LILE UNALOFIKIRI(WAZA) AKILINI, ZURI AU BAYA NDILO HUTOKEA KUWA KWELI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

LILE UNALOFIKIRI(WAZA) AKILINI, ZURI AU BAYA NDILO HUTOKEA KUWA KWELI.

Kinachoipa nguvu kanuni hii ni sheria ya asili ambayo hamna mtu yeyote bado anayeweza kuielezea. Imewakanganya wanasayansi wa zama zote, wanasaikolojia wameipa sheria hii jina, “kujishauri binafsi”, na iache iwe hivyo. Jina ambalo mtu ataiita sheria hii halina umuhimu mkubwa. Jambo muhimu kuihusu ni kuwa, inafanya kazi kwa utukufu na mafanikio ya mwanadamu ikiwa itatumiwa katika hali ya kujenga.

Kama itatumiwa katika hali ya kubomoa, kwa upande mwingine itafanya uharibifu kwa kiwango kilekile. Katika kauli hii unaweza ukapatikana ukweli wenye maana: wale ambao huanguka chini kwa kushindwa na kumalizia uhai wao katika umasikini, taabu na masikitiko, huwa hivyo kutokana na matumizi hasi ya kanuni ya kujishauri binafsi.

Sababu inaweza kuwa hivyo kutokana na ukweli kwamba, MISUKUMO YOTE YA FIKRA INA TABIA YA KUJIVIKA YENYEWE KATIKA HALI YAKE YA KITU HALISI KINACHOWEZA KUONEKANA.

Akili ya ndani(Maabara ya kikemikali ambamo misukumo yote ya fikra hukusanywa na kufanywa tayari kubadilishwa kuwa ukweli halisi unaoweza kuonekana) haiwezi kutofautisha kati ya misukumo ya fikra inayojenga na ile inayobomoa. Hufanya kazi na chochote kile tunachoilisha  kupitia misukumo yetu ya fikra. Akili ya ndani itatafsiri kuwa ukweli wazo linaloongozwa na hofu sawa sawa kama vile itakavyotafsiri kuwa kweli wazo linalochochewa na ujasiri au imani.

Kurasa za historia ya utabibu zimejaa maelezo ya kesi za “vifo vya kujishauri”. Mtu anaweza akajiua kutokana na fikra hasi, sawa kama vile ambavyo angelijiua kutokana na sababu nyinginezo. Katika mji wa Midwestern City, afisa mmoja wa benki aliyeitwa Joseph Grant aliazima kiasi kikubwa cha fedha za benki bila ya idhini ya wakurugenzi. 

Alipoteza fedha zile kwenye kamari. Siku moja mchana  mkaguzi wa benki alikuja na kuanza kukagua hesabu. Grant aliondoka benki na kwenda kuchukua chumba katika hoteli  moja mtaani. Walipokuja kumkuta siku tatu baadae, alikuwa amelala kitandani akilia kwa huzuni na kuomboleza, akirudia tena na tena maneno haya; “Mungu wangu, hili litaniua! Sitaweza kuhimili aibu hii”. Baada ya muda mfupi aliaga dunia. Madaktari walitoa taarifa kwamba kifo kile kilitokana na “Kujiua mwenyewe kiakili”.

Kama vile umeme utakavyozungusha matairi ya kiwanda na kuzalisha huduma zenye maana ikiwa utatumiwa vizuri, au kukatisha uhai ikiwa utatumiwa vibaya, na hivyo hivyo ndivyo sheria ya kujishauribinafsi itakavyokuongoza kwenye  amani na utajiri au chini katika shimo la mateso, maanguko na kifo. Yote itategemea kiwango chako cha uelewa na matumizi yake.

Ikiwa utaijaza akili yako hofu, mashaka na kutokuamini katika uwezo wako wa kujiunganisha na kutumia nguvu kuu zilizo chanzo cha viumbe vyote, sheria ya kujishauri binafsi itaichukua roho hii ya kutokuamini na kuitumia kama kielelezo ambacho akili yako ya ndani itatafsiri kuwa katika kitu  chenye umbo lake halisi.
KAULI HII INA UKWELI SAWA KAMA ILIVYOKUWA KAULI KUWA MBILI NA MBILI NI SAWA NA NNE!

Kama ilivyokuwa upepo ubebao meli moja Mashariki na nyingine Magharibi, sheria ya kujishauribinafsi itakunyanyua juu au kukushusha  chini, kulingana na vile jinsi utakavyoyaendesha mawazo(fikra) zako. Sheria ya kujishauri binafsi ambayo mtu yeyote anaweza akaitumia kufikia urefu wa mafanikio yanayoshangaza akili yanaelezewa vizuri katika shairi lifuatalo;

Ikiwa utafikiria umeshindwa, umeshindwa,
Ikiwa utafikiri haustahili, hustahili kweli
Kama unapenda kushinda, lakini unawaza hautaweza,
Bila shaka hautaweza.

Ikiwa unafikiri utapoteza, umepoteza
Kutoka duniani tunakuta,
Mafanikio huanza na utashi wa mtu-
Vyote vikiwa katika hali ya akili.

Ikiwa unawaza wewe ni bora, upo hivyo,
Unatakiwa uwaze juu ili kuinuka,
Unatakiwa kuwa na uhakika na wewe mwenyewe kabla
Unaweza kushinda zawadi wakati wowote

Vita ya maisha mara nyingi haiendi
Kwa mwenye nguvu zaidi au mbio,
Lakini mapema au baadae anayeshinda
Ni yule ANAYEWAZA(KUFIKIRI) ANAWEZA!

Chunguza maneno yaliyotiliwa mkazo, na utapata maana ya ndani shairi iliyokusudia. Mahali fulani mwilini mwako(pengine katika seli za ubongo wako) imelala mbegu ya ushindi. Ikiwa itaamshwa na kutiwa katika vitendo, hii inaweza ikakufikisha kileleni kiasi ambacho hukuwahi kutumaini kufika.

Kama ilivyo kwa mwanamuziki mahiri anavyoweza akasababisha mapigo mazuri zaidi ya muziki kumiminika kutoka katika nyuzi za gitaa, ndivyo na wewe unavyoweza ukaamsha kipaji kilicholala kwenye ubongo wako, na kukisababisha kukunyanyua juu kuelekea lengo lolote unalotamani kukamilisha.

Abraham Lincoln alikuwa akishindwa katika kila jambo alilojaribu kufanya mpaka pale alipopitisha umri wa miaka 40. Alikuwa “Bwana Asiyejulikana kutoka Kusikojulikana” mpaka pale uzoefu mkubwa ulipokuja katika maisha yake, ukaamsha kipaji kilichokuwa kimelala ndani ya moyo na ubongo wake, na kuipatia dunia  mmoja kati ya watu wake mashuhuri.

“Uzoefu” huo ulikuwa umechanganyika na mihemko ya huzuni na upendo. Ilikuja kwake kupitia Anne Rutledge, mwanamke pekee aliyempenda kweli daima.

Ni ukweli unaofahamika kuwa mhemko wa mapenzi una uhusiano wa karibu na hali ya akili ijulikanayo kama Imani. Mapenzi huja karibu sana kwenye kutafsiri msukumo wa fikra wa mtu kwenda katika upande wake wa pili wa kiroho.

Wakati akifanya utafiti wake, mwandishi aligundua kutokana na tathmini ya kazi na mafanikio ya mamia ya watu wenye utajiri unaoonekana, kwamba kulikuwa na ushawishi wa mapenzi ya mwanamke nyuma ya karibu kila mmoja wao.

Mhemko wa mapenzi katika moyo na ubongo wa binadamu, hutengeneza mazingira yanayofaa ya uvutano wa kisumaku. Hii husababisha kumiminika ndani kwa mitetemo ya juu na laini ambayo huelea katika anga(ether)

Hebu tuangalie nguvu ya Imani kama ilivyothihirishwa na mtu anayefahamika vizuri kwa kila Ustaarabu, Mahatma Gandhi wa India. Kwa mtu huyu dunia ilishuhudia moja kati ya mifano ya kushangaza zaidi ya uwezekano(fursa) za IMANI. Gandhi  alitawala uwezo mkubwa wa nguvu isiyothihirika kushinda mtu mwingine yeyote aliyeishi katika wakati wake, na hii licha ya ukweli kwamba hakuwa na zana halisi za kutawala kama vile, pesa, meli za kivita, askari na zana za kivita. Gandhi hakuwa na pesa. Hakuwa na nyumba. Hakumiliki hata suti moja ya nguo lakini alikuwa na nguvu.

Ni kwa jinsi gani alizipata nguvu hizo?
ALIZITENGENEZA KUTOKANA NA UELEWA WAKE WA KANUNI YA IMANI NA KWA KUPITIA UWEZO WAKE WA KUPANDIKIZA IMANI HIYO KATIKA AKILI ZA WATU MILIONI 200.

Gandhi alitimiza kwa kupitia ushawishi wa Imani, kitu ambacho tawala zenye nguvu za kijeshi duniani zisingeliweza kutimiza, na kamwe hazitoweza kutimiza kwa kutumia wanajeshi na vifaa vya kivita. Alitimiza tendo gumu na la ajabu la kushawishi akili milioni 200 kuungana na kusonga mbele katika umoja, kama akili moja. Ni nguvu gani juu ya dunia isipokuwa Imani, ingeliweza kutenda kiasi hicho?.

Kaulimbiu ya wakati ujao itakuwa ni furaha ya binadamu na kuridhika. Hali hii ya akili inapokuwa imefikiwa, uzalishaji utajiendesha wenyewe kwa ufanisi zaidi kuliko kitu chochote kilichowahi kukamilishwa wakati watu walipokuwa hawachanganyi au wanashindwa kuchanganya imani na matamanio binafsi pamoja na kazi.

Kutokana na uhitaji wa imani na ushirikiano katika biashara na viwanda, litakuwa ni jambo la kuvutia na lenye faida kulitathmini tukio maalumu. Hili hutoa uelewa mzuri kabisa wa njia ambayo wenye viwanda na viongozi wa makampuni hujichumia utajiri kwa kutoa kabla hawajapata. Tukio lililochaguliwa kwa ajili ya maelezo haya lilitokea huko nyuma mwaka 1900, wakati Shirika la Kimarekani la Chuma cha pua(United States Steel Corporation) lilipoundwa. Kama utakavyo isoma simulizi hii, zingatia  akilini ukweli huu na utafahamu jinsi wazo lilivyobadilishwa kuwa utajiri mkubwa.

Kwanza shirika kubwa la Kimarekani la chuma cha pua lilizaliwa katika akili ya Charles M. Schwab katika hali ya wazo aliloliunda kupitia ubunifu wake. Pili, alichanganya imani na wazo lake. Tatu, alitengeneza mpango kwa ajili ya kulibadilisha wazo lake kuwa katika kitu halisi na ukweli kifedha.

Nne, aliuweka mpango wake katika vitendo kwa hotuba yake maarufu katika Klabu ya Chuo Kikuu. Tano, alitekeleza na kuufuata mpango wake kwa uvumilivu pasipo kuacha huku akiusaidia na maamuzi thabiti mpaka pale ulipoanza kufanya kazi. Sita, aliandaa njia ya mafanikio kwa shauku kali ya kufanikiwa

Ikiwa mara nyingi umekuwa ukishangaa ni jinsi gani utajiri mkubwa unavyopatikana, simulizi hii ya kuundwa kwa Shirika la Chuma Cha Pua la Marekani itakupa mwangaza. Kama unayo shaka yeyote kwamba watu wanaweza Wakafikiri na Kuwa Matajiri, simulizi hii inapaswa kukuondoa shaka hiyo kwa sababu ndani yake  unaweza ukaona wazi matumizi ya sehemu kubwa ya Kanuni 13 zilizoelezewa katika kitabu hiki.

John Lowel katika gazeti la New York World-Telegram, kwa heshima yake hapa, imerudiwa kuchapishwa simulizi nzuri ya kushangaza ya nguvu ya wazo.

………………………………………………………………………..

Mpenzi msomaji, usikose  sehemu ya (iv) ya sura hii ya 3 ya “Kitabu cha pesa na mafanikio maarufu zaidi duniani FIKIRI UTAJIRIKE AU THINK & GROW RICH (MSAHAFU WA MAFANIKIO)”.


Pia kwa vitabu vyako mbalimbali vya Biashara na Ujasiriamali katika lugha ya kiswahili, bonyeza SMART BOOKS TANZANIA.
0 Response to "LILE UNALOFIKIRI(WAZA) AKILINI, ZURI AU BAYA NDILO HUTOKEA KUWA KWELI."

Post a Comment