MIFANO (6) YA KUSHANGAZA YA WATU WALIOKUWA NA MSIMAMO THABITI DUNIANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MIFANO (6) YA KUSHANGAZA YA WATU WALIOKUWA NA MSIMAMO THABITI DUNIANI

Mfalme aliyevua taji la ufalme kisa mapenzi (Edward wa III)

Kuwa na MSIMAMO kumebadilisha mambo mengi sana Duniani na kamwe hakuna mafanikio kwenye nyanja yeyote ile kimaisha yanayoweza kupatikana pasipokuwepo na msimamo. Msimamo uliweza hata kubadilisha uelekeo wa urithi wa ufalme wa Uingereza kama tutakavyoenda kuona hivi punde kwenye moja ya mifano yetu 6 

Malkia Elizabeth wa II aliyefariki Dunia hivi karibuni haikutarajiwa na wala hakuwa katika mlolongo wa kurithi kiti hicho cha enzi kama siyo msimamo wa Kimapenzi wa mwanamke mmoja wa Kimarekani dhidi ya Edward wa VIII aliyekuwa Mfalme wa nchi hiyo na babamkubwa wa Elizabeth II. Inasemekana ukiwa na msimamo kwa kitu chochote kile unachokitaka maishani hatimaye kitu hicho ni lazima utakipata tu na haijalishi itakuchukua muda gani.

Mifano ya watu sita (6) ninaoenda kuwaelezea katika makala yangu hii moja kwa moja nitatumia mifano kutoka katika kitabu Mashuhuri cha FIKIRI & UTAJIRIKE  (Think & Grow Rich-Swahili Edition) kama kilivyotafsiriwa na Peter Augustino Tarimo mwaka 2021. Sitaelezea kwa kina sana kwani unaweza kupitia kitabu hicho mwenyewe iwe ni nakala ya kiingereza au kiswahili kwani maudhui ni yaleyale.

Kwanini nikazungumzia sura hii ya 9 ya MSIMAMO?

Kitabu hiki kimebeba falsafa ya MAFANIKIO yenye vitu 13 vinavyounda sura 13 ikiwemo hii ya MSIMAMO yenyewe. Sura zingine 2 za kitabu zipo nje ya falsafa yenyewe. Nasisitiza MSIMAMO kwani ndiyo sifa hata mwandishi mwenyewe wa kitabu anayosema pasipo hiyo hata sifa/vigezo vingine 12 mtu hataweza kuvitimiza kusudi apate mafanikio ama kile anachokihitaji maishani iwe ni Utajiri, Afya, Mapenzi, Mamlaka au Chochote kingine. Ukiniambia una muda mchache sana wa kusoma lakini ungependa kunufaika na falsafa za kitabu hiki basi ningekushauri usome japo Sura hii moja tu ya 9 na utakuwa umepata kila kitu sawa na mtu aliyesoma kitabu kizima.

Bila kupoteza muda hebu tuanze mara moja kuwataja;

1.  HENRY FORD, CARNEGIE, ROCKFELLER na EDSON: Hawa ni watu wanne tofauti na nimewataja kwa pamoja makusudi kwani habari zao zimetapakaa karibu katika kila sura ya kitabu hiki na kwenye suala la msimamo hasa kwa Henry Ford kwenye sura hii ya 9 mwandishi ameanza naye pale mwanzoni kabisa kwa kueleza kuwa Ford alikuwa na msimamo usioyumbishwa kirahisi hasa wakati alipotaka kutimiza malengo yake. Katika hii sura miamba hii 4 imetajwa mara nyingi kwa misimamo yao iliyowaletea mafanikio ya kustaajabisha. 

2.  FANNIE HURST: Kisa cha mwandishi wa Vitabu Fannie Hurst ukurasa wa 252 wa tafsiri ya kitabu cha Think & Grow Rich kwa kiswahili ikiwa wewe ni mwandishi uliyehangaika muda mrefu na kazi zako bila mafanikio ya kuchapishwa kinaweza kuwa mfano mzuri sana kwako. Bi Hurst kwa miaka 4 alisaga soli za viatu vyake akiingia kila ofisi ya mchapishaji bila matumaini. Alikataliwa mara 36 kabla ya kuja kukubaliwa na kampuni moja ya uchapishaji ya The Saturday Evening Post na baada ya hapo wachapishaji wengine walimiminika kwake kama mvua na pesa zikawa si shid tena kwake. Kisa hiki nakifananisha na kile cha wasanii wa hapa kwetu kama kina Diamond, Mr. Nice, Ali Kiba na Ferooz , wote walivuma sana na kupata umaarufu lakini ni wachache kati ya hao walioweza kuwa na msimamo wa kuendelea kufanya muziki mzuri wakadumu mpaka leo hii. 

3.  KATE SMITH: Kisa cha mwimbaji muziki aliyeimba miaka mingi bila ya kupata senti 5 lakini alishikilia msimamo wake uleule mpaka mwisho akajikuta anapata pesa kwa wiki zinazolingana na mshahara wa mwaka mzima wa mtu wa kawaida. Kisa hiki kizima utakutana nacho ukurasa wa 245

4.  MFALME EDWARD VIII na Bibi WALLIS SIMPSON: Ni kisa cha mapenzi kilichosisimua zaidi Ulimwengu katika karne ya 20. Kinapatikana kuanzia ukurasa wa 254. Kisa mpaka mfalme wa Uingereza akaamua kuachia taji la ufalme ni msimamo wa mapenzi kati yake na mwanamke wa Kimarekani tena mwenye umri mkubwa na mtalaka wa ndoa 2. Kimaadili haikupaswa mfalme aoe mwanamke toka taifa jingine tena aliyekwishatalikiwa. Kidini pia kanisa la Kianglikana isingewezekana.

Walishauriwa waachane lakini katu misimamo yao haikupingika mwishowe ikabidi mdogo wake na mfalme ambaye ndiye baba mzazi wa Malkia Elizabeth II ndio ashikilie taji kwani EDWARD VIII aliachia ngazi na hakuwa na mtoto wa kumrithi. Ni kisa cha kusisimua mno! Edward na Simpson walikuja kuishi hadi kifo kilipokuja kuwatenganisha ingawa wala hawakuwahi kupata watoto.

Katika wakati tulionao sasa hivi kuna mfano mzuri wa mtu mwenye msimamo usioyumba (Rais Vladmir Putin wa Urusi) ijapokuwa si msimamo mzuri kwani anasababisha mauaji ya binadamu. Msimamo kama huu ikiwa unaushikilia kwa jambo chanya ni mzuri.

5.  MTUME MKUBWA WA MWISHO MUHAMMAD: Kama ulikuwa unafikiri kitabu hiki ni cha wasiomwamini Mungu basi soma sura hii vizuri na sura nyingine zilizowataja mitume wakubwa kama Yesu Kristo, Muhamad na wengineo katika dini zao. Kipekee kabisa katika Sura hii ya MSIMAMO mwandishi ametumia wasifu wa Mtume Muhammad kama ulivyochambuliwa na Essad Bey. Uchambuzi huu mfupi wa hicho kitabu uliandikwa na Thomas Sugrue katika Jarida la Herald Tribune. Ukisoma Simulizi hii ya kusisimua ya Mtume Muhammad utatambua vizuri nguvu ya MSIMAMO inayojulikana katika ustaarabu. Waarabu ni vigumu sana kuamini miujiza lakini katika wasifu huu tunaambiwa miongoni mwa vitu Mtume alivyovifanya kwao nyakati hizo ilikuwa ni Muujiza mkubwa.

Nimegusia kwa kifupi sana mifano hii katika hii sura ya 9 inayohusu MSIMAMO. Kwa kweli kuna mengi makubwa ya kujifunza na kama nilivyotangulia kusema hata kama huna muda wa kusoma kitabu chote basi nikusihi usome hata sura hii ya 9 tu peke yake inatosha.

Kitabu cha Think and Grow Rich kinapatikana kwa urahisi sana mtandaoni, unaweza kusoma nakala ya kiingereza lakini pia kuna nakala ya Kiswahili ambayo hupatikana kwa malipo kwa aliye na simu janja katika mtandao wa kuuza vitabu vya nakala tete(softcopy) uitwao GETVALUE kupitia kiungo kifutatacho, FIKIRI & UTAJIRIKE

Ili kupata kitabu ni lazima ujisaji kwenye huo mtandao kwa kutumia baruapepe(email) na nenosiri(password). Baada ya hapo DOWNLOAD application yao kwa kutumia simujanja yako kisha ujaze tena ‘baruapepe’ na ‘nenosiri’ ulivyotumia wakati unajisajili. App ikishafunguka basi unaweza ukasoma kitabu chako kwenye simu bila wasiwasi.

ZAWADI KWA WATU 10 TU SIKU 3 !

Watu 10 wa mwanzo watakaonunua kitabu hiki kwa simu zao za Smartphone kuanzia leo hii baada ya kusoma huu ujumbe watapata pia fursa ya kutumiwa kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI au MAFANIKIO YA BIASHARA YADUKA LA REJAREJA (unachagua kimoja kati ya hivyo 2) pamoja na kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku (MKOMBOZI CHICKS PLAN) chenye michanganuo ya kuku wa kienyeji, kuku wa nyama na kuku wa mayai.

Ikiwa umesoma ujumbe huu na unahitaji basi bonyeza linki hii hapa; THINK & GROW RICH SWAHILI EDITION 2021 kisha fuata maelekezo ya kununua, ukishanunua kitabu chako nitumie meseji kama unataka kitabu kipi kati ya vile 2 kisha nitacheki kuhakikisha kama kweli umeshanunua na nitakutumia kitabu na kifurushi chako cha michanganuo ya kuku muda huohuo. Kumbuka kitabu cha FIKIRI NA UTAJIRIKE katika mtandao wa GETVALUE kinauzwa sh. Elfu 10 tu na unalipia kwa kutumia mitandao ya simu.


SOMA PIA MAKALA HIZI;




2 Responses to "MIFANO (6) YA KUSHANGAZA YA WATU WALIOKUWA NA MSIMAMO THABITI DUNIANI"

  1. thanks naimani ntajifunza mengi zaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bill shaka Anonymous utajifunza mengi endelea TU kutufuatilia

      Delete