KWANINI BIASHARA ZA MTAJI MDOGO NYINGI ZILIKUFA 2022 LAKINI CHACHE ZIKASTAWI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI BIASHARA ZA MTAJI MDOGO NYINGI ZILIKUFA 2022 LAKINI CHACHE ZIKASTAWI?

Mwanaume akisikitika biashara yake kufa

Ikiwa una matazamio ya biashara yako ndogo kukua mwaka huu ujao wa 2023 ni lazima kwanza utilie maanani ukweli huu kwamba, kuna biashara nyingi za mitaji midogo kama yakwako ambazo hazitaweza kuuona mwaka mpya wa 2023, lakini pia baadhi ya biashara hizo chache zikashamiri na kustawi licha ya kuwa zilianza kipindi kimoja.

Ni kitu gani hasa kilichosababisha biashara hizi chache kustawi ilihali nyingi zikifa? Majibu ya swali hili bila shaka yatakusaidia sana katika kuiweka mikakati ya kuiinua biashara yako ndogo ya mtaji mdogo ili hatimaye nayo iweze kufikia viwango vingine itakapokwenda kufika kipindi kama hiki mwakani kuelekea  2024.

SOMA: Hatua 7 rahisi za kuanzisha biashara yako ndogo ukiwa bado kazini umeajiriwa

Takwimu mbalimbali zilizofanyika nje na ndani ya Tanzania zinaonyesha kwamba karibu asilimia 50% ya biashara zote ndogondogo mpya hufa kila mwaka na zile zinazobakia ni chache sana zitatimiza umri wa miaka 5. Sababu kubwa nne (4) zinazopelekea vifo vya kusikitisha vya biashara hizi na njia za kukabiliana navyo ni hizi zifuatazo;-

 

1. Ukosefu wa Fedha/Mtaji

Sababu moja kubwa zaidi inayozifanya  biashara nyingi za mitaji midogo zisiweze kusheherekea birthday zao za mwaka mmoja 2023 ni ukata au kutokuwa na mtaji wa kutosha, wataalamu huita, mtaji endeshi wa biashara (working capital).

Wakati mwingine mjasiriamali anaweza akafahamu kabisa ni kiasi gani cha fedha zinazohitajika kwenye uendeshaji wa biashara yake kila siku kama vile, kulipa mishahara, kulipia gharama za kudumu na zile zisizokuwa za kudumu pamoja fedha za kununulia malighafi au bidhaa kwa ajili ya kuuza lakini shida huja pale mjasiriamali huyu anaposhindwa kujua apate wapi fedha hizo baada ya kupata fedha kidogo za kuanzia.

SOMA: Biashara ndogondogo Tanzania zenye faida ya haraka ni hizi hapa, zipo nne(4)

Wajasiriamali wengi hujipa moyo kwa kusema, “labda mauzo ya biashara yangu yatakuwa mazuri na nitapata fedha za kuendeshea biashara kutokana na hayo mauzo”. Hata hivyo ni bahati mbaya sana biashara nyingi mpya na hasa zile ndogondogo za mitaji midogo huweza kuanza moja kwa moja na mauzo ya kuridhisha, mauzo hupanda taratibu mno kiasi cha kutokumpa mjasiriamali muda wa kuendelea na biashara yake na matokeo yake ni kufungwa kwa biashara.

Kuna wakati pia mjasiriamali hushindwa kupanga vizuri bei zake na kuweka bei ya chini mno akifikiria eti ndiyo anawavutia wateja wengi zaidi waje kununua kwake kumbe ndiyo njia nyepesi ya kujimaliza mwenyewe.

SOMA: Njia rahisi ya kupanga bei ya huduma au bidhaa unayouza

Matokeo ya mkakati huu mbovu ni kwamba hataweza asilani kumudu gharama za uendeshaji wa biashara na  hujikuta anatumia fedha nyingi zaidi kuendesha biashara kuliko zile anazozipata kama mauzo. Mbinu hii inaweza kufaa tu kwa muda mfupi ila siyo endelevu.

Ingawa mjasiriamali anaweza akakopa fedha mahali, lakini biashara nyingi ndogondogo huwa hazina uwezo wa kuwashawishi wakopeshaji kutokana na kukosa mauzo mazuri, kutokuwa na dhamana za mkopo wala historia ya muda mrefu.

SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini

Suluhisho kwa tatizo hili la ufinyu wa mtaji ni kwa mjasiriamali mwenyewe kufahamu jinsi ya kubajeti fedha kidogo alizokuwa nazo ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha za kuendeshea biashara yake kabla hata hajaianza. Uelewa huu anaweza kuupata kwa kupitia kujua namna ya kuandaa mpango wa biashara (Business plan) katika karatasi au hata kichwani mwake tu inatosha.

2. Kukosekana Usimamizi mzuri wa biashara

Sababu nyingine ya biashara nyingi ndogondogo zilizoanzishwa mwaka 2022 kushindwa kufika mwaka 2023 ni wamiliki wa biashara hizo au timu nzima ya usimamizi kukosa mbinu bora za usimamizi wa biashara. Ikumbukwe kuwa biashara nyingi zile ndogo huendeshwa na kusimamiwa na wamiliki wenyewe, na mara nyingi mmiliki asipokuwa na ujuzi katika eneo fulani tuseme labda katika masoko, fedha au kuajiri basi anaweza akasababisha biashara kufeli kiurahisi.

SOMA: Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti

Suluhisho la tatizo hili ni mjasiriamali kutafuta mtu anayeweza eneo fulani yeye asilolimudu badala ya kujidai kufanya kila kitu peke yake.

 

3. Kutokuwa na Mpango wa Biashara

Biashara nyingi ndogondogo huwa wamiliki wake hawaweki uzito kwenye mpango wa biashara. Kama ninavyosisitiza kila mara kuwa mpango wa biashara siyo lazima uuandike katika karatasi ndipo ukusaidie, ukiupangilia vizuri kichwani kwako tu inatosha ilimradi ujue jinsi ya kuupangilia na vipengele vyake vyote ni nini. Ili mtu uweze kuielewa mipango ya biashara ikoje na ni vipi unaweza ukaandaa wa kwako unaweza ukasoma ‘sample’ mbalimbali zilizokwishaandikwa.

Sisi tunazo sample hizo ambazo ni michanganuo mbalimbali kamili iliyoandikwa kwa kiingereza na Kiswahili tunaweza kukupatia usome. Tuna michanganuo ya aina za biashara ndogondogo za mtaji mdogo lakini pia aina za biashara za mtaji mkubwa na wa kati zikiwemo pia na aina za viwanda mbalimbali vya kusindika vyakula na vya bidhaa nyinginezo mbalimbali

Mpango mzuri wa biashara utakuwezesha kulifahamu vizuri soko lako, sekta biashara yako ilipo pamoja na ushindani unaokuzunguka kabla hata hujaanzisha biashara yenyewe

 

4. Kukosa mikakati mizuri ya Masoko

Mkakati mzuri wa masoko unahitaji bajeti ya pesa ambazo kama tulivyokwishaona huko nyuma mmiliki wa biashara ndogo anakuwa hana na kosa kubwa tunalolifanya wamiliki wa biashara ndogo ni kuhamishia hata pesa kidogo za bajeti ya masoko zilizopo kwenda kuziba mapengo katika maeneo mengine jambo ambalo ni kosa kubwa sana la kiufundi. Hakuna kitu chenye umuhimu mkubwa kwenye biashara kushinda soko hasa ikiwa kama bado ni mpya.

SOMA: Katika vitu 3, usimamizi, soko na uendeshaji kipi ni muhimu zaidi katika mafanikio ya biashara?

Pia wamiliki wa biashara hizo wakati mwingine hushindwa kujua ni jinsi gani wakadirie soko lao, namna ya kulifikia na tabia za wateja wao kwa ujumla vitu ambavyo ni muhimu mno katika uhai wa biashara yeyote ile.

Suluhisho la matatizo yote manne 4 kwa pamoja linaweza kupatikana tu pale mjasiriamali atakapoelewa vyema jinsi ya kuipangilia biashara yake kabla na baada ya kuianza kwani kwa kila hatua ya biashara huwa ina kipengele chake kwenye mchanganuo wa biashara.

SOMA: Sababu kubwa kwanini biashara inaweza kufa hata kama ina faida nzuri tu na ya kutosha

Ninayo PACKAGE/KIFURUSHI kizima cha vitu 21, vitabu, michanganuo kamili ya biashara na masomo mbalimbali kinachomwezesha mtu yeyote yule kuelewa nje ndani Michanganuo ya biashara, jinsi ya uandaaji wake, uandishi na hata ikiwa unapenda tu kuisoma kama kujihamasisha “Inspiration” ili uweze kuiendesha na kuisimamia vyema biashara yako kwa uhakika isife.

Package hii kwa bei ya Offa kabla wiki hii haijamalizika (kwani ndiyo wiki ya mwisho) utaipata kwa kulipia shilingi elfu 10 tu ikiwa ni pamoja na kuunganishwa na group letu la masomo whatsapp na telegram (Michanganuo-online). Kwenye group pia utapata masomo mengine yote tuliyojifunza siku zilizopita.

Lipia sasa hivi kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo kisha nitumie ujumbe wa Wasap au SMS usemao;

 “NITUMIE KIFURUSHI CHANGU NA KUNIUNGA GROUP LA MASOMO”

Nitumie pia na anuani ya email na namba ya telegramu kama unayo

Ikiwa hutumii watsap wala telegramu unaweza kutumiwa offa zote na masomo kwa njia ya email.

Kumbuka hii offa inamalizika wiki hii hii muda wowote ule kwani idadi ya wanachama wanaotakiwa karibu inatimia na hata wasipotimia offa bado itafungwa rasmi.

 

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa michanganuo ya Biashara

SIMU/WATSAPP: 0712202244  au 0765553030

0 Response to "KWANINI BIASHARA ZA MTAJI MDOGO NYINGI ZILIKUFA 2022 LAKINI CHACHE ZIKASTAWI?"

Post a Comment