KWANINI WAZO LA BIASHARA INAYOWEZA KUKULETEA FAIDA KUBWA SIYO TATIZO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI WAZO LA BIASHARA INAYOWEZA KUKULETEA FAIDA KUBWA SIYO TATIZO?

Zamani ndiyo ulikuwa ukimsikia mtu akihangaika kulinda kwa udi na uvumba wazo lake la biashara kusudi mtu mwingine mjanja asije akaliiba na kwenda kulifanyia kazi na hivyo kumpiku kibiashara, lakini katika dunia ya leo ambapo utandawazi umebadilisha karibu kila kitu kuanzia biashara mpaka jinsi tunavyowasiliana, wazo la biashara la kipekee tena siyo ishu kubwa kivile.

Zilikuwa ni zile enzi za ugunduzi, sasa hivi ni nani tena anayegundua kitu kipya kabisa kirahisi ambacho hakifanani hata kidogo na vile vilivyokwisha kugunduliwa kabla? Bila shaka hakuna na hata kama vipo vitakuwa ni vichache  kwa nadra sana.


Wazo la biashara hata hivyo ni muhimu sana na linapaswa tu kuwa ni wazo la biashara ambayo utakuwa na uwezo wa kuifanyia ubunifu mkubwa kusudi uweze kuhimili  ushindani katika soko na siyo lazima liwe la kipekee hapana. Katika uchumi wa leo uliojaa ushindani usiokuwa na hata chembe ya huruma, ikiwa kama hautaweza kufikiria nje ya boksi na kuja na ubunifu  mkubwa wakati uleule unapokuwa ukilitekeleza wazo lako, ukategemea upekee wa wazo hilo peke yake, utakuwa umepitwa na wakati.

Hapa siri kubwa inabakia kuwa katika utekelezaji ambao mara nyingi nimekuwa nikiusisitiza. Unaweza ukakaa na wazo lako bora la biashara hata miaka 10 lakini kama hakuna utekelezaji(execution), unabakia kuwa sawa tu na mtu yule asiyekuwa na wazo la biashara lolote lile la maana kichwani.


Dunia imejaa mifano ya biashara na makampuni mbalimbali yanayong’ara duniani kote sasa hivi kutokana na kutumia ubunifu katika mawazo yaliyoasisiwa na watu au makampuni mengine tofauti kabisa huku waanzilishi wenyewe wa mawazo hayo wengine wakiwa hata hawajulikani kama ni wao walioanzisha.

Kampuni ya Microsoft kwa mfano imepata umaarufu mkubwa kote duniani kwa mifumo yake ya uendeshaji kompyuta(Operating Systems) lakini Bill Gates hakuwa ni mtu wa kwanza kuigundua mifumo hiyo, naye aliiga kutoka watu/makampuni mengine na kuiboresha huku waanzilishi wake kwa kukosa ubunifu wakatoweka kwenye ushindani na kumwacha Gates ‘akipeta’


Hapa kwetu Tanzania pia tuna mifano mingi na mmoja wapo ni Kampuni ya uchapishaji ya Global Publishers chini ya mwasisi wake Bwana Eric James Shigongo, Shigongo hakuwa mtu wa kwanza kuanzisha biashara ya magazeti ya udaku hapa Tanzania. Hapo kabla tokea miaka ya 70 palikuwepo na magazeti ya udaku kama vile SANI, HEKO, KASHESHE, SANIFU, KOMESHA nk.  lakini Eric Shigongo alikuja na ubunifu wake wa kipekee wa kutunga hadithi tamu akafanya mapinduzi makubwa katika tasnia nzima ya magazeti hayo pendwa nchini na kupata mafanikio makubwa.

Halikadhalika kampuni kubwa la Google, Google haikuwa Search Engine ya kwanza mtandaoni, hapo kabla kulikuwepo na akina, Webcrawler, Yahoo, Excite nk. lakini leo hii kutokana na ubunifu, Google kwa kutumia mawazo yaleyale ya kwao anakaribia kuwapoteza kabisa kwenye ulimwengu wa search engines.

Orodha ni ndefu, tukitaja makampuni yote hapatatosha hapa lakini yote kwa yote ni kwamba kama unahangaika kupata wazo zuri la biashara itakayokutoa, kitu kikubwa cha kufanya wewe wala usiwaze sana fanya hivi;…………


……………………………………................

Ndugu msomaji wangu, somo hili hapa ni kipande tu, somo zima tutasoma leo katika Group la Whatsap la MICHANGANUO ONLINE. Masomo kama haya na yale yahusuyo jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara huwa tunajifunza kila siku.

Na hata ikiwa hutapata nafasi ya kushiriki leo, hujachelewa sana kwani masomo ya tangu January mpaka mwisho wa mwaka wetu unaoishia mwezi February mwakani tunayatunza kwa ajili ya mwanachama yeyote anayejiunga kabla ya muda huo kumalizika. Baada ya muda huo ukijiunga huwezi tena kupewa mfululizo wa masomo hayo.

Kiingilio ni sh. Elfu 10 tu na unalipa kupitia namba 0712202244 au 0765553030 jina hutokea Peter Augustino Tarimo. Ukishalipia tuma anuani yako ya email kwa meseji pamoja na ujumbe huu; NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO au unaweza kuwasiliana nasi kwa wasap 0765553030 kwa maelezo zaidi. Ikiwa hutumii wasap email inatosha tutakutumia masomo na  semina kama kawaida. Unapewa pia na kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali bure.

KARIBU!

0 Response to "KWANINI WAZO LA BIASHARA INAYOWEZA KUKULETEA FAIDA KUBWA SIYO TATIZO?"

Post a Comment