Una kampuni nzuri, unazalisha bidhaa bora
kabisa kupita washindani wako, unao mtaji mkubwa wa kutosha lakini unashangaa
hupati wateja wengi kama vile ambavyo ungependa iwe. Na hata unapojaribu
kufanya matangazo ya biashara katika vyombo vya habari mbalimbali bado huoni
matokeo mazuri, hamna wateja wanamiminika kuja kununua.
Matangazo ya biashara au kwa jina jingine
promosheni ni moja ya silaha 5 au tuseme nguzo za masoko ambapo soko ndiyo
kiini kikubwa cha uhai wa biashara. Silaha nyingine 4 za masoko ni Bidhaa, Bei,
Eneo na Watu, kwa kimombo, Product, Price, Place & Peple. Bila soko hamna
mtiririko chanya wa pesa kwenye biashara yeyote ile na soko ni lazima litafutwe
kwa njia ya matangazo.
Kabla hatujakwenda kuziona sababu zenyewe nne
zinazosababisha matangazo ya biashara nyingi kutokuzaa matunda yaliyokusudiwa
yaani kuleta wateja wa kutosha, hebu kwanza kwa kifupi tuone matangazo ya
biashara ni kitu gani, yanafanya kazi gani na dondoo mbili tatu kuhusiana na
matangazo ya biashara.
Kutangaza biashara maana yake ni kile kitendo
cha kuvutia hisia za watu kwenye bidhaa ama huduma unayouza katika jamii au
umma wa watu kwa lengo la kuifanya bidhaa yenyewe iuzike kwa haraka na kwa
wingi zaidi.
Tangazo ni ule ujumbe, unaweza ukawa aidha
katika mfumo wa maandishi, sauti, picha au hata video.
KAZI MUHIMU ZA MATANGAZO YA BIASHARA
· Hutengeneza
uhitaji wa kile kitu unachouza.
· Huwapa
wateja taarifa kuwa kuna mahitaji katika maisha yao yanayotakiwa kutimizwa.
· Hukusudiwa
kutoa taarifa na kushawishi tabia na mitizamo ya watu.
Ili ujumbe wa tangazo uweze kufanya kazi
vizuri, watu tofauti wanahitaji kusikia au kuona tangazo hilohilo kila mara na mara nyingi
kadiri iwezekanavyo kupitia njia tofauti.
Ni bora tangazo liwafikie idadi ndogo
kabisa ya watu lakini ujumbe mzito wa maana ufike, kuliko tangazo kuwafikia
mamilioni ya watu pasipo kufikisha ujumbe mzito wa maana.
DONDOO:
UKWELI KUHUSU MATANGAZO YA BIASHARA
· Hakuna
tangazo linaloweza kupendwa na kila mtu
· Tangazo
moja pekee kamwe halitaweza kuleta mafanikio kwa asilimia 100%
· Tangazo
hubeba taarifa na ni njia inayoweza kuwashawishi watu kubadili mitazamo yao na
tabia.
· Tangazo
la biashara litapoteza umuhimu uliokusudiwa ikiwa litatazamwa au kusikilizwa na
watu wasiokuwa walengwa au wenye chuki na bidhaa/huduma inayotangazwa
SASA
BASI SABABU HASA NNE (4) KWANINI MATANGAZO YA BIASHARA YAKO HAYALETI WATEJA NI
ZIPI?.....
………………………………………….
Mpendwa msomaji wa makala hizi, ungana na mimi leo kwenye
kundi la masomo ya kila siku la WHATSAPP la MICHANGANUO-ONLINE. Huko tunakuwa
na masomo yahusuyo fedha kila siku pamoja na Semina za mara kwa mara juu ya
namna ya kuandika Mpango wa biashara(Michanganuo ya biashara zile zilizo na
uwezo mkubwa wa kuzalisha faida)
Ili kujiunga na Group hili kuna kiingilio/ada
ya shilimgi elfu 10(10,000) na mara tu mtu anapomaliza kulipa huwa
tunamuunganisha papo hapo na Group ikiwa ni pamoja na kumtumia masomo na semina
zote zilizopita tangu January, Vitabu na michanganuo kamili mbalimbali. Namba
za kulipia ni 0712202244 au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino
Tarimo. Ukishalipa tuma ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”
0 Response to "SABABU 4 KWANINI MATANGAZO YA BIASHARA YAKO HAYALETI WATEJA KAMA UNAVYOTAKA"
Post a Comment