Habari za muda huu ndugu msomaji wa blog ya jifunzeujasiriamali;
Karibu
kwa makala nyingine tena tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka 2024 na kuanza mwaka
mpya wa 2025. Kama kaulimbiu yetu ya mwaka inavyosema; “MAKE YOURSELF GREAT
AGAIN” tunaendelea na makala na masomo yanayoamsha ndani yetu ari ya kupambana
kurudisha ukuu uliopotea ama kujenga ukuu utakaotusaidia kwenye maisha yetu
yajayo hasa kiuchumi.
Kabla ya Donald Trump kushinda kura ya Urais Marekani
niliandika makala iliyosema, KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO ULIOPOTEA au MAKE YOURSELF GREAT
AGAIN, nikasema kwamba mwaka 2025 hiyo ndiyo itakayokuwa kaulimbiu yetu kuu
Blog ya jifunzeujasiriamali, tukilenga kujifunza na kuhamasishana mbinu
mbalimbali za mafanikio kwenye biashara bila kujali uliwahi kufanikiwa ukaja
kufeli au ndio kwanza unaanza safari yako ya utafutaji pesa.
Nilisema kutumia kaulimbiu hii ya Trump simaanishi kwamba
mimi ni shabiki kindakindaki wa siasa za Trump au chama cha Republican nchini
Marekani hapana, bali niseme tu ukweli mimi ni shabiki mkubwa wa mikakati ya
kibiashara ya Bwana Trump ambayo bila shaka mikakati hiyo pia ameweza kuitumia
kwenye siasa na ikampatia mafanikio makubwa.
SOMA: Jinsi ya kuanzisha biashara ya uwekezaji kwenye ardhi na
majengo hata kama huna mia mfukoni
Sasa leo hii nitazumngumzia vitu vikubwa vine (4) ambavyo
bila shaka Donald Trump Bilionea wa biashara ya uwekezaji kwenye ardhi na
majengo (Real Estate) alivitumia kikamilifu hatimaye akaweza kuibuka kidedea
kwenye kinyanganyiro cha uchaguzi licha ya kura za maoni mpaka dakika za
majeruhi kuonyesha Bibi Harris alikuwa akienda kumbwaga vibaya Trump. Mikakati
hiyo ni hii hapa chini;
1.
Usijaribu kuligundua tairi upya (You can’t
Reinvent the Wheel)
Hakuna tatizo jipya chini ya jua, karibu kila kitu
unachojaribu kuwaza kuna mtu mwingine alishawahi kufanya hivyo na wengine
kupata suluhisho kabisa, kwa hiyo wewe jambo la msingi ni kutumia masuluhisho
yao kutatua tatizo lako uokoe muda wa kuanza kuhangaika kugundua suluhisho lako
jipya mwenyewe.
SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza corona tanzania kubusti
uchumi wako unaosambaratika
Trump kwa mfano alifahamu fika ya kwamba mtandao maarufu
wa Twitter (sasa X) ulikuwa ni Game
changer kwake, lakini angelifanya nini wakati tayari mmiliki wake wa mwanzo
Jack Dorsey akishirikiana na maadui zake kisiasa walikwisha mpiga marufuku
kuutumia na hata kudelete kabisa account yake?
Ni nani ajuaye ikiwa swahiba yake Trump Bilionea namba
moja Duniani Elon Musk ulikuwa ni mkakati maalumu waliokuwa wameupanga na Trump
kuinunua Twitter mwaka 2021 ili baadae ije kuwapiga tafu?
SOMA: Kamwe, kamwe, usikate tamaa(never, never give up)
Pamoja na Trump kuhangaika kuanzisha jukwaa lake jipya
mwenyewe liitwalo TRUTH lakini ukweli ni kwamba lisingeweza katika kipindi
kifupi namna ile kuvutia idadi kubwa ya watu ambao Twitter ilikuwa imevutia,
hivyo hapa utaona kwamba Trump mara moja kwa
kulitambua hilo hakukubali kirahisirahisi kufanya kampeni zake nje ya
jukwaa la X au Twitter. Trump nje ya Twitter ni sawa na samaki nje ya maji
Somo kuu tunalojifunza hapa ni kwamba angalia kile
kinachofanya kazi uwekeze nguvu zako kwake, tuseme kwa mfano kila siku kwenye
mitaa unayoishi unaona kabisa watu wengi wanakazana kuuza nyanya katika magenge
yao kwa kuwa zinatoka haraka, sasa wewe na mtaji wako kidogo usianze
kubahatisha kuweka gengeni kwako vitu hata hujawahi kuona mtu akiuza mtaani
vitakudodea bure, labda tu iwe mtaji wako siyo wa wasiwasi basi unaweza
kubahatisha vitu namna hiyo.
SOMA: Njia wajanja wanayoitumia kupata matokeo bora zaidi kwa kila
wanachokifanya maishani
Sihamasishi kuiga biashara za watu wengine hapana bali
ninachosisitiza hapa tu ni kwamba, soma kwanza mazingira kuona ni kipi kinawezekana
kwa rasilimali chache ulizokuwa nazo, angalia pia muda ulio nao nk. Kisha
ongeza ubunifu kwa kile unachoiga.
SOMA: Hotuba ya kwanza kabisa ya Rais Donald J. Trump baada ya
kuapishwa kuingia ikulu White house
Trump angeliweza kung’ang’ana tu na jukwaa lake la TRUTH
lakini siamini ikiwa angetoboa ndani ya miezi ile michache iliyokuwa imebakia
uchaguzi ufanyike. Na si hivyo tu, wapinzani wake pia wangeliweza kulitumia
jukwaa hili lenye nguvu la X kumshinda kiurahisi mno.
2.
Pesa ni Ulinzi, pesa ni karibia kila kitu kasoro uhai tu!
Pamoja na kasoro zote za Donald Trump katika Ikulu ya
White House mhula wake wa kwanza, lakini kwa kweli pesa iliweza kumsafishia
njia akarudi tena. Binafsi siamini kabisa ikiwa Trump angekuwa mtu wa kawaida
tu kama marais wengine waliopita angeliweza kurudi tena Ikulu.
SOMA: Je, pesa inaweza kutatua kila tatizo duniani au ndio chanzo cha
matatizo yote?
Tumeshuhudia pesa ikitumika vizuri utaratibu wa kisheria
unaweza ukacheleweshwa hata kama ikiwa hautasitishwa kabisa na ndivyo
tulivyoona kwa kesi za Trump, tunaambiwa tu hazijaamuliwa bado na zinaweza
kucheleweshwa mpaka baada ya kipindi chake kumalizika. Hivi angekuwa mtu
hohehahe asiyeweza kuwalipa wanasheria nguli unadhani angeponyoka kweli?
Siyo siri Elon Musk alitumia pesa “kuwahonga” wapiga kura
kukichagua chama cha Republican ingawa kisheria hakuvunja sheria na hakuna mtu
wa kuhoji ni kwanini atumie pesa zake kwenye kampeni
Sasa ni somo gani tunapata hapa kwenye pesa? Ikiwa
serikali na taasisi kubwa kubwa hutegemea kupata pesa toka sehemu mbalimbali
kwa ajili ya kufanikisha mipango yake mikubwa, hivi wewe na mimi na biashara zetu
hizi ndogondogo au hata za kati si ndiyo kabisa tungehitaji pesa kwa udi na
uvumba?
SOMA: Ili ufanikiwe kuwa tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi
4
Kuanzia sasa hebu amini kwamba ili utoke pale ulipo
unahitaji namna fulani ya uwezeshaji zaidi ya fedha unazopata mwenyewe kila
siku kufanya mambo makubwa zaidi, unahitaji mmoja kati ya watu wafuatao au
wote, wabia, benki, washirika, masponsa au vyovyote vile utakavyowaita wewe
ilimradi tu unawakaribisha walete mtaji kwako ili uweze kufanya zaidi ya vile
unavyoweza kufanya binafsi kwa mtaji kidogo ulio nao.
Ni mambo mangapi umekuwa ukitamani kuyafanya lakini kikwazo
kikubwa kikawa ni PESA? Sisemi ukipata pesa ndiyo muarobaini wa kila kitu
hapana, bali mipango yeyote ile mwisho wa siku inahitaji bajeti ya pesa
kuitekeleza huku pesa hiyo ukiisimamia kikamilifu itumike kulingana na mipango
uliyoweka.
3. Kufanya
utafiti (Research) na kuheshimu matokeo yake
Kabla ya kufanya mradi wa aina yeyote ule uwe ni wa
kibiashara au wa kisiasa ni muhimu sana kufanya kwanza utafiti wa kina na
kuzingatia matokeo yake ili kuepuka makosa yatakayosababisha anguko la mradi
husika. Kosa kubwa lililowagharimu ushindi chama cha Democrats ni kuidharau
kanuni hii. Utafiti siyo wa kura za maoni tu peke yake bali hata matukio ya
nyuma unaweza kuyatumia kwenye utafiti.
Hawakuhitaji maprofesa wa utafiti kubaini Wamarekani
hawajafikia hatua ya kumkubali Mwanamke kuwa Raisi wa Taifa lao, ule uchaguzi
wa Bibi Hilary Clinton na Trump ulitosha kuwapa alama ya tahadhari. Safari hii
wakidanganywa na udhaifu wa Biden na historia ya fujo ya Trump wakadhania
Wamarekani ingekuwa rahisi kuachana na kasumba yao ya ubaguzi wa kijinsia. Bibi
Harris asingepita kirahisi kama angeshindanishwa na wanaume wa chama chake.
Tunapata somo kubwa hapa kwamba, chochote utakachokifanya
kwenye biashara yako ukitaka ufanikiwe basi heshimu matakwa ya wateja wako na
siyo yakwako binafsi.
Usifikirie kwa kuwa wewe unapenda sana juisi ya mapera
basi na dukani kwako ukajaze juisi kibao
za pera ukidhani kila mtu anapendelea kile unachopenda wewe, chunguza kwanza
wateja wa eneo unalofungua biashara yako wanapenda vitu gani ndipo uviagize
vitu hivyo kwa wingi na siyo kuagiza vile unavyojisikia kuvipenda wewe na
familia yako vitakudodea.
SOMA:
Nimetumia mfano huu wa juisi ya pera kwani unanikumbusha
wakati naandika kitabu cha MICHANGANUO
YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI katika sura ya pili inayohusu somo la kufanya utafiti
au upembuzi yakinifu kwenye biashara nilitumia mfano wa mfanyabiashara
aliyekuwa akitafiti soko la juisi za embe na juisi ya pera. Ni moja kati ya
masomo muhimu sana kwenye kitabu hiki wasomaji wengi hunipa mrejesho mara kwa
mara.
4. Kuwa
na Washirika sahihi
Umuhimu wa kuwa na Washirika sahihi tunauona kwa Bwana
Trump, timu yake nzima ya kampeni mpaka mgombea mwenza wake. Kuna watu walihoji
chaguo la Trump kwa atakayeshika nafasi ya umakamu wa Rais kuwa ni mtu
asiyekuwa na jina kubwa lakini yeye ndiye mtu sahihi aliyeona atamfaa. Kitendo
cha kushirikiana na watu kama kina Elon Musk, R.F Kennedy Junior na wengineo
ulikuwa ni mkakati wake mkubwa wa ushindi.
SOMA: Kwanini kundi la kushauriana (master mind group) ni muhimu kwa
kila anayetafuta mafanikio?
Trump ni muumini mkubwa wa kuunda ushirika sahihi na
ukitaka kulithibitisha hili nenda kasome kitabu chake alichoandika
akishirikiana na nguli mwingine mkubwa wa biashara Bwana Robert Kiyosaki
kiitwacho, WHY WE WANT YOU TO BE RICH
Somo tunalolipata hapa ni kuwa kwenye biashara tunapaswa kuwa na washirika mbalimbali tunaoweza kunufaika kutoka kwao lakini pia na wao kunufaika kutoka kwetu. Usifikirie tu ni nini utapata kutoka kwa mshirika bali pia ufikirie ni nini utatoa kwa msirika wako muhimu. Unaweza ukajenga ushirika kupitia magroup ya watsap kama lile la kwetu (MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP 2025) ama hata kuwa na washirika wengine nje ya mitandao.
SOMA: Kitabu baba tajiri na baba masikini (rich dad, poor dad) cha
robert kiyosaki
Naamini katika siri au pointi hizi 4 Donald Trump
alizotumia kupata ushindi na wewe pia zinaweza kukusaidia kwa namna moja ama
nyingine kufanikisha biashara yako mwaka 2025.
Ikiwa basi utapenda kujiunga na Washirika wengine ndani
ya Mastermind group letu la Michanganuo
online 2025 kujifunza zaidi masomo ya ubunifu kwenye biashara karibu nafasi bado zipo chache. Chakufanya ni
kulipia Semina na OFFA ya vitu 11 hapo chini shilingi 10,000/= kisha ujumbe
usemao “NATAKA SEMINA NA OFFA YA MWISHO
MWAKA HUU”
Vitabu na michanganuo hii vitakusaidia kama rejea kwenye
masomo yetu kwa mwaka mzima. OFFA hii ina thamani ya shilingi laki moja lakini
unaipata kwa elfu 10 tu!
Semina ya Kuandika mchanganuo wa biashara ya usagishaji
unga wa Sembe na Dona itafanyika tena tarehe 30/12/2024 mpaka tarehe 7/12/2024
kwa wote ambao hawakupata fursa ya kushiriki semina ya kwanza. Baada ya semina
unaendelea kuwa mwanachama kwa mwaka mzima.
SOMA: Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga safi wa
dona (usado milling)-1
Group letu tunajifunza Michanganuo ya biashara na masomo
ya fedha lakini katika mlengo tofauti kabisa na ilivyozoeleka. Tunazingatia
ubunifu na mbinu za kipekee zinazomwezesha mjasiriamali kukuza haraka mtaji
wake hata ikiwa biashara ni ndogo.
OFFA
INAYOKARIBIA MWISHO WAKE 2024 NI HII HAPA CHINI;
1.
KITABU: Michanganuo ya Biashara na
Ujasiriamali
2.
KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri
wasiyopenda kuitoa
3.
KITABU: Toleo jipya la Elimu ya pesa na Mafanikio
4.
KITABU: Sayansi & Sanaa ya Upishi wa
chapatti laini.
5.
MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji unga
wa Dona (USADO Milling)
6.
MCHANGANUO: Ufugaji kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-Kiswahili &kiingereza
7.
MCHANGANUO: Ufugaji kuku chotara
Kuroiler-nyama
8.
MCHANGANUO: Kilimo cha tikiti maji (Kibada watermelon)
9.
MCHANGANUO: Uboreshaji Mashamba ya zabibu
Dodoma (Makupila Real Estate)
10. MCHANGANUO:
Biashara ya kuuza chipsi
11. MCHANGANUO:
Biashara ya mgahawa (Jane Restaurant) –Kiswahili & Kiingereza
JINSI YA KULIPIA
Namba za malipo ni; 0712202244 au 0765553030 jina ni
Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe wa sms au watsap usemao “NATAKA OFFA YA MWISHO KWA 2024” Mara
moja nitakutumia zawadi zako zote 11 pamoja na kukuunganisha na
MASTERMIND-GROUP LA MICHANGANUO la mwaka 2025
AU
Unaweza kuingia kwenye Duka letu hili la
vitabu mtandaoni, Selar.co, na kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 pasipo
kuwasiliana na sisi ukitumia mtandao wowote unaotumia halafu utapewa kifurushi
cha ZIP utakachodownload zawadi. Unzip kifurushi na kutoa zawadi zako
zote 11. Kisha nitakuunga kwenye MASTERMIND GROUP muda huohuo
NB:
Unaweza kunikumbusha kwa meseji nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo.
0 Response to "TUMIA SIRI HIZI 4 ZA USHINDI WA TRUMP BIASHARA YAKO IFANIKIWE 2025"
Post a Comment