ELIMU YA FEDHA PEKE YAKE HAITOSHI KUKUPA UWEZO KIFEDHA, KUNA VITU VINGINE (4) MUHIMU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ELIMU YA FEDHA PEKE YAKE HAITOSHI KUKUPA UWEZO KIFEDHA, KUNA VITU VINGINE (4) MUHIMU

mjasiriamali akihesabu pesa zake

Siku hizi elimu ya fedha imekuwa ikitolewa sehemu nyingi hasa baada ya mitandao ya kijamii kutawala nafasi kubwa iliyokuwa hapo awali ikishikiliwa na majukwaa au vyombo vya habari(media) mbalimbali vilivyozoeleka siku nyingi mfano vitabu, majarida, Tv, redio na magazeti. Mtu kuwa na uwezo wa kifedha na mtu kuwa na elimu ya fedha ni vitu viwili tofauti ingawa cha kwanza kinategemea sana hicho cha pili.

Kuwa na uwezo wa kifedha ni mjumuiko wa vitu zaidi ya kimoja(vipo vitu vikubwa vipatavyo vitano 5, elimu ya fedha ikiwa ndio namba moja). Mtu anapokosa kimoja kati ya vitu hivi vitano basi na ujue mtu huyo hawezi kuufikia uwezo kamili wa kifedha unaohitajika mtu awe nao ili aweze hatimaye kuwa huru kifedha. 

Uwezo wa kifedha hapa namaanisha ni ule uwezo wa mtu kusimamia kivitendo masuala yake ya kifedha huku akipiga hatua za kimaendeleo na wala simaanishi utajiri ingawa hali hii ndiyo inayoweza kumfanya mtu hatimaye kuwa tajiri.

SOMA: Kama fedha haijawahi kuwa rahisi kupatikana kwanini uchezee pesa?

Watu pasipo kujua tumekuwa tukiweka msisitizo mkubwa katika kujifunza elimu na ujuzi wa fedha, kitu ambacho siyo kibaya ni muhimu lakini tunasahau kuwa kuna vitu vingine vinne (4) sambamba nayo ambavyo navyo vina umuhimu wa kipekee katika kumfanya mtu aweze kumiliki uwezo kamili wa kusimamia masuala yake yote ya kifedha kwa ukamilifu.

Na hii ndio sababu kubwa ni kwanini watu wengi hulalamika kutokuona matokeo chanya ya kivitendo baada ya kujifunza elimu ya fedha. Nimekutana na swali hili kutoka kwa wasomaji wangu wengi wakilalamika wamesoma makala za fedha muda mrefu, wengine miaka miwili, mitatu, mpaka  mitano lakini hali zao kifedha zimeendelea kubakia vilevile zilivyo.

SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha

Kuwa na uwezo kifedha siyo tu suala la ni nini unachokifahamu bali pia ni utashi uliokuwa nao, kujiamini na fursa ya kutia katika vitendo kile unachokifahamu. Hivyo tunaweza tukauelezea uwezo wa mtu kifedha kwa maneno machache yafuatayo kabla sijayataja mambo hayo mengine manne sambamba na elimu yenyewe ya fedha.

Maelezo hayo yanatoa ufafanuzi wa kina zaidi kuliko maelezo yale ya kawaida tuliyozowea ya elimu ya fedha ambayo yanalenga tu eneo dogo kuhusiana na kupata ujuzi na mbinu mbalimbali za kifedha kama vile kufuatilia matumizi, uwekaji akiba, kuweka rekodi ya mapato na matumizi nk. 

Ijapokuwa mambo hayo ni muhimu katika kujenga uwezo wa mtu kifedha lakini yanashindwa kuelezea nguvu ya utashi au hamasa ya kutenda pamoja na vikwazo vinavyozuia mtu kutenda.

SOMA: Njia 7 unazotumia kubana matumizi lakini kumbe zinakuzidishia tu umasikini

Kuna watu wamekariri mbinu na mikakati yote ya kifedha iliyozoeleka lakini bado wana ‘struggle’ kukamata pesa halisi mkononi, Je, ni vitu gani hivyo walivyokosa?  Ungana na sisi leo tarehe 22/07/2021 saa 3 usiku  katika MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE uweze kufahamu kwa kina vitu hivyo. Pamoja na masomo mengine zaidi ya 70 yaliyopita, yote unaweza kuyadownload katika channel yetu ya telegram bure kwa mwaka mzima.

Kujiunga na group & channel yetu, lipia ada ya mwaka(miezi 12) Tsh. 10,000/= kupitia namba 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo,  kisha tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE MASTERMIND GROUP & CHANNEL-2021”  Nitakutumia Vitabu na michanganuo kisha kukuunganisha muda huohuo. *Offa ya vitabu na michanganuo ni ya muda mfupi.

NB: Hakikisha una account ya Watsap na Telegramu, lakini pia hata kama hauna bado unaweza kupata kila kitu kupitia e-mail yako, nijulishe mapema nikupe utaratibu.

Masomoya liyohifadhiwa katika channel yetu ni mchanganyiko wa elimu ya msingi ya fedha kamili (full basic financial education) pamoja na elimu ya juu ya fedha(Advanced financial education) Hivyo ni wewe mwenyewe unachagua ujifunze masomo yapi, ila ni vizuri ukajifunza yote kwa kuanza na yale basic kisha advanced.

0 Response to "ELIMU YA FEDHA PEKE YAKE HAITOSHI KUKUPA UWEZO KIFEDHA, KUNA VITU VINGINE (4) MUHIMU"

Post a Comment