizo pesa. Kwa mfano labda unakusudia kupata $100,000 ifikapo tarehe 1 Januari, miaka mitano ijayo na kwamba unakusudia kutoa huduma binafsi kama malipo kwa pesa hizo katika nafasi ya mwakilishi wa mauzo. Kauli yako ya maandishi ya lengo lako inatakiwa ifanane na hii ifuatayo;
“Ifikapo tarehe 1 January 20… nitakuwa namiliki $100,000 ambazo nitazipata katika viwango tofauti kutoka muda hadi muda ndani ya kipindi hicho. Kama malipo kwa fedha hizi nitatoa huduma bora zaidi ambazo naweza kuzitoa katika ukubwa na ubora wa kiwango cha juu kabisa kwa kadri inavyowezekana kama mwakilishi wa mauzo wa(taja huduma au bidhaa unazokusudia kuuza)

‘Ninaamini nitazimiliki hizi pesa . Imani yangu ni thabiti kiasi kwamba sasa naweza kuziona hizi pesa mbele ya macho yangu. Naweza kuzishika kwa mikono yangu. Sasa zinasubiri kuhamishiwa kwangu katika uwiano ninaotoa huduma ninazokusudia kubadilishana nazo. Ninasubiri mpango nitakaotumia kupata pesa hizi, na nitafuata mpango huo nitakapoupokea.

2.  Rudia programu hii usiku na asubuhi mpaka utakapoweza kuona(katika akili yako) pesa unazokusudia kuzipata.

3. Weka nakala ya kauli ya maandishi mahali unapoweza kuiona usiku na asubuhi. Isome mara kabla hujalala na wakati unapoamka mpaka inakaa akilini.

Utakapokuwa ukitekeleza mafunzo haya, kumbuka kuwa unatumia kanuni ya kujishauribinafsi kwa lengo la kutoa maelekezo  kwa akili yako ya ndani, kumbuka pia kwamba akili yako ya ndani itafanyia kazi tu  maelekezo yale yenye mhemko na yaliyokabidhiwa kwake kwa “hisia”. Imani ndiyo mhemko wenye nguvu kushinda yote na uliokuwa na faida zaidi. Fuata mafundisho yaliyotolewa katika sura ya 3.

Mafunzo haya yanaweza, mwanzoni yakaonekana ni nadharia. Usiliruhusu hili likusumbue. Yafuate vyovyote vile . Muda utafika haraka. Ikiwa utafanya kama ulivyoagizwa katika roho na pia katika vitendo, ni wakati Ulimwengu wote mpya wa nguvu utakapojifunua kwako. Kushuku kunakoambatana na mawazo yote mapya, ni tabia ya wanadamu wote. Lakini ikiwa utafuata maelekezo yaliyoorodheshwa haraka kushuku kwako kutatawaliwa na imani,  na hii matokeo yake  yatadhihirika haraka kama imani kamili.  Kisha utafika mahali ambapo unaweza ukasema kweli, “Mimi ni Bwana wa Majaaliwa yangu, mimi ni Kapteni wa Roho yangu”

Wanafilosofia wengi wametoa kauli kwamba watu wana udhibiti juu ya maisha yao wenyewe ya hapa duniani, lakini wengi wao wanashindwa kusema  ni kwa nini huwa inakuwa hivyo. Sababu ni kwanini mtu anaweza akadhibiti hali yake mwenyewe ya maisha ya hapa duniani na sanasana hali ya mtu ya kifedha  imeelezwa kwa ufasaha katika sura hii. Watu wanaweza wakaongeza udhibiti wa wao wenyewe na mazingira yao kwa sababu wana uwezo wa kushawishi akili zao za ndani, na kupitia hizo huongeza ushirikiano wa Nguvu kuu isiyokuwa na mipaka(Mungu).

Sasa unasoma sura inayowakilisha msingi wa tao la hii filosofia . Mafunzo yaliyomo ndani ya sura hii ni lazima yaeleweke na kufanyiwa kazi kwa uvumilivu  ikiwa unataka kufanikiwa katika kugeuza shauku kuwa pesa. Kitendo halisi cha kugeuza shauku kuwa pesa huhusisha matumizi ya kujishauribinafsi. Tunza wazo hili akilini, na wakati wote utakuwa na ufahamu wa sehemu muhuhimu ya kanuni ya kujishauribinafsi, ni kufanya jitihada zako kupata pesa kupitia njia zilizoelezwa katika kitabu hiki. Tekeleza maelekezo haya kama vile wewe ni mtoto mdogo. Ingiza katika jitihada zako kitu kinachofanana na imani ya mtoto mdogo. Mwandishi amekuwa makini sana kuona kwamba hamna mafunzo yasiyotekelezeka yaliyowekwa kwasababu ya shauku yenye nia njema ya kusaidia.

Baada ya kusoma kitabu kizima, rudi katika sura hii na kufuata kwa moyo na kwa vitendo hili fundisho:

SOMA SURA NZIMA KWA SAUTI MARA MOJA KILA USIKU MPAKA UNASHAWISHIKA KABISA KWAMBA KANUNI YA KUJISHAURIBINAFSI NI DHABITI, KWAMBA ITAKUKAMILISHIA YALE YOTE YALIYODAIWA KWAKE. UTAKAPOKUWA UKISOMA, PIGIA MSTARI KWA PENSELI KILA SENTENSI INAYOKUVUTIA ZAIDI.

Fuata maelekezo haya na yatafungua njia kwa uelewa kamili na umahiri katika kanuni za mafanikio.

…………………………………………………………………………
Na huo ndio mwisho wa sura hii ya 4, tukutane tena Sura inayofuata ya 5 ya kitabu hiki cha pesa na mafanikio mashuhuri kupita vitabu vingine vyote vilivyowahi kuandikwa Duniani na mwandishi yeyote yule.

Ukihitaji pia vitabu vya kiswahili vya biashara na ujasiriamali, namna ya kuandaa mpango wa biashara yako, jinsi ya kufanikia katika biashara yeyote ile ya rejareja na njia ya uhakika ya kujipatia kipato cha ziada nje ya shughuli zako za msingi, wasiliana na sisi kwa simu 0712 202244 au bonyeza>>> hapa kwa maelezo zaidi.


1 Response to "HATUA 6 + KANUNI YA KUINGIZA KIASI CHOCHOTE CHA PESA UNAZOTAKA MAISHANI"