NAANZA UTUMISHI JANUARI, NIFANYEJE KUWA HURU KIFEDHA AU NIKAKOPE? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NAANZA UTUMISHI JANUARI, NIFANYEJE KUWA HURU KIFEDHA AU NIKAKOPE?


Ndugu msomaji wangu karibu tena katika makala ya Ushauri ambapo tunaweka hapa katika blogu ushauri kwa msomaji aliyetutumia swali au changamoto anayokumbana nayo kuhusiana na ujasiriamali au biashara kwa ujumla. Leo hii kuna msomaji mmoja yeye kauliza kama ifuatavyo

“Nataraji kuanza utumishi mwezi wa kwanza, na kabla ya hapo niliwahi kumsaidia kaka yangu kazi ya kuuza duka la vifaa, hata hivyo nikiwa mtumishi ningependa kuwa huru kifedha kwa kuanzisha mradi wangu mwenyewe wakati nikiendelea na utumishi sasa swali ni je, itawezekana au lazima nijiingize kwenye mkopo?”

SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, nipeni ushauri nina wakati mgumu.

MAJIBU.
Asante sana na hongera ndugu yangu kwa ajira na malengo uliyokuwa nayo. Upo sahihi kabisa kwani utumishi tofauti na baadhi ya watu wengine wanavyouchukulia, siyo kitu kibaya bali ni chanzo kizuri sana na cha uhakika cha mtaji kwa ajili ya kuwekeza katika shughuli nyinginezo za kiuchumi na biashara.

Bila shaka umepata uzoefu kiasi fulani kutoka katika hilo duka la ndugu yako, na hiyo ni faida pia. Ninachokushauri hasa ni kwamba, chukua muda wa kutosha kufanya maandalizi ya biashara au uwekezaji wowote ule utakaoufanya wakati ungali ukifanya utumishi wako. Kumbuka utakuwa na muda ‘limited’ sana nikimaanisha muda kidogo. Hivyo shughuli utakayoianzisha ni lazima uiwekee mfumo(system) madhubuti ambayo haitaingiliana na utumishi wako hata kidogo.

SOMA: Kutumia nyumba, kiwanja au ardhi kama rehani kuomba mkopo ni sahihi? naomba ushauri. 

Zingatia sana hili:  usikubali hata kidogo ‘kuisacrifice’ kuitoa sadaka ajira yako kwa ajili ya shughuli ya kujiajiri mwenyewe kabla haujahakikisha shughuli ama biashara hiyo inao uwezo wa kukutiririshia pesa zinazozidi pesa unazotumia(mtiririko wako wa fedha kuwa chanya), matokeo yake utakwama vibaya sana na maisha yako kiuchumi yanaweza kwenda kuvurugika.

Suala la kukopa sikushauri uliwekee kipaumbele cha kwanza japo baadaye haliwezi kuepukika. Katika hatua za awali mradi wowote ule wa kibiashara ni vizuri zaidi kufadhiliwa na vyanzo vya pesa ambavyo siyo mikopo hasa hii ya riba kwani iwapo itatokea mradi kutofaulu madhara yake huwa makubwa na magumu kuhimili. Mkopo ni mzuri pale biashara inapoanza kujitegemea yenyewe na kuzalisha mapato ya uhakika. Labda mkopo wenyewe uwe ni kiasi kidogo sana ambacho hata mtaji ukikatika hautasumbuka kuurejesha.

Asante, nakutakia kila la kheri katika majukumu yako.

Peter Tarimo
Self help books Tanzania.

…………………………………………………….

Ndugu msomaji nakualika katika SEMINA kwenye blogu ya private ya kulipia itakayoanza tarehe 3 siku ya Alhamisi mwezi wa kwanza. Somo kuu ni JINSI YA KUUFANYA MZUNGUKO WAKO WA FEDHA KUWA CHANYA MWAKA HUU WA 2018 na tutakuwa tukijifunza mawazo na biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza pesa kwa uhakika. Mawazo ya biashara hizo ni ya kipekee na yaliyofanyiwa utafiti wa kutosha uliothibitika kuzalisha faida haraka na kwa urahisi huku ukitumia mtaji kidogo unaoweza kuumudu. Tutakuwa pia na mpango mkakati mzima wa biashara hizo.

 KIINGILIO ni shilingi elfu 10 tu, na unapata fursa ya kusoma na semina nyingine zote zilizopita pamoja na fursa ya kuingia semina nyingine zote zitakazofuata bila kulipa tena kiingilio. Unapewa na kitabu cha michanganuo ya biashara na ujasiriamali bure. Offa ya kitabu itadumu kwa muda maalumu tu.


Malipo ni kupitia namba 0712202244  au  0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Tuma na anuani yako ya GMAIL(isiwe yahoo wala aina nyinginezo) kwa ajili ya kukuunganisha na blogu ya masomo.

Vitabu navyo vipo kwa anayehitaji tuwasiliane kwa namba hizo hapo juu, kwa  SOFTCOPY tuma pesa na anuani yako ya email tutakutumia udownload popote pale ulipo. Kwa HARDCOPY ukiwa Dar  tunakuletea mpaka ulipo kwa gharama ya ziada ya sh. 2,000/= na mikoani tunatuma kwa basi au muagize mtu anayefika Dar akuchukulie kutoka kwetu.

HARDCOPY  TSH. 20,000
SOFTCOPY   TSH. 10,000


HARDCOPY  TSH. 10,000
SOFTCOPY   TSH. 5,000



HARDCOPY  TSH. 5,000
SOFTCOPY   TSH. 3,000
  

Kwa maelezo vitabu zaidi tembelea SMARTBOOKSTZ

0 Response to "NAANZA UTUMISHI JANUARI, NIFANYEJE KUWA HURU KIFEDHA AU NIKAKOPE?"

Post a Comment