CHRISTOPHER MWAHANGILA, MUNGU NI MUNGU TU, DOWNLOAD VIDEO,SIKILIZA WIMBO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHRISTOPHER MWAHANGILA, MUNGU NI MUNGU TU, DOWNLOAD VIDEO,SIKILIZA WIMBO



Hakuna sekta iliyojaa fursa nzuri na ya haraka kama usanii, iwe ni katika filamu, muziki urembo na hata sanaa nyinginezo ikiwa kama mtu utaamua kuifanya kwa umakini wa hali ya juu “seriously”. Kuna mifano ya vijana wengi maisha yao yamekuwa bora na hata wengine kutajirika kupitia sanaa. Haihitaji elimu ya juu sana ijapokuwa pia mtu anapokuwa na elimu hususani inayohusiana na sanaa yenyewe mfano kutoka vyuo vya sanaa kama vile Bagamoyo anakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa.


Christopher  Mwahangila akifanya vitu vyake jukwaani.
Nionavyo mimi, wimbo kama huu wa Christopher  Mwahangila, “MUNGU NI MUNGU TU” kila mtu aliyewahi kuusikiliza hakuna ubishi kuwa una mvuto masikioni, siupigii debe ila kutaka kuonyesha kiwango cha juu cha usanii uliotumika. Nadhani hata ikiwa mtu siyo mtaalamu wa muziki lakini wimbo mzuri utaujua tu kwa midundo, mpangilio wa ala na sauti na hivyo kumfanya msikilizaji kuvutiwa kusikiliza. Uwe ni wimbo wa dini au wowote ule kama ni mzuri masikio ya binadamu yeyote yule yataufurahia.


Na kwa kadiri  watu wengi watakavyopendezewa na wimbo fulani, basi ndivyo hivyo hivyo na soko la wimbo huo au msanii husika litakavyokuwa kubwa na punde watu hushangaa kusikia fulani tayari ameshatoka kimaisha kupitia usanii. Haijalishi unaimba nyimbo za injili au za Dunia, ukiimba vizuri utapata mashabiki wengi tu. Wasanii mfano wa akina Christopher Mwahangila, Edson Mwasabwite, Masanja Mkandamizaji, Diamond Platnumz, Ali Kiba, Marehemu Steven Kanumba na wengineo wengi majina yao yamekuwa maarufu siyo kwa sababu labda vyombo vya habari viliwaandika sana, la hasha, bali ni kutokana na kazi zao kuvutia hisia za watu wengi.

Chanzo cha picha: kichila.blogspot.com  

0 Response to "CHRISTOPHER MWAHANGILA, MUNGU NI MUNGU TU, DOWNLOAD VIDEO,SIKILIZA WIMBO"

Post a Comment