JINSI YA KUTENGENEZA MVUTO WA AJABU NA KUPENDWA HARAKA NA KILA MTU, WAPENZI, WATEJA, NDUGU NA HATA JAMAA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUTENGENEZA MVUTO WA AJABU NA KUPENDWA HARAKA NA KILA MTU, WAPENZI, WATEJA, NDUGU NA HATA JAMAA

MVUTO KWA WATU
Kuna msemo mmoja maarufu watu hupenda sana kuutumia kwa watu wanaofanikiwa kuwavutia kwa haraka zaidi watu wengine iwe ni katika nyanja ya mapenzi, biashara kuvutia wateja na hata wale wanaopendwa zaidi na ndugu, jamaa zao au marafiki. Msemo huo watu husema hivi, “Fulani bwana si bure, yule ana kamzizi” wakimaanisha kuwa fulani ana dawa ya kienyeji inayomwezesha kuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho cha watu kumpenda haraka mithili ya sumaku.

Ushahidi kutokana na tafiti mbalimbali za kisayansi unaonyesha kwamba humchukua binadamu chini ya sekunde 30 kuamua ikiwa amempenda mtu au la. Hii ni silika ya binadamu iliyojengeka taratibu ndani ya vinasaba vyake mamilioni ya miaka yaliyopita wakati binadamu wa kale kabisa alipotaka au kuamua kujenga urafiki na wanadamu wenzake.

SOMA: Jinsi ya kupata marafiki na kuwa na ushawishi kwa watu wengine(How to win friends and and influence people)

Silika au tabia hii katika nyakati tunazoishi leo hii ndio huathiri kwa kiasi kikubwa sana mahusiano yetu binafsi baina ya mtu na mtu na hata yale ya kibiashara au ya kikazi. Maaamuzi karibu yote mtu anayoyafanya kibiashara kuanzia kile kinachomkusukuma anunue bidhaa au huduma fulani kutoka kwa mtu mwingine mpaka kufanya mkataba na mtu wa kibiashara au kazi yanategemea ni kwa kiasi gani watu hao anaofanya nao biashara/mkataba wanavyompenda au kumuamini.

Halikadhalika huwezi ukamtongoza mpenzi awe ni mwanamke au mwanaume akakukubalia hivihivi tu pasipo kwanza kukupenda na kukuamini, kwa hiyo ni lazima kwanza uhakikishe unajenga hiyo hali ya kupendwa na kuaminiwa kabla ya kupendwa kwenyewe. Kwa upande wa biashara ndio hivyo hivyo, haiwezekani mteja atoke huko tu kusikojulikana pap! na kuanza kununua bidhaa/huduma unazozitoa pasipo kwanza kukufahamu na kuifahamu vizuri bidhaa yako, aipende na ajiridhishe kweli inaaminika.

SOMA: Je wajua kitu binadamu anachopenda zaidi kuliko vyote duniani?

Sasa wataalamu wamegundua kwamba ili mtu uweze kupendwa na kuaminiwa haraka zaidi na watu wengine bila kujali ni katika mazingira yapi, mapenzi biashara au kazi, kuna vitu au vitendo ambavyo unaweza kuvifanya ili kutengeneza huo mvuto wa ajabu. Mbinu hizo ni hizi hapa chini;

1.TABASAMU:
Unaweza kufikiria kwamba hili nitendo la kawaida tu lakini hebu kumbuka kwanza siku uliyowahi kuhudhuria mkutano wowote ule wa kibiashara, maonyesho ya biashara au tamasha, unakumbuka jinsi washiriki mbalimbali walivyoonekana siku hiyo? Je walikuwa wamenuna au wametabasamu? Na kama walikuwa wametabasamu walifanya hivyo kwa bahati na sibu au ni kitendo cha kupangwa?

SOMA: Sababu nne kwanini matangazo yako ya biashara hayaleti wateja kama unavyotaka.

Kiukweli suala la kutabasamu wataalamu husema huwa halitokei tu hivihivi kwa bahati, bali ni kitendo cha kukusudia, mtu hutabasamu akiwa na malengo fulani. Kuna watu wengine hudhani labda ili waweze kuonekana ni weledi wenye kuheshimika basi wanatakiwa kuwa wakimya sana(serious) lakini ukweli wa mambo ni kwamba tabasamu dogo tu usoni huweza kukupa kila kitu, heshima, kupendwa na pia watu wavutiwe zaidi kuwa na wewe karibu.

2.KUKUTANISHA MACHO.
Kukutanisha macho yako nay a mtu mwingine maana yake ni kwamba unaaminika na huna chochote kile cha kuficha. Hakikisha lakini hufanyi hivyo kwa kujifanyisha bali inakuwa ni tabia yako uliyoizoea kula siku na muda mzuri wa kukutanisha macho yako na mtu ni pale mtu huyo anapokuwa akizungumza huku ukionyesha shauku ya kweli. Pia kutanisha macho yako nay a mtu mwingine wakati mnapokuwa mkizungumza pointi muhimu au ukisisitiza maoni yako.

SOMA: Hivi unajua ni nani anayeyadhibiti maisha yako?

3.AKISI YULE UNAYEZUNGUMZA NAE
Kuiga mkao au pozi za yule unayezungumza naye kisaikolojia kutamfanya ahisi unakubaliana nae na kupekea kile anachokisema. Kama amesimama mikono kaweka mfukoni na wewe fanya hivyohivyo. Ukikuta kaka chini  na wewe fanya hivyo pia ila usionyeshe kufanya kwa kujilazimisha, fanya kama ni kawaida yako.

4.ONYESHA SHAUKU
Kawaida ya watu hupendelea zaidi kuzungumzia mambo yale yanayowahusu wao tu, kwahiyo wewe mwache azungumze kwanza. Siyo tu itamfanya ajisikie vizuri bali pia itakupa wewe uelewa wa ni kitu gani hasa anachokifikiria akilini mwake. Na unaweza pia kumuuliza maswali yasiyokuwa na majibu ya ndiyo au hapana, kusudi aweze kufunguka zaidi kwako.

SOMA: Siri 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote lile, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala madarasa ya ujasiriamali.

5.ONYESHA SHUKRANI
Kila mtu yupo bize ana shughuli nyingi za kufanya kuliko muda aliokuwa nao, mshukuru kwa muda wake, mshukuru pia kwa kukushirikisha mawazo na maneno yake bila kusahau kumshukuru kwa kufanya biashara na wewe. Watu hupenda sana kushukuriwa, kuthaminiwa na mara zote huvutiwa na wale watu wanaoweza kuwafanya wajisikie hivyo.

……………………………………..

Ndugu msomaji, masomo yetu mengine ya Pesa yanaendelea katika lile Group la MICHANGANUO-ONLINE kila siku, Jana tarehe 27 tulikuwa na somo lisemalo,


Somo letu la leo tarehe 27 usiku ni hili hapa chini;

“KANUNI 8 ZA KUVUTIA PESA ZIJE KWAKO MITHILI YA SUMAKU”

Baada ya masomo ya ile semina ya Hesabu za michanganuo kupotea na kompyuta tunayaandaa tena upya na siku ya semina itatangazwa hivi karibuni, semina hii ni moja kati ya semina kubwa sana kuwahi kufanyika katika group hili kutokana na umuhimu wa mada yenyewe. Kumbuka sehemu inayodhaniwa kuwa ngumu kuliko nyingine zote katika mpango wa biashara ni sehemu hii ya fedha. Na kama utakumbuka kwenye malengo yetu kwa mwaka huu tulisema tutakuwa na Michanganuo mikubwa 4 kuhusiana na Uanzishaji wa viwanda. Kabla ya michanganuo hiyo tunapenda mtu ajifunze kwanza somo hili la fedha ili michanganuo hiyo iwe rahisi zaidi kwake.

Unapojiunga katika group hili moja kwa moja unakuwa na sifa ya kushiriki kila kitu kwa mwaka mzima huu wa 2019. Pia tunakupatia masomo na vitu vyote tulivyojifunza mwaka uliopita kama ifuatavyo.

1.   Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.      Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.      Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Nafasi ya kujiunga bado ipo lakini inazidi kuwa finyu kadiri siku zinavyokwenda, group lina ukomo wa idadi ya watu na itakapotimia ni basi hatutapokea tena washiriki kwa mwaka huu hivyo kama utapenda kuwa nasi 2019 nakusihi sana ujiunge mapemba.

Ukishalipa kiingilio sh. Elfu 10 kupitia namba 0765553030 au 0712202244 tuma ujumbe wa wasap au sms usemao, ‘NIUNGANISHE NA GROUP LA MASOMO’ na nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila kitu kama vilivyoorodheshwa hapo juu.

2 Responses to "JINSI YA KUTENGENEZA MVUTO WA AJABU NA KUPENDWA HARAKA NA KILA MTU, WAPENZI, WATEJA, NDUGU NA HATA JAMAA"