NJIA TISA (9) ZA KUKUSAIDIA KUVUTA PESA, BAHATI NA MAFANIKIO 2023 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NJIA TISA (9) ZA KUKUSAIDIA KUVUTA PESA, BAHATI NA MAFANIKIO 2023

Bahati, pesa na utajiri

Utajibu vipi kama nikikuuliza, Je, unataka mwaka 2023 ujaliwe bahati, pesa na kila fursa za mafanikio? Ikiwa jibu lako ni ndiyo, basi somo hili ni kwa ajili yako, endelea kusoma. Ikiwa jibu ni hapana, basi samahani naomba uishie hapohapo na muda wako ukafanye jambo jingine chanya la kukusaidia maishani.

Duniani hakuna mtu anayeweza akapinga kwamba bahati zipo na mtu yeyote yule anaweza akaipata, lakini pia ninaamini kwamba mtu anaweza akajitengenezea bahati yeye mwenyewe kwa kudhamiria.

Zifuatazo ni njia 9 za nguvu mtu unazoweza kuzifuata mwaka huu mpya wa 2023 na ukajitengenezea chansi kubwa ya wewe kupata mafanikio makubwa na bahati maishani.

 

2. Rekebisha upya mtazamo wako juu ya pesa

Ni nini unachoamini juu ya pesa? Je, unaamini kwamba pesa ni shetani na kamwe tajiri hatauona ufalme wa Mbinguni? Kama unaamini hivyo na vitu vingine vinavyofanana navyo, basi kuanzia sasa acha kabisa na uanze kuamini kwamba unastahili kumiliki utajiri, kwamba pesa ni kitu kizuri na pia anza mara moja kufikiria mambo yote mazuri unayoweza kuyafanya kwa kutumia pesa. Ndiyo, unastahili kuwa na pesa hivyo zidai ni haki yako!


3. Kuwa mvumilivu

Waswahili wana usemi usemao, Roma haikujengwa kwa siku moja. Kiukweli Roma inayosifika leo hii ilijengwa ukuta kwa ukuta, jiwe kwa jiwe na Watawala au Wafalme zaidi ya 70 katika nyakati tofauti. Na wewe sasa amua ni kitu gani unachokitaka kisha uanze kwa vitendo kufanyia kazi malengo yako hayo kwa uvumilivu mkubwa. Uvumilivu siyo blaa blaa wala maneno matupu bali kitu cha kutia kwenye matendo.

 

5. Kufikiri Chanya

Watu walio na fikra chanya siku zote ndio walio na bahati. Wanao uwezo mkubwa na wa ajabu wa kuziona fursa na suluhisho mahali ambapo walio na fikra hasi hawawezi kamwe kuona. Kuna usemi mwingine mashuhuri ndani ya kitabu cha Fikiri & Utajirike usemao, Kile unachofikiri siku zote ndicho unachokuwa, hivyo anza sasa hivi kujijengea fikra chanya akilini mwako kwani hakuna chochote kile kizuri unachoweza kukipata kwa kuanza kufikiria karibu kila kitu katika mlengo hasi.


6. Kuwa na Maono

Ikiwa kitu huwezi kwanza kukimiliki akilini basi na kamwe hutaweza kukimiliki mkononi, Hii ni busara nyingine kubwa niliyojifunza ndani ya kitabu cha Fikiri & Utajirike (Think & Grow rich). Matajiri wote uwaonao leo, waliota kwanza utajiri wao akilini kabla hawajaupata. Anza sasa kuwaza na kuona akilini mwako kila bahati na utajiri duniani vikivutwa kwako mithili ya vile sumaku ivutapo misumari au vyumavyuma vingine.

 

8. Fahamu kile unachokitaka

Ikiwa kama Pesa ndiyo kitu unachotaka kukipata mwaka 2023, ni wakati sasa wa kuchagua, andika mahali malengo yako na hatua za kuchukua ili kuyafikia. Kama malengo yako ni ya kiafya pia fanya hivyohivyo, andika ungetaka pengine kupunguza uzito kilo ngapi na utaruka kamba kila siku mara ngapi nk. Unataka kuanzisha biashara fulani au ungependa kuiboost biashara ndogo uliyonayo ili ikuingizie pesa hata kama umelala usiku? Chukua kalamu na karatasi andika mikakati yako hata kama siyo kwa undani sana au njoo MICHANGANUO=ONLINE tunaandika michanganuo kila siku na malengo ya biashara mbalimbali.


9. Samehe na Sahau

Watu walio na bahati za mtende huwa kamwe hawachafui ulimwengu wao kwa vitu hasi. Wanajua roho ya Ibilisi ipo na inaishi. Kwahiyo kuwa makini sana na nguvu unazozitoa. Msamehe kila mtu aliyekutendea ubaya na uwatakie kheri. Kuondoa vizingiti kutakufungua mwenyewe ili bahati iweze kugeuza makazi ya Neema na Utajiri ndani yako .

........................................................

 

Mpendwa mdau wa blogu hii, niwie radhi kwa kutokuweka makala hii hapa nzima, utaona nilitaja njia 9 lakini ya 1, ya 4 na ya 7 hazipo, sababu ni kwamba tuna masomo ya aina mbili, kwa ajili ya group la MICHANGANUO na megine kwa ajili ya blogu hii. Hili ni la group na hapa tunaweka sehemu tu, mtu akivutiwa basi anajiunga na group kupata masomo kamili. Zamu ya somo la blogu tunaweka somo kamili.

Tunayo masomo zaidi ya 100 ya kipekee katika channel ya MICHANGANUO-ONLINE ambayo kila mwanachama anuwezo wa kuyasoma yote. Unakaribihswa sana kupata na offa yetu ya vitu 22+ leo kwani kesho ndiyo mwisho wake

Mafunzo ya kuandika mchanganuo wa UPENDO CAFE nayo yanaendelea na leo ni siku ya pili ambapo tutaandika maelezo ya Biashara na Bidhaa/huduma hatua kwa hatua. Bofya hapa>>> kusoma dondoo za somo la jana

Kucheki jinsi wadau wanavyo changamkia Offa na vitabu vyetu bofya hayo maandishi.

 

SOMA PIA NA HIZI HAPA;

1. Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wengi?

2. Je, ipo kanuni ya mafanikio ya kifedha? Mtazamo wa kisaikolojia

3. Salamu zangu mwaka mpya kukutakia heri na mfanikio ya kweli 2023

4. Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio & utajiri wa haraka 0 Response to "NJIA TISA (9) ZA KUKUSAIDIA KUVUTA PESA, BAHATI NA MAFANIKIO 2023"

Post a Comment