JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUWA NA USHAWISHI KWA WATU WENGINE(HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUWA NA USHAWISHI KWA WATU WENGINE(HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE)


Katika mfululizo wetu wa vitabu 300 vya pesa na mafanikio(maendeleo binafsi) vilivyoleta athari kubwa kabisa na mapinduzi ya hali ya juu kifikra katika maisha ya watu wengi hasa wale waliofanikiwa kimaisha, leo tutaangalia kitabu kilichoandikwa na mwandishi Dale Carnegie kiitwacho, “HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE” kikimaanisha, JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUWA NA USHAWISHI KWA WATU.

VITABU 300 VYA MAFANIKIO VILIVYOSOMWA ZAIDI DUNIANI

Ni kitabu cha elimu ya mafanikio na maendeleo binafsi kisichopitwa na wakati kamwe. Carnegie anaamini kwamba , uwezo wa kuwasiliana vyema pamoja na utambuzi mzuri ndiyo ufunguo wa mafanikio ya mtu yeyote anayejaribu kutafuta mafanikio. Kitabu hiki kinafundisha mbinu hizi(stadi) kwa kuonyesha namna ya kuwathamini watu wengine na kuwasaidia kujisikia kuwawa na thamani tena badala ya kuwa ni watu wasiokuwa na matumaini yeyote au walioshindwa kabisa kimaisha.

Dale Carnegie, kitabu hiki kauza nakala zaidi ya milioni 15 na kilitungwa hapo mwaka 1937 na kutolewa tena upya mwaka 1981. Kimetafsiriwa katikal lugha 36. Dale Carnegie mwenyewe kitaaluma ni mtu wa mauzo, pia ni mkufunzi wa chuo kikuu. Kitabu chake hiki, JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUWA NA USHAWISHI KWA WATU mpaka leo hii umaarufu wake badpo upo palepale. Kinamfaa mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa katika nyanja yeyote ile ya maisha iwe ni katika biashara na ujasiriamali, elimu na hata katika mahusiano ya kawaida kama ya mtu na mke au rafiki.

………………………………………………………………………..
Mpenzi msomaji, katika zawadi ambayo mtandao wa Intaneti umeleta kwa kizazi hiki cha binadamu tulichokuwa nacho sasa hivi, ni urahisi wa kupata taarifa na elimu kuliko kama vile ilivyokuwa miongo michache iliyopita. Vitabu vizuri kama hiki unaweza ukakipata bure na kwa urahisi kabisa kupitia mtandao wa intaneti, cha kufanya wewe “google” jina la kitabu likiishia na PDF, Ukisachi taratibu hatimaye utakutana nacho aidha katika mfumo wa PDF, Softcopy au hata Video. Download kitabu na kukihifadhi ili baadaye ukisome.

Jipatie pia vitabu vya kiswahili vya biashara na ujasiriamali vilivyotungwa kwa kuzingatia mazingira halisi ya Kitanzania, nonyeza maandishi yafuatayo kuingia ukurasa wenye vitabu hivyo. SMART BOOKS TANZANIA


Soma pia yaliyokuwemo(RATIBA KWENYE SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA) inayoendelea hapo.


0 Response to "JINSI YA KUPATA MARAFIKI NA KUWA NA USHAWISHI KWA WATU WENGINE(HOW TO WIN FRIENDS AND INFLUENCE PEOPLE)"

Post a Comment