KUANDIKA MPANGO KAMILI WA BIASHARA YA CAFE, MTAJI MILIONI 3 (3,000,000/=) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUANDIKA MPANGO KAMILI WA BIASHARA YA CAFE, MTAJI MILIONI 3 (3,000,000/=)

upendo cafe

KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA CHAKULA HATUA KWA HATUA (UPENDO CAFE)


RATIBA YA MAFUNZO

SIKU YA KWANZA TAR. 25/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO;

UTANGULIZI               

1.    Maana halisi ya Mpango wa Biashara

2.    Kitu cha kwanza kufanya kabla hujaanza kuandika mpango wako wa biashara

3.    Jinsi ya kufanya Utafiti wa biashara ya Cafe

4.    Njia kuu 3 unazoweza kuzitumia kuandika mpango wako

5.    Vipengele muhimu 8 vya mpango wa biashara

6.    Jalada la nje linatakiwa liwe na vitu gani juu yake?

 

SIKU YA PILI TAREHE 26/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO;

1.    Muhtasari wa mpango wako

2.    Maelezo ya Biashara

3.    Maelezo ya Bidhaa/Huduma

SIKU YA TATU TAREHE 27/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO

1.    Tathmini ya soko

2.    Mikakati na Utekelezaji

 

SIKU YA NNE TAREHE 28/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO

1.    Mpango wa Uendeshaji

2.    Uongozi na Nguvukazi

 

SIKU YA TANO TAREHE 29/12/2022 TUTAJIFUNZA YAFUATAYO

1.    Mpango wa Fedha

·       Mauzo ya kurudisha gharama(Break even Analysis)

·       Makisio ya Faida na hasara miezi yote 12

·       Makisio ya Faida na Hasara miaka 3

·       Makisio ya Mtiririko wa fedha miaka 3

·       Makisio ya Mali na madeni miaka 3

 


UTANGULIZI: 

Mpango wa biashara maana yake ni nini?

Kabla hatujaenda kuanza rasmi kuandika hatua kwa hatua mpango wa biashara hii ya UPENDO CAFE, kwanza ni vizuri kujikumbusha maana hasa ya Mpango/Mchanganuo wa biashara ni kitu gani.

Mpango wa biashara unaweza ukaulezea kwa namna nyingi tofauti lakini kwa mujibu wa Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI mpango wa biashara maana yake ni hii; 

Maandishi yanayoelezea kila jambo kuhusu biashara unayotaka kuiendesha, mambo hayo ni, malengo, mikakati, bidhaa/hudumu utakayouza, soko (wateja), shughuli mbalimbali za masoko na uongozi, gharama, mahitaji, na masuala yote yanayohusiana na fedha. 

Au pia unaweza ukasema hivi;             

Mpango wa Biashara ni jumla ya maelezo yote yanayoihusu biashara, kuanzia malengo ya biashara mpaka mbinu mbalimbali zitakazotumika kufanikisha biashara husika.

Au unaweza ukasema tu kwa kifupi hivi;

Ni dira au ramani inayokuongoza katika biashara yako kujua unatoka wapi na unaelekea wapi.  

 

NUKUU MUHIMU

“Mpango wa biashara ni andiko linaloishi, unachokiandika leo siyo lazima kiwe kile kitakachotokea kesho na ndiyo maana unaitwa utabiri/makisio. Cha msingi ni kufanya marejeo mara kwa mara wakati wa utekelezaji ukilinganisha hali halisi na makisio yako, uongeze nini au upunguze kitu gani kusudi biashara yako iweze kufanikiwa zaidi. Na hii haimaanishi kwamba mpango wa biashara hauna maana hapana, kwani hakuna mtu yeyote yule duniani anayeweza kudai ameanzisha biashara bila kwanza ya kupanga kichwani mwake au kwenye makaratasi ataifanyafanyaje biashara hiyo” – Peter Augustino Tarimo  

 

KITU CHA KWANZA KABISA KUFANYA KABLA HUJAANZA KUANDIKA MPANGO WAKO WA BIASHARA YA CAFE

Kuandika mpango wa biashara maana yake ni kwamba utahitaji taarifa mbalimbali wakati unaandika na taarifa hizo ili kuzipata ni lazima uzitafute kwanza. Kwahiyo kitu cha kwanza kabisa kufanya ni kuanza kuzitafuta taarifa mbalimbali zinazohusiana na biashara yako ya Cafe na kitendo hiki kinaitwa Utafiti wa biashara, wengine huita utafiti wa soko au feasibility study kwa kimombo.

 

JINSI YA KUFANYA UTAFITI WA BIASHARA YA CAFE

Kimsingi katika Utafiti wa biashara mtu unapaswa kuchunguza mazingira yote yanayoihusu biashara husika, kwa maana nyingine ni kwamba unatakiwa kuifahamu hiyo biashara nje ndani. Hivyo ukishindwa kufuata njia za kitaalamu kufanya utafiti usihofu, wala siyo jambo baya, kwani watu wengi hufanya utafiti wa biashara zao bila hata ya wao wenyewe kujua kama wanachokifanya ni utafiti  

Siyo kila kitu kwenye mpango wako utahitaji taarifa za utafiti, sehemu nyingine unahitaji tu maelezo ambayo tayari utakuwa unayo kichwani. Hivyo katika utafiti tutazingatia zaidi maeneo makuu yafuatayo

1. Ufafiti  wa soko na bidhaa utakazouza. 

2. Utafiti wa maswala ya kiufundi na Utawala. 

3. Utafiti wa maswala ya fedha.

Katika vipengele hivyo 3 hapo juu unaweza kuona vinafanana na baadhi ya vile tutakavyokwenda kuona kwenye mpango wa biashara kwa kuwa kimsingi mambo yanayotakiwa uyachunguze katika utafiti ndiyo yaleyale tutakayokuja kutumia majibu yake wakati tukiandika mpango wa biashara. 

Kwenye utafiti wa soko na bidhaa wamiliki wa biashara hii, UPENDO CAFE waliongozwa na maswali yafuatayo; 

1. SOKO.

·      Soko la bidhaa zao ni lipi?

·      Walengwa wao ni akina nani?

·      Tabia za wateja wao zikoje.

·      Wapo wateja wangapi kwenye hilo soko?

·      Kuna changamoto zipi zinazolikabili soko hilo?

·      Ni gharama kiasi gani itakayotumika kulifikia soko?

·      Ni nani washindani wao wa moja kwa moja na wsiokuwa wa moja kwa moja?

·      Bidhaa zao zinafanana au kutofautiana vipi na za washindani wao?

·      Ni nini siri yao kuu ya mauzo?

·      Je washindani wao wanaweza kuwaiga kirahisi?

·      Washindani wao wanachukuliaje ujio wao katika soko?

 

2. Bidhaa /Huduma.

Katika kipengele hiki walitafiti maswali haya yafuatayo kuhusiana na bidhaa na huduma watakazozitoa; 

·      Sifa za bidhaa(chapatti, mandazi supu nk.) watakazouza

·      Jinsi mauzo yatakavyofanyia je ni ndani ya cafe, take away au njia gani nyingine?

·      Chanzo cha malighafi za kutengenezea vyakula mbalimbali ni wapi, na je zinapatikana kwa urahisi? 

·      Mahitaji ya wateja kwa vyakula mbalimbali ni kiasi gani?

·      Kiwango cha uzalishaji kwa siku/mwezi

·      Upekee wa bidhaa zao ni kitu gani?. 

·      Ni teknolojia ipi au ufundi utakaotumika?

·      Ukubwa na aina ya mashine na vifaa vitakavyotumika ukoje?

·      Kukadiria mahitaji ya vifaa na malighafi zitakazohitajika. 

·      Ni kina nani, watakaowapatia  teknolojia  itakayotumika

·      Je, teknolojia watakayotumia ni ya kisasa au imepitwa na wakati?

·      Je, ni teknolojia inayoweza ikaigwa kirahisi?

·      Je, soko linafikika kirahisi? 

·      Tathimini  upatikananji wa vitendea kazi kama vile umeme, gesi maji n./k

·      Tathimini ya uchafuzi wa mazingira.

·      Ni faida gani jamii itakayopata kutokana na huu mradi?

·      Kuangalia sheria na taratibu mbalimbali za nchi zinazohitajika kufuatwa.

·      Kutathimini mwitikio wa jamii inayouzunguka mradi juu ya kuanzisha biashara husika katika mazingira yao.

·      Kutafiti upatikanaji wa malighafi sasa na wakati ujao.

·      Kutathmini ubora na bei za malighafi na njia mbadala za kupata malighafi. 

 

4. Uongozi/Organisation;

·      Jinsi muundo wa uongozi wa biashara utakavyokuwa?

·      Ni kina nani watakaounda menejiment?

·      Uwezo wao ni upi?

·      Uwezo wao utasaidiaje biashara?

·      Wana uaminifu gani?

·      Udhaifu wao utarekebishwaje?

·      Idadi ya watu watakaoajiriwa ni wangapi?

·      Je upo mpango wa kuwapeleka mafunzoni (course)? 

 

Fedha/Financials 

·      Mahitaji yote ya biashara ni shilingi ngapi?

·      Ni kiasi gani cha fedha zitakazotumika kuiendesha?

·      Fedha hizo zitapatikana toka wapi?

·      Matarajio ya mauzo kwa mwezi, mwaka, yatakuwa kiasi gani?

·      Faida itaanza kupatikana baada ya muda gani kupita?

·      Kuna uhitaji wowote wa kukopa mahali ili kuweza kutimiza malengo waliyojipangia?

·      Kuna haja ya kutafuta wabia zaidi?

·      Biashara itarudisha mtaji baada ya muda gani kupita?

 

NJIA KUU 2 ZA KUFANYA UTAFITI WA BIASHARA

Jinsi wamiliki wa Upendo Cafe  Bibi Gladius na Mariam walivyofanya utafiti wao kupata majibu kwa maswali mbalimbali yaliyotajwa hapo juu kuhusiana na biashara yao hii,  iliwabidi kutumia njia hizi mbili zifuatazo;


1. Utafiti wa Msingi (Kuzungumza na watu ana kwa ana)

Waliwafuata moja kwa moja wadau mbalimbali wa biashara za vyakula kama vile wamiliki wa mikahawa, cafe na hoteli, wateja wa vyakula, wauzaji wa malighafi za vyakula taasisi mbalimbali zinazojihusisha au kusimamia biashara za vyakula zikiwemo zile za serikali na za watu binafsi.  nk. kisha kuwauliza maswali mbalimbali kama tulivyoona kwenye orodha pale juu, lengo likiwa ni kupata majibu yake kwa usahihi. 

 

2. Utafiti wa Dawati (Kusoma machapisho na vyombo vingine vya habari)

Walisoma pia machapisho nje na ndani ya mitandao pamoja na kufuatilia vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na biashara hii ya chakula.

Katika vipengele vyote vikubwa 3 walivyochunguza, soko ndiyo kitu muhimu zaidi na kilichohitaji majibu yenye uhakika mkubwa kwani kuanguka au kushamiri kwa biashara yeyote ile kunategemea sana kitu hiki, soko. Ilikuwa ni lazima kulijua soko lao vizuri na kwa kina sana ili kujiridhisha ikiwa kama kweli biashara hii inao uwezo wa kuwaletea faida. Ijapokuwa biashara ya cafe ni moja ya biashara yenye faida kubwa na ya haraka wakati mwingine hata mara 2 ya mtaji uliowekezwa lakini ukikosea kwenye soko hasa eneo basi utaishia kulia na kusaga meno  

Majibu ya maswali hayo yote yatawawezesha hapo baadae katika kuandika mpango wa biashara hii kuweka mikakati mbalimbali ya kufanikisha biashara yao. 

 

NJIA KUU 3 UNAZOWEZA KUZITUMIA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YAKO

 

Baada ya kufanya utafiti wa biashara yako na kufahamu mambo mengi kuihusu sasa unaweza kuandika mpango wa biashara yako ya Cafe au nyingine yeyote kwa kutumia moja kati ya njia 3 zifuatazo; 

1.   kufuata mfululizo wa vipengele vinavyounda mpango wa biashara

2.   .......................................................

3.   ....................................................... 

Ili kupata somo lililokamilika, tafadhali Jiunge na darasa letu la Michanganuo-online

Hapa kwenye somo hili nitatumia njia ya 1 ya kufuata mfululizo wa vipengele vinavyounda mpango wa biashara. Mlolongo wa vipengele hivyo muhimu ni huu ufuatao;  

 

1.0 MUHTASARI TENDAJI 

 

2.0 MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA

2.1 Malengo

2.2 Dhamira kuu

2.3 Siri za mafanikio

2.4 Umiliki wa Biashara

2.5 Kianzio(kwa biashara mpya au historia kwa kampuni

       iliyokwishaanza)

2.6 Eneo la biashara na vitu vilivyopo 

 

3.0 BIDHAA au HUDUMA

3.1 Maelezo ya bidhaa/huduma

3.2 Utofauti wa bidhaa/huduma na za washindani

3.3 Vyanzo vya malighafi/bidhaa

3.4 Kopi za matangazo

3.5 Teknolojia

3.6 Bidhaa au Huduma za baadae 

 

4.0 TATHMINI YA SOKO

4.1 Mgawanyo wa soko

4.2 Soko lengwa 

4.2.1 Mahitaji ya soko

4.2.2 Mwelekeo wa soko

4.2.3 Ukuaji wa soko

4.3 Tathmini ya sekta

4.3.1 Washiriki katika sekta

4.3.2 Usambazaji 4.3.3 Ushindani

4.3.4 Washindani wako wakubwa 

 

 

5.0 MIKAKATI NA UTEKELEZAJI

5.1 Nguvu za kiushindani

5.2 Mkakati wa soko

5.2.1Kauli ya kujipanga katika soko

5.2.2 Mkakati wa bei

5.2.3 Mkakati wa matangazo/promosheni

5.2.4 Programu za masoko

5.3 Mkakati wa mauzo

5.3.1 Makisio ya mauzo

5.3.2 Programu za mauzo

5.4 Mkakati wa ushirikiano

5.5 Vitendo na utekelezaji

5.5.1 Uendeshaji

 

6.0 MAELEZO YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI

6.1 Mfumo wa uongozi

6.2 Timu ya uongozi na wafanyakazi

6.3 Mpango wa mishahara  

 

7.0 MPANGO WA FEDHA

7.1 Dhana/makisio muhimu

7.2 Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even

      Analysis)

7.3 Makisio ya faida na hasara

7.4 Makisio ya mtiririko wa fedha

7.5 Makisio ya mali na madeni (mizania ya biashara)

7.6 Sehemu muhimu za biashara

 

8.0 VIELELEZO/VIAMBATANISHO

• Taarifa za mahesabu ya fedha kwa undani

• Mahesabu yako ya nyuma

• Leseni, vibali ripoti za kodi, hatimiliki na alama za biashara

• Mikataba mbalimbali

• Orodha ya mali na vifaa mbalimbali (Dhamana)

• CV za viongozi na wafanyakazi muhimu

• Kopi za matangazo ya biashara. 

 

JALADA LA NJE LA MPANGO WA BIASHARA

Jalada la nje au (Cover page), hiki siyo moja kati ya vipengele vya mpango wa biashara lakini ni sehemu muhimu sana na ambayo ndiyo msomaji wa mpango wako huanza kukutana nayo mbele kabisa kabla hajafungua ndani kuona kuna nini.

Juu ya  jalada au ‘cover page’ panawekwa vitu vifuatavyo;

1.   Jina la biashara/kampuni

2.   Mwaka na tarehe ya kuandikwa

3.   Anuani ya biashara

4.   Unaweza pia ukaweka namba ya toleo, majina ya walioandaa, logo ya biashara/kampuni pamoja na hadhira (kwa wale mpango unakolengwa kwenda).


Hata ikiwa hutaweka kila kitu kilichoorodheshwa hapo juu lakini angalau jina la biashara, mwaka na anuani ya mwandishi au biashara visikosekane. Jalada la mchanganuo wa biashara ya Upendo Cafe unaweza kuliona hapa chini;


Mpaka kufikia hapo, kwa siku ya leo tumefika mwisho wa somo letu la kuandika mchanganuo wa biashara ya chakula ya UPENDO CAFE hatua kwa hatua. Tukutane tena kesho tarehe 26/12/2022 na tutajifunza vitu vifuatavyo;


1.   Muhtasari Tendaji (Executive Summary)

2.   Maelezo ya Biashara/Kampuni (Business Description)

3.   Maelezo ya Bidhaa/Huduma (Products/Service Description)


Kumbuka pia mwisho wa somo hili tutaunganisha vipengele vyote 8 na kupata mchanganuo kamili wa biashara hii ya UPENDO CAFE.

Kupata mfululizo kamili wa mafunzo haya, jiunge na Familia yetu ya MICHANGANUO-ONLINE mahali ambapo tunajifunza michanganuo ya biashara kwa kina kabisa pamoja na masomo adimu ya fedha usiyoweza kuyapata mwingine kokote.

Kujiunga lipia ada yako ya mwaka sh. Elfu 10 kwa namba 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo na nitakuunganisha papo hapo pamoja na kukutumia vitabu na michanganuo ya bure. Ndani ya channel yetu ya Telegram pia utakutana na Masomo mengine yote ya fedha tuliyojifunza siku za nyuma.

Njoo na swali lolote kuhusu michanganuo na ikiwa una Biashara yeyote ile ambayo ungependa tuiandikie mchanganuo wake hatua kwa hatua ndani ya group njoo nayo pia. Usikose kesho muendelezo wa somo hili.


Somo limeandaliwa na

Peter Augustino Tarimo

Business Plan expert

 

SOMA NA HIZI PIA:

1. Biashara ya mgahawa wa chakula; mchanganuo na mtaji mdogo wa kuanza


2. Biashara ya chakula usipokuwa msafi utaiona chungu


3. Unajua bishara ya chipsi kuku, soda inavyolipa Dar?


4. Chakula cha kuku wa kienyeji kina tofauti gani na cha kuku wa kisasa?


0 Response to "KUANDIKA MPANGO KAMILI WA BIASHARA YA CAFE, MTAJI MILIONI 3 (3,000,000/=)"

Post a Comment