JINSI YA KUJIUNGA NA MASOMO YA SEMINA YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA

Kujiunga na Darasa hili, lipa shilingi elfu 10 kupitia namba za simu 0712202244  au  0765 553030, jina litatokea Peter Augustino Tarimo, halafu tuma kwa meseji anuani yako ya barua-pepe(GMAIL). Baada ya hapo tutatumia e-mail yako hiyo kukuunganisha na DARASA LA SEMINA AU BLOGU HII HAPA, utakapobonyeza maandishi hayo huku ukiwa “umesign in” kwa e-mail yako hiyo ya GMAIL, basi moja kwa moja blogu itafunguka na kukupa fursa ya kudownload masomo mbalimbali ya michanganuo katika mifumo ya PDF na Sauti MP3. Sambamba na njia hizo 2, vile vile utapokea masomo hayo kwa njia ya email ambapo ni njia nzuri zaidi ya kuyatunza siku zote pasipo kupotea au kuharibika.

Kwa wateja wote wanaonunua au waliokwisha nunua kitabu cha Michanganuo ya biashara na ujasiriamali cha karatasi(hardcopy) hawatalipa kiingilio kwenye semina hii, kama wewe ulishanunua kitabu basi tuwasiliane ili tuweze kupata email yako kwa ajili ya kukuunganisha na blogu ya Semina. 

Darasa la Semina ya kujifunza jinsi ya kuandaa mpango wa biashara limeanzishwa rasmi kwa lengo la kuhakikisha wale wote wanaonunua kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lengo la kusoma michanganuo mbalimbali ya biashara pamoja na kujifunza namna ya kuandika michanganuo ya biashara zao wanapata fursa ya kuwa karibu zaidi na wakufunzi wa somo hili ikiwa ni pamoja na kuuliza maswali yanayowatatiza na mwisho kuhakikisha wanaandaa mpango wa biashara wanayotaka wao wenyewe wakipewa usaidizi kila wanapokutana na ugumu wowote ule.

Hakutakuwa na kisingizio cha aina yeyote ile kwa yule mwenye nia ya kujua michanganuo ya biashara. Katika maisha ya biashara na pesa mtu huwezi ukasema kuwa haitafika siku ukaja kuhitaji mpango wa biashara. Hata kama hutahitajika kuandika mwenyewe lakini kuna wakati unaweza ukahitajika labda na benki au taasisi yeyote ile uwasilishe mpango wa biashara yako, utakapokwenda kwa mtaalamu akuandikie unatakiwa angalao uwe na uelewa wa msingi juu ya mpango wa biashara ndipo mtaalamu aweze kukuandikia mchanganuo mzuri.

Si hivyo tu sehemu nyingi wanazohitaji upeleke mpango/mchanganuo wa biashara pia watakutaka ukauwasilishe mwenyewe kwa mdomo wako. Hivyo ni muhimu sana mtu yeyote uliyekuwa na ndoto za kuja kuwa mfanyabiashara na mjasiriamali mkubwa kujifunza walao hata kwa kusoma tu jinsi ya kuandaa mpango wa biashara na namna mipango yenyewe halisi inavyokuwa.


Lakini faida kubwa zaidi pengine kushinda zote za mtu kufahamu michanganuo ya biashara ni ile ya kuendesha biashara yako vizuri kwa ufanisi, unapofahamu namna ya kupanga biashara yako unazidisha uwezekano wa mafanikio katika biashara hiyo. Faida haipo kwenye mchanganuo wenyewe kama kurasa na maandishi hapana bali ipo kwenye mchakato mzima wa kufikiria kwani MPANGO WA BIASHARA ni kila kitu kinachohusiana na biashara kuanzia wazo lenyewe la biashara mpaka unapofikia hatua ya kupata faida.

Kwa hiyo kile kitendo tu cha kukaa na kuifikiria biashara yako, mwanzo mwisho namna utakavyoiendesha ni mchanganuo tosha wa biashara hata pasipo kuchukua kalamu na karatasi. Ndiyo maana nasisitiza kuwa unaweza kujifunza michanganuo ya biashara hata kama hupendi kuiandika na hilo linatosha wewe kuendesha biashara yako vizuri kimkakati.

Semina hili ijapokuwa lina muda wake wa mwisho wa kujiunga lakini hatujautaja rasmi kutokana na mfumo wenyewe wa kuiendesha ulivyo. Si lazima washiriki kuanza semina siku moja, wanaweza kila mmoja akaanza siku yake kulingana na siku aliyolipa kiingilio au ada. Lakini masomo watakayosoma kila mtu ni yaleyale na wote watapewa huduma zote kama kujibiwa maswali na kupewa usaidizi kwenye kuandaa mipango yao ya biashara. Pia mshiriki anaweza akatoa maoni yake.


0 Response to "JINSI YA KUJIUNGA NA MASOMO YA SEMINA YA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA"

Post a Comment