Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi.

kuku wa kienyeji
Ukiachilia mbali ufugaji wa kuku ule wa mazoea wa kujenga afya ambao mtu huokota yai moja, mawili au matatu kwa siku na kuchinja jogoo siku ya sikukuu za Iddi, Pasaka au Krismasi peke yake, wale wanaoamua kufanya biashara ya kufuga kuku kwa dhati, wawe ni kuku wa kienyeji, kuku wa mayai wa kisasa, kuku wa nyama(broiler) au hata kuku chotara kama vile kroiler hutumia njia na mbinu mbalimbali nyingine zikiwa ni za kitaalamu na nyingine hata za kienyeji lakini zenye uwezo wa kuleta faida.


Ufugaji wa kuku  tangu vifaranga wa siku moja mpaka wanataga au kuuzwa kwa ajili ya nyama una gharama mbalimbali lakini gharama iliyokuwa kubwa kuliko nyingine zote ni ile ya chakula. Gharama za chakula cha kuku huchukua asilimia 70% mpaka asilimia 75% ya gharama zote. Hivyo unapozungumzia upunguzaji wa gharama za utunzaji wa kuku ni lazima uanze na gharama kwa upande wa chakula. Fursa au njia nitakazozitaja hapa chini mtu anaweza akachagua kutumia zile atakazoona zinafaa kulingana na mazingira yake anayofugia kuku na wala siyo lazima mtu azitumie zote.

1.Kujitengenezea chakula cha kuku mwenyewe.
Unapoamua kuchanganya chakula cha kuku mwenyewe nyumbani, ni lazima kwanza ufahamu uwiano  sahihi(ratio) wa viambato(malighafi) mbalimbali zikiwemo nafaka zinazotumika kutengenezea mchanganyiko huo wa chakula cha kuku. Kanuni ya kuchanganya vyakula vya kuku siyo hesabu ngumu sana na mtu yeyote yule anaweza akaitumia ikiwa atapata maelekezo vizuri.


Kwa kawaida kuku kama walivyokuwa viumbe hai wengine kiafya wanahitaji makundi yote muhimu ya vyakula, wanahitaji wanga na mafuta kwa ajili ya kutia joto na nguvu, Protini kwa ajili ya kujenga miili yao na Vitamini na Madini kwa ajili ya kuwalinda na magojwa.Vile vile wanahitaji maji safi ya kunywa. Kwa hiyo unapofahamu uwiano wa vitu hivi na ukachanganya chakula chako katika hali ya usafi unaotakiwa utajikuta ukipunguza gharama za ulishaji kuku wako kwa zaidi ya asilimia 50% ya bei ya vyakula kama hivyo madukani.

Kuna teknolojia moja rahisi sana na yenye faida kubwa ambayo mbegu za nafaka huoteshwa kwa kutumia maji bila udongo kabisa na baada ya siku nne zinapokua zimemea zinakuwa zinaongezeka uzito karibu mara 7 ya uzito wake wa awali. Majani haya ni chakula kizuri sana cha kuku na hata ndege aina nyingine na mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo.

3.Uzalishaji wa minyoo, funza, mchwa na azola.
Wadudu hawa na aina ya mimea iitwayo Azola huweza kuzalishwa kwa wingi kwa kutumia teknolojia rahisi sana mfano kama funza unaweza ukatumia damu ya wanyama kama vile ng’ombe, ukaiozesha katika chombo kama ndoo kwa siku chache mpaka funza watakapozaana na kukua kisha unawasuuza kwa maji safi tayari kwa ajili ya kuwalisha kuku wako. Mchwa nao ni hivyohivyo unategesha kivutio cha mchwa karibu na eneo wanakopenda kupita, wakishajaa pale unatifua na kulisha kuku wako.


4.Kulisha kuku mabaki ya vyakula.
Unaweza kutumia mabaki ya vyakula nyumbani kwako lakini pia kama kuna sehemu nyingine mfano mashule, mahospitali, mahoteli au taasisi yeyote ile wanakopika vyakula vingi kila siku unaweza ukajenga nao ukaribu  wakawa wanakupa mabaki ya vyakula. Lakini vyakula hivyo hakikisha vinakuwa havijaanza kuharibika au kutengeneza kuvu kwani vinaweza kuwadhuru kuku wako kutokana na sumu au magonjwa.

5.Lisha kuku wako huria.
Kana unalo eneo la kutosha na ambalo unaweza kuweka uzio wa kuzuia wanyama na wadudu hatari wanaokula kuku, unaweza kuwaachia kuku wako wakajitafutia chakula wenyewe katika eneo la wazi kama wafanyavyo wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji.


6.Lima mazao ya nafaka, mbogamboga na matunda
Pia hii ni kama unalo eneo au unaishi maeneo ya kijijini.Ukilima mwenyewe vyakula hivi utakuta gharama ya kuwalisha kuku wako inakuwa chini sana na faida inapanda juu. Kwa mfano ufugaji wa kuku wa mayai, ufugaji wa kuku wa nyama na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mfugaji anayetumia majani mabichi kulisha kuku wake kama chalula cha ziada anaweza kupata faida nyingi hasa katika upande wa gharama za madawa kwani kuku hawaugui ovyoovyo na mayai huwa na kiini cha njano jambo linalovutia wateja wengi kuyanunua.

7.Chagua aina ya kuku wanaokula chakula kidogo na usilishe kuku wako kupita kiasi.
Waatu wengi hudhani kwamba kuku wanatakiwa wale mpaka wasaze, hii siyo sahihi. Ukishawapa kuku kiasi kile cha chakula wanachostahili kupewa kwa siku basi usiongeze zaidi ya hapo. Vile vile punguza kuku waliozeeka na ambao utagaji wao ni hafifu.


Njia nilizozitaja na nyinginezo ambazo pengine unaweza kuwa unazijua ndizo wale wote unaowaona wakifuga kuku  bila kuacha huzitumia kila siku  na kushangaa wanapatajepataje faida na wala hakuna muujiza mwingine wowote ule.

……………………………………
Ndugu msomaji, karibu ujiunge na group letu la whatsap, mle tunajifunza kila siku masomo mbalimbali ya ujasiriamali na mzunguko wa fedha ikiwemo michanganuo ya biashara mbalimbali kama vile michanganuo ya kuku aina zote.

Kiingilio ni shilingi elfu 10, na unapata, kifurushi cha michanganuo ya kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACK), na vitu vingine vingi kama kitabu cha Michanganuo na Ujasiriamali na semina za mara kwa mara. Unakuwa pia mwanachama wa kudumu bila kulipa zaidi.

Namba za kulipia ni 0712202244  au 0765553030 na baada ya malipo tuma ujumbe wa kawaida au wasap kwa namba 0765553030 usemao; “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

Somo la leo tarehe 10 October usiku saa 3 ni hili lifuatalo;

“RASILIMALI 2 ADIMU ZAIDI DUNIANI KULIKO DHAHABU NA ALMASI NA JINSI YA KUZIPATA”   

Usikose somo hili muhimu.


0 Response to "Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi."

Post a Comment