NYIMBO NZURI ZA KRISMASI ZINAZOPENDWA ZAIDI NA SIRI KUBWA 2 ZILIZOJIFICHA NDANI YAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NYIMBO NZURI ZA KRISMASI ZINAZOPENDWA ZAIDI NA SIRI KUBWA 2 ZILIZOJIFICHA NDANI YAKE

KUZALIWA KWA YESU KRISTO

*Makala hii siyo ya ujasiriamali, ina vionjo vya kidini na nimeandika kwa lengo la kuhabarisha na pengine kuelimisha tu peke yake na wala si vinginevyo. Ikiwa kwa namna yeyote ile wewe mfuatiliaji wa blogu hii utakwazika tafadhali tunaomba radhi.

Katika Ulimwengu mzima wa Kikristo na hata katika baadhi ya maeneo yasiyokuwa na Wakristo wengi inapofika msimu wa sikukuu ya Christmas aghalabu utasikia watu wakisheherekea kwa kupiga nyimbo mbalimbali maarufu za krismas kama vile Jingle bells, Feliz Davidad, Marry’s Little Boy Child, Silent Night, Santa Claus na nyinginezo nyingi tu. Kuna hata nyimbo nyingine za Krismas zilizopigwa na bendi za hapahapa kwetu, Congo au Afrika Mashariki kama vile wimbo maarufu wa mwimbaji kutoka DRC zamani Zaire aliyekuwa akiishi nchini Kenya, Baba Gaston Ilunga wa Ilunga uitwao Viva Krismasi au Noela Christmas(Kakolele), wimbo mwingine ni wa Simba wa nyika na Orchestra Jobiso uitwao Sikukuu imefika. Ndala Kasheba naye akiwa na bendi ya OSS aliwahi kupiga kibao cha Krismasi.

SOMA: Sikiliza wimbo Ipo siku yangu tu wa Goodluck Gosbert 

Watu kwa miaka mingi wamekuwa na utamaduni wa kuzipiga nyimbo hizi sambamba na desturi nyingine za Krismasi kama vile, kupamba mti wa krismasi, Pango la noeli linalowekwa sanaa mbalimbali zinazoelezea tukio la kuzaliwa kwa Masihi Yesu Kristo katika mji wa Bethlehemu ya Uyahudi enzi hizo za Herode huku mamajusi wakionekana kumletea zawadi, uvumba na manemane. Siku ya kufungua zawadi(boxing day) nk. Desturi hizi huambatana pia na watu hasa Wakristo kununua vitu vipya mfano mavazi, vyakula na vinywaji kisha kusherekea kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo mika zaidi ya 2000 iliyopita.

Lakini pamoja na kufurahia nyimbo na miziki hiyo unaijua siri kubwa iliyojificha katika nyimbo hizo tamu za krismasi?

1.Nyimbo nyingi za krismasi zimetungwa na kuimbwa na watu wasioamini(Wakristo majina)     
Unaposikiliza melodi tamu za mziki wa krismasi mfano ule uliopigwa na John Lennon, Happy Xmass unaweza ukadhani labda John Lennon alikuwa mcha Mungu sana kutokana na maneno na melodi ya wimbo unavyoleta upako, kumbe usichokijua ni kwamba Lennon alikuwa ni mwanamuziki tu wa kawaida msaka kipato na bila shaka wakati akiutunga wimbo huo pengine hakuwa na upako wowote ule rohoni kama watu wengi wanavyoweza kudhania. Wimbo kuwa na upako haimaanishi kwamba mtunzi wake naye lazima alikuwa ni mtu mwenye upako hapana.

SOMA: Christopher Mwahangila Mungu ni Mungu tu, download video na kusikiliza wimbo.

Tuangalie mifano ya waimbaji wengine kama vile Jim Reeves na nyimbo zake kama, Jingle bells, Mary’s little boy child, Silent night na nyinginezo nyingi alizoimba. Kwa wasioijua historia yake wengi hudhani labda Jim Reeves alikuwa mchungaji wa kanisa fulani hivi au mwanakwaya, lakini ukweli ni kwamba zaidi ya kusali Madhehebu ya Kibaptist tena wakati mwingine baadhi yao huwa hawaamini sikukuu za krismas, Reeves alikuwa ni mwimbaji wa kawaida wa muziki wa Coutry aliyejipatia umaarufu mkubwa miaka ya 50 na 60 kabla ya kupata ajali ya ndege ndogo aliyokuwa akiiendesha mwenyewe katika anga lililojaa mvua na radi siku hiyo. Hata hivyo nyimbo za Krismasi tofauti na baadhi ya waimbaji wengine yeye aliziimba kwa umahiri mkubwa na ujumbe wake ulikuwa kweli  ni ule unaoendana na maana halisi ya Krismasi.

SOMA: Madhehebu ya Kikristo wasiosherekea sikukuu ya Krismasi na sababu kubwa ya kutoadhimisha.

Kundi mfano la Boney M na nyimbo zake za Krismas kama vile Little Drummer boy, Holly Night, Winter family tale, White Christmas, Ribons of blue, Felis Navidad, Jingle bells, Hooray its holy holy day na nyinginezo nyingi ingawa nyingi walirudia nyimbo zilizokwishapigwa na wasanii wengine hata hivyo zilipendwa sana na mpaka leo zinapopigwa redioni huvutia hisia za watu wengi.


Lakini mbali na mafanikio hayo yote sidhani kama hata waimbaji wa kundi hili walikuwa wakihudhuria kanisani licha ya ukweli kwamba wengi wao walitokea madhehebu ya Kiprotestant na hasa Lutheran kutokana na asili yao kuwa ni huko Ulaya(Ujerumani na Norway). Kundi hili machachari lilipiga muziki wa Pop lakini muziki wa Krismasi bila shaka waliupiga kwa lengo la kibiashara zaidi kwani sijawahi kusikia kama waliwahi  kuwa wanakwaya katika kanisa lolote.

SOMA: Msichana aliyejaliwa uwezo wa ajabu wa kuimba mashairi

Kuimba nyimbo za Krismasi kwa baadhi ya bendi na wasanii wakubwa Duniani huwa wana “take advantage” ya soko kubwa la muziki huo hasa nyakati za sikukuu hiyo na wala siyo kwa nia hasa ya Kumtukuza Yesu Kristo ingawa lakini siwezi nikasema ni wasanii wote wanaofanya hivyo.

Siiliza na kudownload wimbo wa Felis Navidad wa kundi la Boney M hapa chini;


Wimbo unaoitwa ni wa Krismasi mfano wa mwimbaji Maria Carey uitwao All I want  for Christmas is You, unazungumzia mapenzi na wala siyo kweli kuzaliwa kwa Mwokozi, vivyo hivyo pia na wimbo wa Baba Gaston Ilunga wa Ilunga uitwao Viva Krismasi au Noela Christmas wengine huuita Kakolele nao unamsifia na kumbembeleza mrembo amkubali siku ya Krismasi kinyume kabisa na maudhui ya krismasi yenyewe halisi.

2.Nyimbo za Krismasi hupendwa na Wakristo, baadhi ya wasiokuwa wakristo na hata wapagani.
Kutokana na melody nzuri ya nyimbo nyingi za Krismas, imetokea nyimbo hizi kupendwa sana na watu wa imani tofautitofauti hata na baadhi ya wale wasiokuwa Wakristo. Muziki wa krismasi unaweza ukawa unapigwa mahali ukashangaa mtu akifuatilia midundo yake hata ikiwa mtu huyo siyo wa imani ya Kikristo .

SOMA: Hebu soma alichokifanya mwimbaji huyu wa nyimbo za Injili Alex Obadia.

Redio stesheni nazo na hata vituo vya TV bila kujali ni vya kidini au vya kisekula, vituo hivi vimekuwa vikitumia nyimbo na midundo ya muziki mbalimbali wa krismasi katika matangazo ya biashara na burudani hasa msimu wa Krismasi na Mwakampya unapofika. Kitu kingine cha kushangaza ni kwamba kuna baadhi ya watu wa Vikundi  na madhehebu ya Kikristo ambao kutokana na tofauti kubwa walizokuwa nazo ni vitu vichache sana huweza kuwaweka pamoja lakini nyimbo hizi ni kama vile huwaunganisha kutokana na jinsi utakavyokuta wanazikubali na kuzisikiliza bila ubaguzi.

………………………………………..

Mpenzi msomaji wa blogu hii, Unaweza pia kupata masomo mazuri yahusuyo fedha na mipango ya biashara kila siku katika Group letu la WASAP liitwalo  Michanganuo-online kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu.

Unakuwa mwanachama wa kudumu pamoja na kutumiwa masomo yote yaliyokwishapita kwenye group hilo. Ni masomo na semina nzuri, michanganuo ya biashara mbalmbali zinazolipa pamoja na vitabu vizuri. Wahi offa ya mwisho wa mwaka kabla hatujaanza mwaka 2019 kwani bei itapanda.

Kulipia group tumia namba za simu 0712202244 au 0765553030 kisha tuma ujumbe, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

Unaweza pia kujipatia vitabu vyetu hapa chini;




   




0 Response to "NYIMBO NZURI ZA KRISMASI ZINAZOPENDWA ZAIDI NA SIRI KUBWA 2 ZILIZOJIFICHA NDANI YAKE"

Post a Comment