JINSI YA KUGEUZA MSHAHARA WAKO KUWA MASHINE YA KUTENGENEZA PESA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUGEUZA MSHAHARA WAKO KUWA MASHINE YA KUTENGENEZA PESA

MTAMBO WA KUTENGENEZA PESA

Kuna baadhi ya watu wasiojua ukweli wa mambo ulivyo, wanapotoa maoni yao juu ya kazi ya ajira utawasikia wakiilaumu na kuifanya ajira kana kwamba haifai kabisa, inamfanya mtu kuwa mtumwa maisha yake yote na hata wakati mwingine wanafikia hatua ya kutoa viapo kuwa hawatakaa maisha yao yote waajiriwe.

Lakini wasichokijua watu hawa ni fursa ya ajabu iliyojificha nyuma ya ajira au kazi ya kulipwa mshahara. Hawajui kama ajira inaweza kuwa daraja bora kabisa linalowezesha kumvusha mtu mahali ambapo ingelimchukua muda mrefu sana akihaha (hustling) huku na kule akisaka mtaji kwa ajili ya kuwekeza katika vitegauchumi vingine.

Jana kwenye darasa letu ndani ya kundi la MICHANGANUO-ONLINE nilitoa somo lililokuwa na kichwa cha habari, Ili mtu afanikiwe kifedha anatakiwa kuwa na mifereji mingapi ya kipato? Katika somo hili pia kulikuwa na swali jingine lililouliza ikiwa mtu mwenye ajira nzuri inayomlipa mamilioni ya pesa kama kuna umuhimu wowote ule wa yeye kumiliki mifereji mingineyo ya kipato. Majibu kwa swali hilo niliyatoa ndani ya somo hilohilo na kwa kweli ikiwa na wewe ni miongoni mwa wale wanaolaani kazi za ajira basi majibu hayo nadhani yanaweza yakakuacha midomo wazi.

Kwani mashine ya kutengeneza pesa ni kitu cha namna gani?

Kabla ya kulijua hilo hebu kwanza tuone Mashine ni nini? Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu, mashine ni kitu chochote chenye uwezo wa kurahisisha kazi. Unatumia juhudi kidogo kupata matokeo makubwa zaidi. Tuchukulie mfano wa gari, ukiambiwa utoke Dar mapaka Morogoro ukitembea kwa miguu ni kazi ngumu kwelikweli, lakini kwa kutumia gari inakuchukua muda mfupi sana. Gari ni aina ya mashine na juhudi kidogo unayotia pale ni nauli yako tu.

Hivyo mashine ya kutengeneza pesa haina tofauti na gari tuliloona hapo juu, unaweka pesa kidogo kupata pesa nyingi ndani ya muda mfupi tena hata pasipo kufanya kazi yeyote ya ziada zaidi ya nauli yako uliyotoa, hakuna atakayekuambia njoo ukasukume gari limekwama matopeni labda tu itokee bahati mbaya sana limeharibika.

Katika makala nzima hii wala dili siyo mashine yenyewe ya kutengeneza pesa bali kitu cha muhimu zaidi ni jinsi gani mtu unavyoweza kugeuza mshahara kuwa mashine ya pesa (mchakato mzima), watu wengi hujaribu na kuishia katika pointi hii. Sasa kaa tayari kabisa nitakwenda kukuelezea ‘exactly’ ni nini cha kufanya (Hatua 4 muhimu sana) ili kuondoa kizuizi hiki na hatimaye kumiliki mashine yako mwenyewe ya kutengeneza pesa itakayoamua mustakabali mzima wa maisha yako ya baadae.

Je ungependa kuzijua hatua (njia) hizo na kuanza kuzifanyia kazi mara moja? Basi ungana na mimi leo hii tarehe 24/01/2023 saa 3 usiku katika somo hili zima ndani ya MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP kwa kiingilio cha shilingi elfu 10 tu kwa mwaka mzima. Ndani ya group utakutana na masomo mengine yaliyopita zaidi ya 80 usiyoweza kuyapata mahali kwingine kokote nje na ndani ya mtandao.

Na ikiwa utapenda na  “OFFA YETU ISIYOWAHI KUTOKEA” inayokaribia kumalizika muda wake hivi karibuni, basi ukishalipia kiingilio chako sh. elfu 10 nitumie ujumbe Wasap au SMS ukisema; “NATAKA NA ILE OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA” Ndani ya dakika 3 mpaka 5 nitakuwa nimeshakutumia offa zako zote pamoja na kukuunganisha Mastermind group tayari kwa masomo ya fedha kila siku na michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa.

Namba zetu ni; 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo


............................................................

VITU VYA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA NI HIVI VIFUATAVYO;-

KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali

KITABU: Siri ya Mafanikio ya Biashara Duka la Rejareja

KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa

KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE

KITABUNjia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30

MCHANGANUO: Kuku wa mayai

MCHANGANUO: Kuku wa nyama - kwa kiswahili

MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

MCHANGANUO: Kuku wa kienyeji

MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji

MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa Kiswahili

MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula –kwa kiingereza

MCHANGANUO: Kiwanda cha Dona (Usado milling)

SEMINA: Jinsi ya kuandika mchanganuo wa kiwanda cha unga

SEMINA: Kuandika mchanganuo wa kuku wa nyama

MCHANGANUO: Kuandika mchanganuo wa Cafe


1. Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?

2. Ajira siyo laana, ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji

3. Kwanini biashara humpa mtu uhuru zaidi wa kifedha kuliko ajira?

4. Kwanini kama huipendi ajira yako bado unaendelea kuifanya?


0 Response to "JINSI YA KUGEUZA MSHAHARA WAKO KUWA MASHINE YA KUTENGENEZA PESA"

Post a Comment