Hakuna shaka kwamba kila binadamu angetamani
siku moja aje kuufikia uhuru kamili wa
kifedha, kwahiyo ikiwa lengo lako kuu kwenye safari hii ya maisha ndio hilo
basi hauna budi kubadili ‘meli’
uliyopanda sasa kutoka ile ya ajira kwenda ya biashara, hili halina ubishi,
inawezekana usibadili sasa lakini ni lazima utafanya hivyo hapo baadae hata baada
ya kustaafu.
Katika somo letu hili leo, hiki hasa ndio
kitu tutakachoenda kujifunza. Biashara peke yake tu inaweza isiweze kukupa
uhuru kamili wa kifedha lakini ni moja kati ya viungo muhimu sana vinavyosaidia
kuharakisha kukufikisha huko.
Uwezekano wa mtu kuufikia uhuru wa kifedha
akiwa katika ajira ni mdogo ingawa hatuwezi kabisa kuuondoa uwezekano huo. Si
kama mwajiriwa hawezi kabisa kupata uhuru wa kifedha ila mchakato wake ni mrefu
na mgumu kuliko vile ilivyo kwa mfanyabiashara. Wafanyabiashara mara nyingi
sana utakuta hujiandaa kisaikolojia katika safari hii, kivipi? - tutajua zaidi
kwenye aya zinazofuata.
Katika kazi za ajira, watu wengi huishi
maisha ya wasiwasi kutokana na upungufu wa fedha. Na wala haijalishi ni
mshahara mkubwa kiasi gani aupatao mtu, mara nyingi utamkuta akibeba akilini
fikra za upungufu wa fedha. Na hili hutokea kwasababu waajiriwa wengi wanakuwa
na tabia ya kufanya matumizi mengi zaidi kushinda wenzao wafanyabiashara. Wafanyibiashara
wao mara nyingi hupenda kuwa waangalifu sana kwenye matumizi yao ya fedha.
SOMA: Fedha zako zinapotea kiajabu? Njia rahisi ya kutambua fedha zako zinakoishia kila siku hii hapa.
Kwanini
basi mfanyabiashara huwa mwangalifu sana kwenye matumizi ya pesa?
Mchakato wa biashara mpaka imetengeneza faida
unahusisha mlolongo wa vitu vingi na hivyo kumfanya mfanyabiashara kuchukua pia
hatua mapema za kujihadhari kusudi biashara isije kuanguka. Kumbuka kwenye
biashara hakuna ulinzi(security) kama
ilivyo kwenye ajira, hivyo mfanyabiashara anajua kabisa akiteleza kidogo tu
imekula kwake.
Chati hiyo hapo juu inaonyesha jinsi biashara
inavyotengeneza yenyewe fedha za ziada. Utaona ya kwamba biashara hupitia
mchakato mrefu mpaka imeweza kutengeneza fedha za ziada ambazo ndizo zinazobeba
jukumu kubwa katika zoezi la kufanikisha uhuru wa kifedha wa mfanyabiashara
kama tutakavyoona baadae kidogo.
Wakati sasa mfanyabiashara akitekeleza
shughuli mbalimbali za biashara yake ndipo anapojijengea tabia hii ya kuwa
muangalifu kupita kiasi kwenye matumizi ya fedha kusudi ahakikishe mwishoni
kunakuwa na fedha za ziada kwa ajili ya kuzirudisha tena kwenye biashara kama
mtaji lakini pia kwa ajili ya kulipia gharama zake nyingine mbalimbali za
kimaisha.
KAZI/AJIRA
Hivyo ndio kusema kwamba mwajiriwa hawezi
kabisa kusimamia fedha zake vizuri mpaka na yeye akaufikia uhuru wa kifedha? Hebu tena tuangalie chati hii ifuatayo;
Kama ilivyokuwa kwa biashara, ajira nayo inaweza ikatengeneza fedha za ziada. Lakini tofauti na biashara katika ajira kunakosa muunganiko, kunakuwa na pengo kati ya ajira yenyewe(kazi) na fedha. Uthibiti wa mwajiriwa kwenye kutengeneza fedha zake za ziada umewekewa mipaka, kivipi? Kuna vitu viwili (2) vifutavyo;............
Ndugu msomaji makala hii itaendelea katia Group la Michanganuo- online leo hii. Ili kuweza kuisoma kwa ukamilifu na masomo mengine yenye maudhui ya fedha mengi yaliyopita, jiunge na group hilo pamoja na Channel yetu kwa kiingilio cha sh. elfu 10 tu mwaka mzima.
Kulipia tumia namba, 0765553030 AU 0712202244 Jina Peter Augustino Tarimo
0 Response to "KWANINI BIASHARA HUMPA MTU UHURU WA KIFEDHA ZAIDI KULIKO AJIRA?"
Post a Comment