HOTUBA YA KWANZA KABISA YA RAIS DONALD J. TRUMP BAADA YA KUAPISHWA KUINGIA IKULU WHITE HOUSE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HOTUBA YA KWANZA KABISA YA RAIS DONALD J. TRUMP BAADA YA KUAPISHWA KUINGIA IKULU WHITE HOUSE

Rais wa 45 wa Marekani Donald Trump akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa leo
Vifuatavyo ni baadhi tu ya vipande(siyo hotuba kamili) vya hotuba ya Raisi wa 45 wa Marekani Donald J. Trump punde tu baada ya kuapishwa kuingia ikulu ya white house ya Marekani.


"Hatukabidhi madaraka kutoka utawala mmoja kwenda mwingine au chama kimoja kwenda chama kingine bali bali tunahamisha madaraka kutoka Washington DC kwenda kwenu watu……..

Hii ni siku yenu

Hizi ni sherehe zenu…………

Kilichokuwa muhimu siyo chama gani kinachotawala serikali yetu bali ni ikiwa serikali inatawaliwa na watu

Wanaume na wanawake wa Taifa letu waliosahaulika, hawatasahaulika tena, kila mtu anawasikiliza sasa.

Kwa miongo mingi tumekuwa tukivitajirisha viwanda vya nje kwa gharama za viwanda vya Marekani, kutoa ruzuku kwa majeshi ya nchi nyingine wakati tukiruusu mdororo wa kuhuzunisha wa jeshi letu

Tumekuwa tukilinda mipaka ya mataifa mengine wakati tukikataa kulinda ya kwetu wenyewe. Na tumepoteza matrilioni kwa matrilioni ya dolla nje wakati miundombinu ya Marekani ikiishia kuoza na kukatisha tamaa
Tumezifanya nchi zingine kuwa matajiri wakati utajiri, nguvu na kujiamini kwa nchi yetu kukipotelea kwenye upeo wa macho.
Viwanda kimoja baada ya kingine vimefungwa na kuacha fukwe zetu zikiwa hazina hata wazo moja kuhusiana na mamilioni kwa mamilioni ya Wafanyakazi wa Marekani walioachwa nyuma.
Utajiri wa watu wetu wa tabaka la kati umeporwa kutoka majumbani mwao na kisha kugawanywa tena kote duniani. Lakini hiyo ilikuwa ni zamani na sasa tunatazama mbele tu…………………

Marekani itaanza kushinda tena, kushinda kuliko ilivyoshinda awali
Tutazirudisha ajira zetu.
Tutairudisha mipaka yetu

Tutaurudisha utajiri wetu, na tutazirudisha ndoto zetu…………………..

Hatutafuti kulazimisha njia yetu ya maisha kwa mtu yeyote, lakini badala yake kuiacha ing’are kama mfano
Tutang’ara kwa kila mmoja kuiga mfano.

Mwisho, ni lazima tufikiri mambo makubwa na hata kuota mambo makubwa zaidi. Katika Marekani tunatambua kwamba  Taifa linaishi tu ikiwa kama litafanya jitihada. Hatutaendelea tena kuwakubali wanasiasa ambao wote huongea pasipo vitendo, wakilalamika mfululizo lakini bila ya kufanya chochote.

Muda wa mazungumzo matupu umemalizika. Sasa saa ya vitendo imewadia

Usimruhusu mtu yeyote kukuambia kwamba haiwezekani kufanyika. Hamna changamoto inayoweza ikafanana na moyo na mapambano na roho ya Marekani. Hatutashindwa. Nchi yetu itanawiri na kuwa tajiri tena.
Kwa pamoja tutaifanya Marekani kuwa na nguvu tena, tutaifanya Marekani kuwa tajiri tena, tutaifanya Marekani kujivunia tena, tutaifanya Marekani kuwa salama tena
Na, ndiyo, pamoja tutaifanya Marekani kuwa yenye nguvu tena

Asanteni
Mungu awabariki
Na Mungu Ibariki Marekani”




0 Response to "HOTUBA YA KWANZA KABISA YA RAIS DONALD J. TRUMP BAADA YA KUAPISHWA KUINGIA IKULU WHITE HOUSE"

Post a Comment