RATIBA YA SEMINA: JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO / MPANGO WA BIASHARA 2022 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

RATIBA YA SEMINA: JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO / MPANGO WA BIASHARA 2022

JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA

KUHUSU SEMINA YA MWAKA HUU 2022

Semina ya kuandika mpango wa biashara au mchanganuo wa biashara, ni masomo ya kina 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara  yatakayotolewa kwenye group hili la MICHANGANUO-ONLINE kila siku kwa washiriki watakaopenda kufuatilia masomo hayo sambamba na programu zetu nyingine kwenye group. 

Kwa wanafunzi wapya watakaokuwa wakijiunga wanaweza kufuatilia semina katika channeli yetu ya telegramu au kutumiwa semina nzima katika email huku wakiendelea kusoma somo la kila siku toka kwa mkufunzi. Mwanagroup ambaye tayari amekwishaelewa masomo haya ana hiyari ya kutohudhuria somo la siku akaendelea kuhudhuria tu programu nyingine.

Washiriki wapo huru kuuliza swali lolote lile pale wanapokuwa hawajaelewa na mwisho wa semina kila mshiriki atakuwa ameandaa mpango wa biashara yake atakayochagua yeye mwenyewe huku akipewa usaidizi wa karibu na mkufunzi wa semina.

 

Tofauti na semina za miaka mingine hii hakuna mshiriki atakayeachwa nyuma kwa namna yeyote ile kutokana na vile wakufunzi walivyoamua kujitolea muda wao kuhakikisha lengo la washiriki linatimia. Maswali yanakaribishwa muda wowote hata ikiwa kama siyo muda maalumu wa masomo.

Ada ya kujiunga na semina ni sh. elfu 10 na inafanyika ndani ya Mastermind Group la Michanganuo-online kupitia watsap, Telegram na email. Watu 30 wa kwanza watajipatia Offa ya vitabu na michanganuo kamili ya biashara mbalimbali jumla vitu 20, pia kuungwa group la masomo ya kila siku kwa mwaka mzima. 

Mwisho wa OFFA ya vitu 20 ni tarehe 30/5/2022


IFUATAYO NI RATIBA YA MASOMO

 

SOMO LA KWANZA

Maana ya Mchanganuo/Mpango wa biashara

·       Majina mbalimbali ya mpango wa biashara

·       Ni kina nani wanaohitaji mpango wa biashara

·       Aina za michanganuo ya biashara na tofauti zake.    

·       Aina za Michanganuo ya Biashara

·       Matumizi ya mpango wa biashara      

 

SOMO LA PILI

Jinsi ya kuanza kuandika mpango/mchanganuo wa biashara

·       Unaanzaje kuandika mapango wa biashara?

·       Mawazo utayatoa wapi?

·       Utafiti wa soko/biashara au feasibility study

·       Vipengele/sehemu za mpango wa biashara

·       Ni kipengele kipi huanza na ni kipi humalizia.

 

SOMO LA TATU

Kasha la nje, kichwa cha mchanganuo na Yaliyomo

Utajifunza ni vitu gani hukaa nje kwenye jalada na namna ya kuvipanga

Pia utaona ni nini huwekwa kwenye yaliyomo

 

SOMO LA NNE

Muhtasari.

·       Ni vitu gani muhimu vinavyounda Muhtasari?

·       Mifano ya  muhtasari ya biashara mbalimbali

·       Aina za muhtasari

·       Muda muafaka wa kuandika Muhtasari

·       Mbinu za kuandika Muhtasari utakaomfanya msomaji yeyote asiweze kukwepa kusoma mpango wako mzima.

 

SOMO LA TANO

Maelezo kuhusu biashara au Kampuni

·       Umiliki wa biashara: kampuni, ubia au mtu binafsi

·       Historia ya kampuni.

·       Usajili wa biashara

·       Jina na eneo biashara ilipo

·       Dhamira kuu

·       Maono

·       Malengo ya biashara

·       Siri za mafanikio.

 

SOMO LA SITA

Maelezo kuhusu Bidhaa

·       Bidhaa au huduma utakazouza

·       Kwanini wateja wanunue kutoka kwako?

·       Faida atakayipata mteja kutokana na bidhaa au huduma zako

·       Namna utakavyopata malighafi au bidhaa na jinsi utakavyokidhi mahitaji ya wateja

·       Teknolojia itakayotumika

·       Mabadiliko ya bidhaa au huduma katika soko kwa siku za baadae.

 

SOMO LA SABA

Mpango/Tathmini ya soko.

·       Wateja wako ni kina nani?

·       Mahitaji ya wateja na tabia zao

·       Kwanini wanunue kutoka kwako na siyo kwa washindani wako?

·       Mwelekeo wa soko na jinsi wateja walivyosambaa

·       Ukubwa wa soko unalomiliki

·       Ukuaji wa soko

·       Tathmini ya sekta uliyopo

·       Washindani wako wakubwa

·       Tathmini ya Nguvu, Udhaifu, Fursa  na Vikwazo

 

SOMO LA NANE

Mikakati na utekelezaji.

·       Mkakati wa masoko

·       Bidhaa/Huduma,

·       Bei,

·       Matangazo,

·       Eneo na Usambazaji

·       Huduma kwa wateja

·       Programu ya masoko

 

·       Mkakati wa mauzo

·       Makisio ya mauzo

·       Programu za mauzo

 

·       Utekelezaji/Uendeshaji

·       Kazi za kila siku

·       Mpango wa utekelezaji vitendo na muda maalumu wa utekelezaji

 

SOMO LA TISA

Uongozi na Wafanyakazi

·       Mchoro wa Utawala

·       Timu ya viongozi, wasifu wao na majukumu watakayohusika nayo

·       Idadi ya wafanyakazi na sifa zao

·       Pengo la wafanyakazi na mahitaji ya wafanyakazi ya siku za baadae.

·       Jedwali la mishahara.

 

 

SOMO LA KUMI

Makisio ya Taarifa za Fedha

·       Unaingiza vipi fedha?

·       Muhtasari wa mahitaji yote ya fedha, vyanzo na matumizi yake

·       Makisio ya gharama za awali(unazolipa mara moja)

·       Makisio ya mali(rasilimali) za kudumu

·       Makisio ya mauzo

·       Makisio ya gharama za mauzo

·       Gharama za kudumu za uendeshaji

·       Makisio ya kodi na riba ya mikopo

·       Makisio ya Faida na Hasara(Projected Profit & Loss)

·       Makisio ya fedha taslimu (Projected Cash Flow)

·       Makisio ya mali na madeni (Projected Balance Sheet)

·       Tathmini ya mauzo yatakayorudisha gharama zote (Break even analysisi)

·       Uwiano wa Sehemu muhimu za biashara (Business Ratio).

 

SOMO LA KUMI NA MOJA

Viambatanisho Muhimi

·       Majedwali na vielelezo

·       Leseni, vibali na stakabadhi za kodi na benki

·       Taarifa za mahesabu ya nyuma

·       Kopi za barua na mikataba mbalimbali.


0 Response to "RATIBA YA SEMINA: JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO / MPANGO WA BIASHARA 2022"

Post a Comment