NI SIRI KUBWA WALIOFANIKIWA HUITUMIA LAKINI WENGI BADO HATUIJUI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI SIRI KUBWA WALIOFANIKIWA HUITUMIA LAKINI WENGI BADO HATUIJUI

Nelson Mandela na Muhammad Ally

Hivi umewahi kujiuliza ni kwanini watu wengi huwa tunafahamu fika siri, njia, mbinu na mikakati yote ya mafanikio lakini bado tu tumekuwa tukishindwa kuyafikia mafanikio tunayotamani tuwe nayo. Kufuatia mapinduzi makubwa  kwenye zama hizi za taarifa, siri kubwa walizotumia waliofanikiwa karibu katika kila nyanja hapa duniani zinajulikana.

Katika makala hii tutakwenda kufahamu kile hasa kinachotuzuia tusiitumie siri hiyo ingawa tayari tunaifahamu.

SOMA: Kumbe Nelson Mandela alikuwa mpenzi wa vitabu vya Mafanikio

Kuna watu wengi mashuhuri Duniani na hata hapahapa Tanzania waliowahi kuitumia siri hii na ikafanya kazi vizuri sana kwao, mtu kama Eric Shigongo ikiwa uliwahi kufuatilia makala zake utakubaliana nami kuwa aligundua na kuitumia siri hiyo. Lakini pia kuna watu kama kina Ophrah Winfrey, Muhammad Ally, Nelson Mandela, Kelvin Kiptum, Magic Johnson na wengineo wengi.

Yamkini kwa miaka mingi umekuwa ukijifunza njia nyingi za mafanikio katika maisha, siri ya pesa, ujasiriamali na siri nyingine lukuki za kufanikiwa kibiashara lakini cha kustaajabisha imekuwa vigumu mno kwako kuyatia hayo kwenye vitendo kusudi uweze kupata matokeo tarajiwa

SOMA: Muhammad Ali, uvumilivu, nidhamu, ujasiri, msimamo vilimpa ubingwa Kinshasa Zaire 

Katika blogu na makala zangu kwenye mitandao ya kijamii nimekuwa nikifundisha wajasiriamali mbinu na mikakati bora kabisa ya kuzikuza biashara zao zifike viwango vingine pamoja  na njia za mafanikio katika maisha lakini bado wapo wengine pamoja na kujifunza yoote hayo wanaendelea tu kuhaha huku na kule wakisaka dawa ya mafanikio katika biashara zao. Shida ni nini hasa?

MTAZAMO WA AKILI (MINDSET)

Hili ndilo jibu lake: Tunafahamu kila kitu cha kufanya ili tufanikiwe lakini hatufanyi kwa sababu mitazamo ya akili zetu haiwezi kuturuhusu tufanye hivyo, inatuvuta nyuma. Siri kubwa waliofanikiwa huitumia wengine hatuijui ni kujenga  Mtazamo chanya wa akili (Positive mindset)

Kwani mtazamo wa akili (Mindset) ni kitu gani hasa?

Mindset kwa maana rahisi kabisa ni jinsi mtu anavyofikiri. Ni imani au maoni ya mtu aliyojengewa tokea utotoni juu yake mwenyewe na vitu vingine mbalimbali vinavyomzunguka. Imani hii ndiyo huamua kufanikiwa ama kufeli kwake. Huathiri namna anavyofikiri, anavyojihisi na tabia yake kwa ujumla.  

SOMA: Imani, mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa

Aina 2 za Mtazamo wa akili

Kuna aina mbili za mtazamo wa akili, Mtazamo chanya wa akili(+) na Mtazamo hasi wa akili (-) Kwa walio na mtazamo chanya wa akii wanaamini mambo mbalimbali yanawezekana wakati walio na mtazamo hasi huamini karibu kila jambo ni mkosi haiwezekani kulifanya kirahisi.

Jinsi ya kubadilisha mtazamo wako wa akili

Kwa bahati njema sana Mwenyezi Mungu ameweka njia ya walio na mitazamo hasi ya akili kuwa na uwezo wa kurekebisha mitazamo yao na kuwa na mitazamo chanya. Kuna njia mbalimbali unaweza ukazitumia kurekebisha mtazamo wako wa akili lakini mimi hapa napendekeza njia zilizotajwa kwenye kitabu kilichoandikwa na Napoleon Hill, Think & Grow Rich (FIKIRI & UTAJIRIKE)

SOMA: Vipaji, uwezo, akili ni vitu tunazaliwa navyo au kujifunza?

Kama jina la kitabu linavyosadifu, kitabu hiki kwa asilimia kubwa kinazungumzia jinsi mtazamo wa akili wa mtu unavyoweza kumsaidia kufanikiwa au kutokufanikiwa katika nyanja aitakayo maishani iwe ni katika pesa, mahusiano, masomo, kiroho nk. Napoleon Hill anataja njia ya Kujishauri-binafsi (Autosuggestion) katika sura ya 4 kama njia kuu ya kurekebisha mtazamo hasi wa akili kuwa mtazamo chanya wa akili kupitia kitendo cha kukariri ama kurudiarudia kujiambia maneno chanya yanayoweza hatimaye kuchukua pahala pa maneno hasi uliyopandikiziwa tangia utotoni au siku za nyuma.

Mbinu hii hutumiwa pia hata na Wahubiri wa dini katika imani mbalimbali siku hizi, sijui kama huipata kwenye vitabu vya imani zao ama wanaichukua kutoka vitabu vya kawaida kama hiki cha Napoleon hill, lakini inafanya kazi kwao pia.

Utamsikia kiongozi wa dini au madhehebu flani akiwahimiza waumini wake kukariri maneno kwa mfano anaweza kurudiarudia maneno, “Pokea muujiza, pokea gari” mara nyingi kiasi kwamba muumini huamini kweli anamiliki kitu mfano gari, pesa nk. mtazamo huu anaojengewa muumini hatima yake unatengeneza njia na mipango itakayomwezesha kweli kumiliki gari au kitu alichoaminishwa kukipata.

Soma vizuri sura zifuatazo kubadiliisha mindset yako;

Sura ya pili (SHAUKU)-“Hatua 6 za kubadilisha shauku yako kuwa katika kipimo halisi cha fedha”,

Sura ya 4 (KUJISHAURIBINAFSI)- “Hakuna mawazo yawe ni chanya ama hasi, yanayoweza kuingia akili ya ndani bila msaada wa kanuni hii ya kujishauri-binafsi”

Sura ya 14 (MLANGOFAHAMU WA 6)Kuitisha mikutano ya kufikirika na kundi la washauri wasioonekana

Kwahiyo unapokuwa na mtizamo sahihi wa akili ni suala la muda tu, hakuna kitakachokuzuia kutoboa kwani njia ya kufanikiwa kwako ni nyeupe pee kama theluji.

................................

Makala yetu iliyopita tulizindua kaulimbiu ya mwaka huu isemayo; UBUNIFU NA AKILI BANDIA, VITUMIE KUIBOOST BIASHARA YAKO IFIKE VIWANGO VINGINE. Nikiwa na maana kwamba 2024 tuta-focus zaidi kwenye vitu hivi 2 katika kuzifanya biashara zetu kupiga hatua kubwa na kwa haraka zaidi.

Kwa mantiki hiyo tumeanza pia kwenye MASTERMIND GROUP letu la watsap semina za kuandaa Michanganuo bunifu ya biashara zinazolipa haraka. Siku ya Jumatatu ya tarehe 25 saa 3 usiku tutaanza semina ya kuandika Mchanganuo bunifu wa Biashara ya ufugaji wa kuku Chotara (300) aina ya Kuroiler

Kwa kuwa focus yetu kubwa ni UBUNIFU, katika mchanganuo huu tofauti na michanganuo mingi ya miradi ya ufugaji wa kuku uliyowahi kupitia, huu tumeonyesha ubunifu wa kipekee kabisa ambapo mtu anatengeneza faida kubwa ndani ya kipindi kifupi sana.

Ufugaji wa kuku ni miradi inayopendwa sana na watu wengi nchini kutokana na urahisi wake lakini pamoja na hivyo watu hujikuta wakivunjika mioyo baada ya kukuta kumbe siyo rahisi kivile kupata faida ya uhakika kama inavyodhaniwa. Kuna changamoto kubwa ambazo kama mtu hujawa mbunifu utaiona biashara ya kufuga kuku kama ni bishara ya faida kidogo sana au kwaajili tu ya kitoweo cha Idi na Krismasi

Tafadhali fuatilia makala zetu siku hizi 2 kujua yatakayokuwemo katika semina hiyo, ratiba na muda wa kumalizika.

JINSI YA KUJIUNGA NA SEMINA HII

Tiketi ya kushiriki semina unapaswa kuwa na mchanganuo kamili wa kuku wa nyama aina ya kuroiler ambao tayari tumekwishauandaa pamoja na Kitabu chetu cha Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali. Ili kupata vitu hivi unalipia shilingi elfu 10 tu badala ya sh. Elfu 20

Mchanganuo wa kuku chotara wa nyama utakuwezesha kufuatilia semina yetu kwani tutauandika upya hatua kwa hatua. Kitabu ni kwa ajili ya marejeo ya kanuni mbalimbali za uandishi wa Michanganuo ya Biashara za aina mbalimbali.

BONUS

Mbali na michanganuo 10 iliyoko ndani ya kitabu lakini pia utapata papo hapo bure michanganuo ifuatayo isiyo ndani ya kitabu na yenye thamani ya sh. elfu 60;

1.   Mchanganuo wa kuku wa nyama( Tumaini Broilers)-kiingereza

2.   Mchanganuo wa kuku wa nyama (Tumaini) -kiswahili

3.   Mchangauo wa kuku wa mayai (Mayai Bora Project)-swahili

4.   Mchanganuo wa Matikiti maji (Kibada watermelon)-kiswahili

5.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant)-kiingereza

6.   Mchanganuo wa Mgahawa wa chakula (Jane Restaurant) -kiswahili

Kujiunga lipia sh. 10,000/= kwa namba 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe usemao; “NIUNGE SEMINA BUNIFU YA KUROILER”

Utatumiwa kila kitu muda huohuo na kuunganishwa Mastermind group la MICHANGANUO-ONLINE


UPEKEE WA GROUP LA MWAKA HUU

Ukishamaliza semina una hiyari ya kuendelea kubakia katika MASTERMIND GROUP letu kwa ajili ya masomo ya kila siku ya fedha na Michanganuo pamoja na mentorship

Tofauti na magroup ya miaka iliyopita hili tumetumia mtindo uliopendekezwa na Napoleon Hill katika kitabu cha Think and Grow Rich, Sura ya 10 (NGUVU YA USHIRIKA) au The Power of Mastermind -“ushirikiano wa maarifa na juhudi katika roho ya masikilizano kati ya watu wawili au zaidi kwa ajili ya kufikia lengo kamili”

 

VITABU ZAIDI NA HUDUMA TUNAZOZITOA

·      Ukitaka kitabu cha Think & Grow Rich nakala ya Kiswahili tembelea mtandao huu hapa>>GETVALUE na ukifuata taratibu zote utakipakua kwenye simu janja yako.

·      Kwa vitabu vyetu vingine vyote ukilipia tu tunakutumia kupitia simu au kompyuta yako muda huohuo, Cheki ushuhuda kwa mteja wa kitabu cha SIRI YA MAFANIKIO YA DUKA LA REJAREJA HAPA alvyonunua nakala yake na kutumiwa muda uleule.

·      Tunatoa pia huduma ya kuandika Mchanganuo wa biashara yeyote ile kwa gharama rafiki. Wasiliana nasi tuweze kufanya kazi pamoja: call/watsap: 0712202244 au 0765553030

 

 

0 Response to "NI SIRI KUBWA WALIOFANIKIWA HUITUMIA LAKINI WENGI BADO HATUIJUI"

Post a Comment