SABABU KUU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA, ZIPI ZINAKUVUTA NYUMA USIFANIKIWE? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SABABU KUU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA, ZIPI ZINAKUVUTA NYUMA USIFANIKIWE?

Njia mpya za kutafuta soko la huduma
‘Kazi’ sasa ni ‘ubia’

Wanaume na wanawake wanaotaka kutangaza huduma zao kwa faida zaidi kwa siku zijazo ni lazima watambue maabadiliko makubwa sana yaliyotokea katika mahusiano baina ya mwajiri na mwajiriwa.

Muda utafika ambapo “Sheria ya dhahabu” na siyo  “Utawala wa dhahabu” kitakuwa kigezo kinachotawala katika kutafuta soko la bidhaa na huduma. Pia uhusiano baadaye kati ya waajiri na waajiriwa wao utakuwa zaidi katika hali ya ubia ukijumuisha :
(a)        Muajiri
(b)        Muajiriwa
(c)        Jamii wanayoihudumia
       
Njia hii mpya ya kutafuta soko la huduma inaitwa mpya kwasababu nyingi. Kwanza, wote mwajiri na mwajiriwa wa wakati ujao watachukuliwa kama waajiriwa wenza ambao biashara yao itakuwa ni kuhudumia jamii kwa ufanisi . Zamani waajiri na waajiriwa walibadilishana wenyewe kwa wenyewe, wakiendesha makubaliano mazuri kabisa waliyoweza kuafikiana kila mmoja bila ya kujali kwamba katika tathmini yao ya mwisho ukweli walikuwa wakipatana kwa niaba ya upande wa tatu, jamii waliyoihudumia.

SOMA: Uchumi ukishuka na ajira kuwa adimu, ubunifu wa soko la biashara zetu unahitajika.

Wakati ujao, wote waajiri na waajiriwa watatambua kwamba hamna tena upendeleo wa kuendesha mapatano kwa niaba ya wale waliowahudumia. Mwajiri wa kweli wa wakati ujao atakuwa ni jamii. Hili linatakiwa kupewa kipaumbele akilini na kila watu wanaotafuta soko la bidhaa zao kwa ufanisi.

Heshima na huduma ndiyo kaulimbiu ya biashara leo. Vinafanya kazi kwa mtu anayetafuta soko la huduma zake hata moja kwa moja zaidi kuliko kwa mwajiri wanayemfanyia kazi, kwasababu katika tathmini ya mwisho, wote mwajiri na mwajiriwa wanaajiriwa na jamii wanayoihudumia. Ikiwa watashindwa kuihudumia vizuri, watalipa kwa kupoteza upendeleo wao wa kutoa huduma.

Kipimo chako cha “UKI” ni kipi?
Sababu ya kufanikiwa katika kutafuta soko la huduma kikamilifu na la kudumu imeelezwa kwa ufasaha. Ikiwa kama sababu hizo hazitasomwa, kuchunguzwa, kueleweka na kutumiwa, hakuna mtu atakayeweza kutafuta soko la huduma zake kwa njia kamilifu na ya kudumu. Ni jukumu lako kuuza huduma zako mwenyewe. Ubora na Kiasi cha huduma zitolewazo na Imani huduma inayotolewa ndiyo huamua kwa kiasi kikubwa bei na muda wa ajira. Katika kutafuta soko la huduma kikamilifu(ambapo maana yake ni soko la kudumu, katika bei muafaka, chini ya mazingira mazuri) mtu ni lazima akubali na kufuata kanuni ya UKI, ambayo maana yake ni UBORA jumlisha KIASI jumlisha IMANI sahihi ya ushirikiano sawa na utafutaji soko kamilifu wa huduma. Kumbuka kanuni ya ‘UKI’ lakini fanya zaidi- itumie kama mazoea!

SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unazotaka maishani.

Hebu tuichambue kanuni hiyo kuhakikisha tunaelewa hasa inamaanisha kitu gani.
1.  UBORA wa huduma unamaanisha utendaji kazi wa kila kitu kwa kina, kuhusiana na nafasi yako, katika hali ya ufanisi mkubwa inavyowezekana, kwa lengo la ufanisi mkubwa mara zote akilini.
2.  KIASI cha huduma humaanisha TABIA ya kutoa huduma zote unazoweza kutoa, kwa muda wote, kwa lengo la kuongeza kiasi cha huduma kwa kadiri unavyoongeza maarifa kupitia vitendo na uzoefu. Msisitizo tena unawekwa katika neno TABIA
3.  IMANI ya huduma humaanisha TABIA ya ukubalifu(kukubali) kitendo cha utengamano kitakachochochea ushirikiano kutoka kwa washirika na wafanyakazi wenza.

Wingi wa UBORA na KIASI cha huduma havitoshi kudumisha soko la kudumu kwa huduma zako. Mwenendo au IMANI ambayo unatoa huduma ni kigezo kikubwa kinachohusika na vitu vyote viwili, bei unayopata na kiasi cha muda unachoajiriwa.

Andrew Carnegie alisisitiza kipengele hiki zaidi kuliko wengine katika maelezo yake ya sababu za kufanikiwa katika kutafuta soko la huduma . Alisisitiza tena na tena umuhimu wa tabia ya masikilizano- Alisisitiza kwamba, asingeweza kumvumilia mtu yeyote ambaye hakufanya kazi kwa roho ya masikilizano licha ya ukubwa wa kazi au ufanisi wa ubora wa kazi yake. Bwana Carnegie alisisitiza juu ya kila mtu kukubaliana. Kuthibitisha hilo aliweka thamani kubwa kwenye sifa hii, aliruhusu watu wengi walioendana na viwango vyake kuwa matajiri sana. Wale ambao hawakuendana ilibidi wawapishe nafasi wengine.

SOMA: Nguvu na udhaifu wa akili yako, hutokana na kujiamini binafsi au kukosa kujiamini. 

Umuhimu wa haiba inayokubalika umesisitizwa kwa sababu unamuwezesha mtu kutoa huduma katika imani sahihi. Ikiwa mtu ana haiba inayopendeza na anatoa huduma katika roho ya masikilizano, rasilimali hizi mara nyingi huziba pengo kwa mapungufu katika vyote, ubora na wingi wa huduma anazotoa mtu.

Thamani ya Mtaji wa Huduma zako
Mtu ambaye kipato chake chote hutokana na mauzo ya huduma zake hana tofauti na mfanyabiashara anayeuza bidhaa. Inaweza kuongezewa vizuri kwamba mtu kama huyo analengwa na sheria zilezile na taratibu kama ilivyokua kwa mfanyabiashara anayeuza bidhaa. Hili limesisitizwa kwasababu wengi wetu wanaoishi kwa kuuza huduma zao, hufanya makosa ya kujichukulia wenyewe kuwa hawahusiki na sheria za taratibu na wajibu unaoambatana na wale wanaojihusisha katika kutafuta soko la bidhaa.

Thamani halisi ya mtaji wa ubongo wako inaweza kujulikana kwa kiasi cha mapato unachoweza kuzalisha (kwa kuuza huduma zako). Makadirio ya haki ya thamani ya mtaji wa huduma zako  inaweza kupatikana kwa kuzidisha mapato yako ya mwaka kwa 16 na mbili ya tatu, kama ilivyokuwa sahihi kukadiria kwamba mapato yako ya mwaka yanawakilisha asilimia sita ya thamani ya mtaji wako. Fedha hukodishwa kwa asilimia sita kwa mwaka. Fedha haina thamani kushinda ubongo, mara nyingi ina thamani ndogo zaidi.

‘Ubongo’(akili)shindani ikiwa zitatafutiwa soko kikamilifu huwakilisha aina ya mtaji unaofaa zaidi kushinda ule unaohitajika kuendesha biashara inayohusika na bidhaa. Hii ni kwasababu  ‘ubongo’(akili) ni aina ya mtaji ambao hauwezi ukashushwa thamani  moja kwa moja kwenye mdororo wa uchumi, wala aina hii ya mtaji hauwezi ikaibiwa wala kupotea. Zaidi ya hapo, pesa zinazohitajika kuendsha biashara thamani yake ni ndogo kama mchanga mpaka pale zitakapochanganywa  na akili yenye ufanisi.


Sababu Kuu 30 za Kuanguka.
Ni ngapi kati ya hizi zinazokurudisha nyuma?
Maisha ni janga kubwa linalojumuisha wanaume na wanawake ambao kwa kweli hujaribu na kufeli! Janga hilo lipo katika idadi kubwa kupindukia ya watu wanaofeli, ukilinganisha na watu wachache wanaofanikiwa.

SOMA: Utajiri huanza na wazo, ukomo wa utajiri hupangwa na mtu mwenyewe akilini.

Nilikuwa na bahati ya kuchunguza maelfi kadhaa ya Wanaume na Wanawake, kati yao asilimia 98 walikuwa wamewekwa katika kundi la “waliofeli”. Kuna kitu fulani kisichokuwa sahihi kabisa kuhusu ustaarabu na mfumo wa elimu unaohusu watu wengi kiasi hicho kupitia maisha kama walioshindwa. Lakini sikuandika kitabu hiki kwa lengo la kupima mema na mabaya ya dunia, hilo lingeweza kuhitaji  kitabu chenye ukubwa mara 100 zaidi ya hiki.

Kazi yangu ya kutathmini ilithibitisha kwamba kuna sababu kuu 30 za kuanguka. Kama utakavyoipitia orodha hiyo, iangalie mwenyewe kipengele kwa kipengele kugundua ni sababu ngapi kati ya hizi za kuanguka zinazosimama katikati yako na mafanikio.

1. KURITHI MAZINGIRA YASIYOFA.
Kama kuna kitu chochote kinachoweza kufanyika ni kidogo sana kwa watu wanaozaliwa na upungufu katika nguvu ya ubongo. Filosofia hii hutoa njia moja tu ya kurekebisha upungufu huu kupitia msaada wa nguvu ya ushirika ‘Master mind’(angalia uk. wa 193). Chunguza kwa faida, hata hivyo kwamba hii ndiyo sababu pekee kati ya sababu 30 za kufeli ambayo haiwezi kuirekebishwa kirahisi na mtu yeyote.

2. KUKOSA LENGO LILILOKUWA WAZI MAISHANI.
Hakuna matumaini ya mafanikio kwa mtu asiyekuwa na kusudi kuu, au lengo dhahiri la kulenga. Watu tisini na nane kati ya kila mia ya wale niliowachunguza hawakuwa na lengo la namna hiyo. Pengine hii ndiyo iliyokuwa sababu kubwa ya maanguko yao.

SOMA: Nguvu inayohitajika kuweka malengo ya kupata mali na utajiri ni sawa na ile inayohitajika kuleta mateso na umasikini.

3. KUKOSA NIA THABITI YA KUWA NA MALENGO MAKUBWA.
Hatutoi matumaini kwa watu wasiojali kabisa kutaka kupiga hatua maishani na asiyekuwa tayari kulipa gharama.

4. ELIMU DUNI
Hiki ni kilema kinachoweza kuondolewa kwa urahisi zaidi. Uzoefu umethibitisha kwamba watu walioelimika vizuri mara nyingi ni wale wanaojulikana kama ‘waliojijenga wenyewe’ au waliojielimisha wenyewe. Huchukua zaidi ya shahada ya chuo kikuu kumfanya mtu kuwa mtu wa elimu. Mtu yeyote aliyeelimika anajifunza kupata chochote kile atakacho maishani bila ya kuingilia haki za wengine. Elimu haina maarifa mengi sana, bali maarifa yanayotumiwa kikamilifu na kwa uendelevu. Watu hulipwa siyo tu kwa kile wajuacho, bali zaidi hasa kwa kile wakifanyacho na kile wakijuacho.

5. UKOSEFU WA NIDHAMU BINAFSI
Nidhamu huja kupitia kujizuia binafsi. Hii ina maana kuwa ni lazima udhibiti sifa zote hasi. Kabla haujadhibiti hali ni lazima kwanza ujidhibiti mwenyewe. Kujidhibiti binafsi ndiyo kazi ngumu zaidi utakayopambana nayo. Ikiwa hautaishinda nafsi, utashindwa na nafsi. Unaweza ukaona katika nafsi moja na kwa wakati mmoja watu wote wawili yaani rafiki yako mkubwa na adui yako mkubwa , kwa kusogea mbele ya kioo.

6. AFYA MBAYA.
Hakuna mtu anayeweza kufurahia mafanikio yanayoonekana pasipokuwa na afya njema . Nyingi ya sababu zinazoleta afya mbaya hutegemea ustadi na udhibiti. Nazo kwa kiasi kikubwa ni;
·       Ulaji wa vyakula visivyofaa kwa afya.
·       Mazoea mabaya ya kufikiri, kuonyesha hisia hasi.
·       Matumizi mabaya na kuendekeza ngono kupita kiasi.
·       Ukosefu wa mazoezi ya viungo yanayofaa.
·       Ukosefu wa hewa safi, unaotokana na upumuaji usiofaa.

7. ATHARI ZA MAZINGIRA YASIYOFAA WAKATI WA UTOTO
Kwa kadiri tawi linavyokunjwa, ndivyo mti nao utakavyoota, watu wengi walio na tabia za kihalifu, walizipata kutokana na mazingira mabaya na makundi yasiyofaa wakati wa utoto

SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika.

8. KUSITASITA.
Hii ni moja ya sababu kubwa ya kushindwa. ‘Kikongwe kusitasita’  husimama miongoni mwa vivuli vya watu wote akisubiri nafasi ya kuharibu fursa zao za mafanikio. Wengi wetu huishi maisha kama waliofeli kwasababu tunasubiri muda wa ‘kuwa sahihi’ kuanza kufanya kitu fulani chenye manufaa. Usisubiri. Muda hautakaa ‘uwe sahihi’. Anzia pale uliposimama, fanya kazi na zana yeyote unayoweza kuwa nayo, na zana bora zitapatikana kadiri utakavyokuwa ukisonga mbele.

9. KUKOSA UVUMILIVU.
Wegi wetu ni waanzilishi wazuri lakini ni wamaliziaji wabaya wa kila jambo tunaloanzisha. Na zaidi, watu ni wepesi wa kukata tamaa katika dalili za mwanzo za kushindwa. Hakuna mbadala wa uvumilivu. Mtu mvumilivu hugundua kwamba ‘Kikongwe anguko’ mwishowe huchoka na kutoweka . Anguko haliwezi kustahimili uvumilivu.

10. HULKA MBAYA.
Hakuna matumaini ya mafanikio kwa mtu anayewafukuza watu kupitia tabia hasi.Mafanikio huja kupitia matumizi ya nguvu na nguvu hupatikana kupitia ushirikiano wa watu wengine. Hulka hasi hazitavuta ushirikiano.

11. KUSHINDWA KUZUIA TAMAA YA NGONO
Nguvu ya ngono ndiyo kichocheo chenye nguvu zaidi kuliko vingine vyote vinavyomsukuma mtu kutenda. Kwa kuwa ndiyo mhemko ulio na nguvu zaidi, ni lazima udhibitiwe kupitia mageuzi na kubadilishwa kwenda kwenye mikondo mingine.

12. HAMU ISIYOTULIZIKA YA KUPATA KITU BILA YA KUTOA CHOCHOTE.
Tabia ya kucheza kamari huwafanya watu wengi kuanguka .

13. KUKOSA UWEZO ULIOKUWA DHAHIRI WA MAAMUZI.
Watu wanaofanikiwa hufikia maamuzi mara moja na kuyabadilisha taratibu ikiwa ni lazima kufanya hivyo. Watu wanaoanguka hufikia maamuzi mara kwa mara na kwa haraka. Kutokufanya maamuzi na kuahirisha ni vitu mapacha, kinapokuwepo kimoja, kingine mara nyingi huwepo pia. Waue marafiki hawa wawili kabla hawajakufunga katika kinu cha maanguko moja kwa moja.

14. MOJA AU ZAIDI YA HOFU SITA.
Hofu hizi zimetathminiwa kwako katika sura ya 15. Ni lazima zifahamike vyema kabla haujaweza kutafuta soko la huduma zako kikamilifu.

SOMA: Imani mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa.

15. UCHAGUZI MBAYA WA MWENZA KATIKA NDOA.

Hii ndiyo sababu kubwa zaidi ya kuanguka. Mahusiano ya ndoa huwaleta watu karibu kimapenzi. Ikiwa kama uhusiano huu siyo wa masikilizano, kuna uwezekano mkubwa wa maanguko kufuata. Zaidi, itakuwa ni aina ya maanguko yaliyoambatana na taabu na huzuni, vikiharibu dalili zote za matumaini. 


 Soma sura na sehemu za kitabu think & grow rich zilizopita hapa

0 Response to "SABABU KUU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA, ZIPI ZINAKUVUTA NYUMA USIFANIKIWE?"

Post a Comment