NINI MAANA YA MCHANGANUO WA BIASHARA? - SOMO LA KWANZA-2022 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NINI MAANA YA MCHANGANUO WA BIASHARA? - SOMO LA KWANZA-2022

Somo la kwanza semina ya michanganuo-2022
Hapa nitakwenda kuweka kwa kifupi kabisa yale tuliyojifunza katika Semina yetu ya jinsi ya kuandika Mchanganuo wa Biashara 2022, kupata Mfululizo mzima wa kozi hii, vitabu, michanganuo kamili , templates na mengineyo mengi  ni vizuri mtu ukajiunga na group la Michanganuo-online ;

 

Somo letu la kwanza kabisa lilikuwa na vitu hivi 5;-

                                                                        

1)  Maana ya Mchanganuo / Mpango wa biashara

2)  Majina mbalimbali ya mpango wa biashara

3)  Ni kina nani wanaohitaji mpango wa biashara

4)  Aina za michanganuo ya biashara na tofauti zake.

5)  Matumizi ya mpango wa biashara  


1. MAANA YA MPANGO WA BIASHARA

Kwanza kabla hatujajua maana yake niseme kwamba ukiona nimetumia neno Mchanganuo wa biashara  ni sawasawa na neno Mpango wa Biashara, hivyo usije ukadhani ni vitu viwili tofauti hapana.

 

Mchanganuo wa biashara kwa kimombo (Business plan) ni maandishi yanayoelezea kila jambo kuhusu biashara unayoiendesha, mambo hayo ni, malengo, mikakati, bidhaa/hudumu utakayouza, soko (wateja), shughuli mbalimbali za masoko na uongozi, gharama, mahitaji, na masuala yote yanayohusiana na fedha.

 

Hata hivyo hakuna maana moja tu ya mpango wa biashara, maana zinaweza kutofautiana kulingana na aina ya mpango wenyewe kwani pia kama tutakavyoona huko mbele kuna aina nyingi za mipango ya biashara. Hivyo hapa chini nitaweka maana nyingine za mpango wa biashara ukiacha ile ya kwanza hapo juu.

 

Mchanganuo wa biashara ni dira au ramani ya biashara yako kuonyesha unakotoka na unakokwenda. Basi.

AU
Mpango wa biashara ni jumla ya maelezo yote yanayoihusu biashara, kuanzia malengo ya biashara mpaka mbinu mbalimbali zitakazotumika kufanikisha biashara husika. Ni dira au ramani inayokuongoza katikabiashara yako kujua unatoka wapi na unaelekea wapi.

AU
Mpango wa biashara ni andiko linaloelezea fursa ya kibiashara kwa wawekezaji na taasisi za kifedha.

AU
Mpango wa biashara ni mpango kazi unaoonyesha kila shughuli itakayofanyika katika biashara yako.

2. MAJINA MBALIMBALI YA MPANGO WA BIASHARA

Unaweza kusikia sehemu mbalimbali yakitajwa maneno tofauti yanayomaanisha kitu kilekile kimoja na mpango wa biashara ni hivyohivyo. Baadhi ya maneno yanayomaanisha au kuhusiana kwa karibu na mpango wa biashara ni haya yafutayo;

·       Mpango wa biashara lenyewe

·       Mchanganuo wa biashara.

·       Andiko la biashara.

·       Upembuzi wa biashara

·       Mpango kazi

·       Andiko la mradi.nk.


3. NI KINA NANI WANAOHITAJI MPANGO WA BIASHARA?

·       Wale wanaotaka kuanzisha biashara mpya

·       Wenye biashara zilizokwisha anzishwa siku nyingi

·       Wawekezaji, mameneja wa mabenki na wabia

·       Wafanyakazi katika taasisi mbalimbali

·       Wanafunzi katika taasisi za elimu na vyuo


4. AINA ZA MICHANGANUO YA BIASHARA NA TOFAUTI ZAKE.

Michanganuo ya biashara ipo ya aina nyingi kulingana na ni malengo gani umekusudia kuutumia;

                              i)      Kwa ajili ya matumizi ya ndani

                              ii)     Kwa ajili ya matumizi ya nje

                             iii)     Kwa ajili ya biashara mpya,

                             iv)    Kwa ajili ya kuendeleza biashara iiliyokuwepo,

                             v)     Kwa ajili ya bidhaa mpya katika soko,

                             vi)    Kwa ajili ya kutafuta masoko nk.

Yote hiyo ni aina ya michanganuo ya bioashara na vipengele vyake huwa ni vile vile ila tofauti yake tu ni kwamba kila aina huzingatia vipengele fulani zaidi kuliko vingine, kwa mfano inategemewa kuwa mchanganuo kwa ajili ya biashara mpya utakuwa na vipengele vichache tu wakati kwa biashara ya zamani vipengele huwa vingi zaidi, kwa ajili ya matumizi ya ndani kwa mfano kuna vipengele kabisa havina umuhimu wa kuviweka mfano, kipengele cha historia ya kampuni na Bidhaa kutokana na sababu kuwa tayari wdau wa ndabi ya kampuni wanavifahamu vizuri.


 5. MATUMIZI YA MPANGO WA BIASHARA

                     a)     Kuanzisha na kuendeleza biashara mpya;ni dira itakayokuongoza katika safari ya kufanikisha biashara yako.

                     b)     Kuweka na kufafanua malengo pamoja na mikakati uliyojiwekea.

                     c)     Kuombea mikopo kutoka taasisi za fedha.

                     d)     Kupima utekelezaji wa malengo mara kwa mara pamoja na kufanya marekebisho pale ulipokosea.

                     e)     Kuainisha mikataba baina ya wabia.

                      f)      Kutathmini bidhaa mpya, kuzitangaza au kupanua bidhaa za zamani.

                     g)     Kuweka viwango  katika biashara/kampuni kwa ajili ya kuiuza au kwa ajili ya maswala mengine ya kisheria.

                     h)     Ni kipimo cha uwezo wako kibiashara.

 

Mawasiliano yetu ni; 0765553030 AU 0712202244

Kujiunga na semina mara moja pamoja na kutumiwa vitu 20 vya offa muda huohuo huku ukiendelea kujifunza mwaka mzima, lipia ada yako sh. 10,000/= kisha tuma ujumbe usemao, “NATAKA SEMINA-2022 NA OFFA YA VITU 20”



OFFA YA VITABU NA MICHANGANUO JUMLA ITEMS 20, INAYOISHA TAREHE 30/05/2022

                      1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                      2.      KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara (One Page Business Plan) -cha kiswahili

 

                      3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                      4.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                      5.      KITABU cha mwandishi Tim Berry cha JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA, ni mwandishi nguli wa Michanganuo Duniani -cha kiingereza

 

                      6.      Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza mvinyo/wine na Juisi ya Rosella -kiswahili

 

                      7.      Mchanganuo wa Kikundi cha Kinamama: Biashara ya kiwanda cha kukoboa mpunga -kiswahili

 

                      8.      Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kiswahili

 

                      9.      Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiswahili

 

                    10.    Mchanganuo Biashara ya ufugajiwa wa kuku wa nyama- kwa kiingereza

 

                    11.    Mchanganuo Biashahara ya Ufugaji wa kuku wa mayai - kwa kiswahili

 

                    12.    Mchanganuo Biashara ya ufugaji wa kuku wa kienyeji – kwa kiswahili

 

                    13.    Mchanganuo kamili wa kilimo cha matikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                    14.    Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa kiswahili

 

                    15.    Mchanganuo wa Biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) –kwa kiingereza

 

                    16.    Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                    17.    Mchanganuo wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                    18.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara (template) kinachokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika Mchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika -Kwa Kiswahili

 

                    19.    Kielezo cha mchanganuo wa biashara(template) –kwa kiingereza

 

                    20.    Somo maalumu kabisa la Mzunguko wa fedha kwenye biashara yako -kiswahili

 

                    21.    Kunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima

 

0 Response to "NINI MAANA YA MCHANGANUO WA BIASHARA? - SOMO LA KWANZA-2022"

Post a Comment