KARIBU KWENYE SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO BUNIFU WA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU CHOTARA (KUROILER) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KARIBU KWENYE SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO BUNIFU WA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU CHOTARA (KUROILER)

Kuku kuroiler

Hii ni Semina ya siku 5 inayoendeshwa ndani ya group maalumu la Semina bunifu za michanganuo ya biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida. Tunakuwa na madarasa kila siku usiku kwa kipindi chote cha msimu wa kuku. 

Walengwa ni wajasiriamali wote walio na nia ya kujua jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara zao, wanaofanya miradi ya ufugaji wa kuku pamoja na mtu yeyote yule mwenye kiu ya kujifunza jinsi ya kutumia ubunifu katika biashara na ujasiriamali kwa nia ya kukuza mtaji haraka

Mkufunzi ni mwandishi na mtaalamu wa michanganuo, Mr. Peter Augustino lakini pia huwa tunashirikiana na wataalamu wengine mbalimbali;

MALENGO YA SEMINA

1.   Kuwajengea wajasiriamali Ubunifu na mbinu mbalimbali zitakazowawezesha wapate faida kubwa na haraka katika miradi yao ya ufugaji wa kuku

2.   Kuwafunza wajasiriamali jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara zao

3.   Kuwapa wajasiriamali ujuzi wa kutambua gharama na faida halisi za miradi yao ya kuku kabla hata ya kuanza

4.   Kushirikishana na wajasiriamali wengine maarifa na taarifa mbalimbali za ujasiriamali hasa katika sekta ya ufugaji wa kuku.

RATIBA YA SEMINA

1. SEHEMU YA KWANZA:

(Maandalizi)


2. SEHEMU YA PILI 

 (Muhtasari, Bidhaa & Biashara)

 

3. SEHEMU YA TATU 

(Soko, Mikakati & Utekelezaji

 

4. SEHEMU YA NNE 

(Uendeshaji, Uongozi na Wafanyakazi

 

5. SEHEMU YA TANO 

(Fedha & Viambatanisho)

 

JINSI YA KUJIUNGA

Mshiriki anapaswa kuwa na vitu 2 muhimu kabla ya kuanza semina; Kitabu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali pamoja na Mchanganuo wa kuku 300 wa Kuroiler uliokuwa tayari kwa ajili ya marejeo na kufuatilia wakati wa semina. Vitu hivi gharama yake ni shilingi elfu 10 tu ambayo hulipwa kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo.

Mara baada tu ya malipo tunakutumia vitu hivyo mara moja pamoja na Bonus/Offa ya Michanganuo mingine mbalimbali 6 kama ifuatavyo;

1.   Mchanganuo wa kuku wa nyama( Tumaini Broilers)-kiingereza

2.   Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

3.   Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-kiswahili

4.   Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

5.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

6.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) -kiswahili

Ni hiyari yako kuendelea kubakia kwenye Mastermind Group letu kwa ajili ya masomo zaidi ya fedha, michanganuo na mijadala itakayochochea zaidi ubunifu na roho ya ujasiriamali (Mentorship)

0 Response to "KARIBU KWENYE SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO BUNIFU WA BIASHARA YA UFUGAJI WA KUKU CHOTARA (KUROILER)"

Post a Comment