BEI NA GHARAMA ZA MAISHA ZINAZIDI KUPANDA JUU, TUFANYE NINI SASA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BEI NA GHARAMA ZA MAISHA ZINAZIDI KUPANDA JUU, TUFANYE NINI SASA?

Marais Vladmir Putin na hasimu wake mkubwa Volodymyr Zelensky   wa Ukraine
Habari za majukumu ya kila siku mpenzi mfuatiliaji wa mtandao huu wa Jifunzeujasiriamali. Natumaini upo vizuri licha ya gharama za maisha kuzidi kupaa juu. Leo hii napenda kukushirikisha mambo muhimi 3 kubwa likiwa ni hili la kuzidi kupaa juu gharama za maisha –je, tufanye kitu gani?

Mengine mawili ni semina ya kuandika michanganuo kama hukubahatika kuipata na la tatu ni offa zetu za mara kwa mara lakini hii ikiwa ni ya kipekee zaidi kama utakavyosoma mwishoni mwa makala hii.

Nikukaribishe tuwe sote mpaka mwisho.

Hata kabla ya ‘janga hili la kiuchumi kuanza, bado wengi wetu tulikuwa na sababu lukuki ni kwanini hatuna mafanikio, utajiri, furaha na upendo kama ambavyo tungelipenda tuwe navyo. Kila mtu angelitoa sababu tofauti kwa hilo, wengine wakisema, “ni shauri ya uchumi mbovu”, “kazi yangu siyo nzuri hailipi”, wengine wangelalamikia mazingira ya biashara na kudai siyo rafiki kwao yanawarudisha nyuma nk.

Kuna idadi kubwa sana ya watu ambao wangewalaumu watu waliowazunguka kama vile ndugu, wenza, watoto, familia na hata marafiki wakidai wao ndio chanzo cha kuporomoka au kudorora kwao kimafanikio. Na sasa hivi tunaambiwa kuwa sababu ya hali ya kiuchumi kuzidi kuwa mbaya duniani na vitu kupanda mno bei kunatokana na vita huko Ukraine pamoja na Covid 19. Unaweza kushangaa kwani ngano na mchele si tunalima wenyewe hapahapa jamani?

Lakini mimi leo ningependa unione wa ajabu kidogo kwa kukuambia kwamba; sababu zoote hizo ikiwemo na vita ya Ukrain na Corona, wala hazina lolote lile la kufanya juu ya mafanikio yako katika nyanja zote ikiwemo kiuchumi na tena nikuambie hakuna sababu yeyote kutokea nje yako wewe inayoweza kukurudisha nyuma kimafanikio.

Tatizo kubwa lipo ndani yetu sisi wenyewe. Na kama huamini hebu chunguza kipindi chote cha mdororo wa kiuchumi, je hawataibuka watu na mafanikio katika nyanja mbalimbali? Je, ni kila mtu atakuwa akikosa hela ya kula, kununulia mafuta na unga?

Falsafa hii ya Mafanikio nimejifunza kutoka kitabu mashuhuri cha Think & Grow Rich, (Fikiri na Utajirike) nakusihi sana kitafute ukisome kama hujakisoma, na si kama napigia debe nakala ya kiswahili niliyotafsiri ili niuze, la hasha, kinapatikana pia bure kwa kiingereza huko mitandaoni na unaweza kukitafuta audio au hata softcopy bila gharama kubwa.

Falsafa hii inatuambia kwamba mtuhumiwa nambari moja wa matatizo yetu mengi ni UBONGO wetu wenyewe. ‘The way’ tunavyoyatazama matatizo ndiyo tatizo lenyewe. Ubongo wa mtu una nguvu kubwa ya kumletea mafanikio lakini pia Ubongo huohuo unaweza kumsababishia mtu maanguko makubwa kiuchumi, kiafya na hata kijamii.

SASA TUFANYEJE?

Dunia ya mtu ya nje ni sawa na kivuli tu cha Dunia yake ya ndani. Badala ya kuona vitu vikipanda bei na kusikitika tusijue la kufanya, tukae tubuni njia za kuongeza vipato vyetu zaidi hasa kwa njia ya kufanya Biashara. Ikiwa vitu vimepanda bei basi hata bidhaa na huduma unazouza lazima pia upandishe bei, hivyo mimi hapo sioni kama kuna tatizo. Ikiwa kama huko nje wanatuletea mafuta kwa bei kubwa wakisingizia vita ya Urusi na Ukraine, basi na sisi tuwauzie korosho, kahawa na katani yetu kwa bei ileile ya juu.

Kwanini tusiwe kama Vladmir Putin? Mataifa ya Magharibi wamemwekea vikwazo vikali yeye akawajibu kwa kuwaambia, sasa tuone gesi, petroli na ngano mtatoa wapi msipokula jeuri yenu”, matokeo yake ndiyo mpaka huku na sisi tunalalamika kupanda bei kwa vitu kulikopindukia, Ulaya yote na Marekani kilio ni hichohicho.

Badala ya kulialia vitu kupanda bei, dawa ni kukomaa tu na biashara mpaka kieleweke, kama wewe ni mfanyabiashara fanya biashara kisasa, ikiwa wewe ni mkulima lima kibiashara, mfugaji fuga kibiashara na ikiwa ni mfanyakazi basi  timiza wajibu wako kwa ufanisi ili kutoa matokeo yanayotegemewa.

Juu ya yote njoo tujifunze biashara na jasiriamali pamoja ndani ya Mastermind group la Michanganuo-online. Nakuhakikishia katika michanganuo 22 ya biashara, 10 ya kwenye kitabu na 12 isiyokuwa kwenye kitabu nitakayokutumia punde baada ya kulipia  ada ya kujiunga sh. Elfu 10, ukiisoma hakuna biashara itaayokubabaisha kwani mchanganuo unagusa kila hatua biashara inayopita kuanzia mtaji mpaka mauzo.

Tunayo pia semina ya jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara yeyote ile inayoendelea kwenye group mwaka mzima. OFFA ya vitabu na michanganuo,  jumla yake ni vitu 20 kama inavyoonekana hapo chini mwisho. Offa hii ni kwa watu 30 tu watakaowahi kujiunga kabla ya siku ya tarehe 30/5/2022 hivyo wahi mapema ikiwa utaguswa na offa hii, sipendi uje kunilaumu, sijui ..ooo…sikupata ujumbe au sababu nyingine yeyote.

Gharamahalisi ya kila kitu pamoja na kuwa ndani ya group la masomo kwa mwaka mzima ni zaidi ya shilingi 100,000/=(laki moja) lakini hapa unalipia shilini elfu 10 tu! Hii ni fursa ya kipekee kabisa kuwahi kutolewa na mtandao wa jifunzeujasiriamali.co.tz

Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wa “NATAKA SEMINA NA OFFA YA VITU 20”

Nitakutumia offa zote muda huohuo pamoja na kukuunganisha na Group na Channel yetu ya masomo na semina.

Kumbuka pia baada ya kujifunza Semina nzima nitatoa kwa kila aliyeshiriki zawadi ya vitabu vipya 2 vya semina hiyo, cha semina ya masomo 11 ya msingi na kingine cha Hesabu za mchanganuo wa biashara kwa undani (Advanced Business Plan Financials). Ukivipata hakuna mchanganuo wa biashara utakaokushinda kuandika. Vyote viwili vipo tayari vikikusubiri umalize semina.

Vilevile kama ulikuwa hujui ni kwamba OFFA ya safari hii nimelenga mtu yeyote anayetaka kufahamu michanganuo ya biashara kwa kina kabisa na hata yule anayependa kuwa Mtaalamu(expert) wa kuandaa Michanganuo ya biashara kama mimi nifanyavyo kwa ajili ya Makampuni na biashara za watu binafsi.    

Ifuatayo ni orodha ya  ya vitabu na michanganuo utakayotumiwa punde baada ya kulipia semina;

                      1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                      2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

                      3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                      4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                      5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

                      6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

                      7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

                      8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

                      9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

                    10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

                    11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

                    12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

                    13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                    14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

                    15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

                    16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                    17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                    18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

                    19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

                    20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

                    21.    Kunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima.

Kumbuka mwisho wa offa hii ni tarehe 30 na watu wakitimia 30 itakwisha hata kabla ya siku hiyo kufika. Tafadhali mjulishe na yeyote unayemjali juu ya habari hizi njema.

Ni mimi,

Peter .A.Tarimo

Mfasiri wa Kitabu cha Think & Grow Rich kwa kiswahili, Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara na pia Mwandishi wa vitabu na makala za Biashara na Ujasiriamali.

0 Response to "BEI NA GHARAMA ZA MAISHA ZINAZIDI KUPANDA JUU, TUFANYE NINI SASA?"

Post a Comment