HATUA 11 ZA KUJINASUA KWENYE MKWAMO WA KIFEDHA (USILAUMU KUKOSA PESA.. (PART II)

kujinasua kifedha

Jana katika sehemu ya kwanza ya somo hili (Usilaumu kukosa pesa bali njia iliyokufikisha pale ulipo) tuliishia kwa kuahidi kwamba leo tungeendelea na sehemu ya pili inayoelezea hatua za kuchukua ili kuzuia mtu kujikuta katika hali ngumu ya kifedha baada ya kupita nyakati na vipindi vyenye fursa mbalimbali za kiuchumi.

Hatua hizo pia zinaweza zikachukuliwa hata na mtu ambaye tayari ameshajikuta yupo kwenye hali kama hiyo ya mkwamo mbaya wa kiuchumi katika harakati zake za kujinasua ili kuweza tena kusonga mbele. Hatua zenyewe ni hizi zifuatazo;

1. Jiwekee kinga na wale wanaokutegemea(Familia)
Kabla hujaanzisha kuwekeza au kufanya biashara hakikisha unajiwekea bima mbalimbali kama vile,bima ya maisha, bima ya matibabu na hata ikiwezekana bima kwa ajili ya nyumba na gari yako.


2. Anza Mapema.
Kuna maajabu katika kuanza jambo lolote lile mapema. Hakikisha unaanza tabia ya kujiwekea akiba kungali bado mapema iwezekanavyo. Yamkini wewe ni mwanafunzi sasa hivi na miaka yako pengine ni 20, 22, 25 nk. huu ndio muda muafaka wa kujizoesha tabia hiyo. Haijalishi pia hata ikiwa tayari umri wako umeshasonga, bado unaweza ukaanza sasa kabla muda haujakwenda zaidi kwani hi heri kuanza leo kuliko kuja kuanza baada ya tuseme miezi miwili au mitatu ijayo.

3. Omba au tafuta Msaada/Ushauri
Siyo kila mtu anao uwezo wa kupanga na kusimamia fedha zake mwenyewe inavyotakiwa. Kama katika eneo hilo unajijua haupo vizuri basi tafuta ushauri wa kitaalamu mahali au hata unaweza kujifunza mwenyewe kwa kusoma vitabu mbalimbali na kuhudhuria semina zinazohusiana na usimamizi mzuri wa fedha. Usiogope kutumia gharama kidogo kupata ushauri bora wa kifedha. Jiunge na magroup makini ya whatsapa, facebook nk.


4. Fuatilia na Kuweka Kumbukumbu za Mali na Madeni uliyokuwa nayo.
Thamani halisi ya mali zako unazomiliki utaijua kwa kuchukua thamani ya mali zote ulizonazo na kutoa thamani ya madeni yote unayodaiwa na watu au taasisi mbalibali zikiwemo zile taasisi za fedha kama vile benki, vicoba au saccos. Fuatilia na kujua pia mtiririko wako wa fedha upoje. Baadhi ya mambo haya tulishajifunza hapa katika group hili la Michanganuo-online.

5. Hakikisha biashara au Uwekezaji wako unakua na kuongezeka hata unapokuwa umelala usiku
Maana yake ni kwamba unatakiwa uhakikishe unawekeza katika biashara au vitegauchumi vilivyokuwa na uwezo mkubwa wa kurudisha fedha zako ulizowekeza. Buni mfumo wa biashara au miradi ile isiyokulazimisha kuwepo pale muda wako wote.


6. Orodhesha Matumizi yako yote ya Mwezi.
Zoezi hili litakuwezesha kujua ni wapi fedha zako zinakotumika kwa wingi kusudi uweze  kubalansi matumizi yako na kuelekeza fedha nyingi zinazotokana na mapato yako kwenye maswala yale ya msingi zaidi kama vile uwekezaji na kuweka akiba. Unaweza kuamua labda tuseme mapato yako asilimia 35 ukayapeleka katika kulipia gharama na matumizi mbalimbali, asilimia 30% kwenye kulipa madeni, asilimia 30% mpaka 32% kwenye uwekezaji na kiasi kinachobakia ukakiingiza kwenye akiba yako.

7. Mshirikishe Mwenzi wako.
Kama unaye mwenzi mshirikishe vitu mbalimbali vya msingi kama vile nywila/password muhimu za benki na za accout zako za simu kuhusiana na Madeni na mali uliyokuwa nayo kwani huwezi kujua leo na kesho kitatokea nini. Unaweza ukadondoka ghafla halafu baadhi ya mali zako nyingine zikaishia kupotea hivihivi tu ikiwa hukuchukua tahadhari muhimu kama hizo.


8. Nidhamu ya Pesa.
Hakuna njia ya mkato kwenye maisha, hakikisha fedha unazozipata kwa jasho unazitumia pia kwa umakini wa hali ya juu. Kamwe usitumie zaidi ya kile unachoweza kuingiza kama faida katika biashara zako na zaidi ni kwamba bana matumizi kusudi uweze kutimiza malengo yako ya kifedha uliyojiwekea kwanza.........

...............................................

Somo hili bado halijaisha na somo zima linapatikana kwenye Group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE. 

Unaweza kuyapata masomo yote kamili tunayojifunza kila siku kwenye group hili kwa kulipa ada/kiingilio ambacho ni shilingi 10,000/= kwa mwaka huu mzima wa 2020

Pamoja na kuwa mwanachama wa group lakini pia punde baada ya kujiunga tunakutumia vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali kwenye simu au kompyuta yako.

Namba zetu za kulipia ni 0765553030  au 0712202244 Jina Peter Augustino Tarimo

Kisha baada ya malipo tuma ujumbe wa wasap au sms ya kawaida ukisema; NIUNGE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO"

Kwa vitabu na Michanganuo zaidi Tembelea DUKA LETU LA MTANDAONI (SMART BOOKS TZ)

................................................

0 Response to "HATUA 11 ZA KUJINASUA KWENYE MKWAMO WA KIFEDHA (USILAUMU KUKOSA PESA.. (PART II)"

Post a Comment