SEMINA SIKU YA PILI: MIKAKATI, UTEKELEZAJI NA UONGOZI (JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SIKU YA PILI: MIKAKATI, UTEKELEZAJI NA UONGOZI (JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN)

Mhudumu katika mgahawa wa Jane Restaurant

Hii ni siku ya pili ya semina yetu ya kuandika hatua kwa hatua mchanganuo wa biashara ya Mgahawa wa Jane. Ili kupata mwendelezo mzuri hakikisha unacho kitabu chako cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamona na Michanganuo yote 3, ule wa Jane Fast Food na Jane Restaurant katika lugha ya kiswahili na Kiingereza


5.0 MIKAKATI NA UTEKELEZAJI.

Tukianza na Mikakati, mikakati ni malengo au vipaumbele mbalimbali wamiliki wa biashara hii walivyochagua kutekeleza kusudi biashara yao iweze kufanikiwa wakizingatia mahitaji ya wateja wao pamoja na upekee wa huduma na bidhaa watakazowapatia.


Mwanzoni kabisa kama Sura nyingine zinavyoanza panakuwa na Muhtasari wa sura nzima lakini ambao huandikwa baada ya vipengele vingine vyote vidogo kuandikwa.


Kisha chini vinafuata vipengele kimoja baada ya kingine ambavyo ni hivi hapa chini ingawa siyo lazima katika mgahawa wa Jane vipengele vyote vitumike;

5.1 Faida au Nguvu za kiushindani

5.2 Mkakati wa soko
5.3.1 Kaulimbiu ya kujipanga katika soko
5.3.2 Mkakati wa bei.
5.3.3 Mkakati wa matangazo
5.3.4 Mkakati wa usambazaji
5.3.5 Programu za masoko

5.4 Mkakati wa mauzo
5.4.1 Makisio ya mauzo
5.4.2 Programu za mauzo
5.5 Mkakati wa ushirikiano
5.7 Vitendo na Utekelezaji.

5.1 Faida za kiushindani

Uwezo mkubwa wa wapishi katika kuandaa vyakula vyenye mlo kamili

 

5.2 Mkakati wa soko

Hapa tunaweka muhtasari wa vipengele vidogo vilivyopo chini ya Mkakati wa soko ambavyo ni, Kaulimbiu ya kujipanga sokoni, mikakati ya bei, matangazo na usambazaji


5.2.1 Mkakati wa matangazo na promosheni.

Katika kipengele hiki kidogo chini ya makakati wa soko tunaorodhesha njia za matangazo tutakazotumia kwa mfano katika mgahawa wa Jane watatumia matangazo ya mdomo kwa mdomo kwa kuwapa zawadi wateja wale wa zamani kusudi waweze kuwahamasisha wateja wengine wapya kuja kula Jane Restaurant.


5.2.2 Mkakati wa bei.

Mkakati wa bei nacho ni kipengele kidogo chini ya Mkakati wa soko. Hapa unaelezea jinsi utakavyopanga bei zako kwa mfano Jane wamesema kuwa watatumia mbinu ya kuweka bei ya wastani kusudi waweze kujijengea msingi mzuri wa wateja.


5.3 Mkakati wa mauzo

Huu ni mkakati unaojitegemea mbali na ule wa soko. Kwenye Jane Restaurant wameeleza kuwa watazingatia huduma nzuri kwa mteja katika kukuza mauzo yao pamoja na mafunzo ya mara kwa mara kwa wahudumu mfano jinsi ya kutambua mitizamo ya wateja nk. Watazingatia pia kujibu malalamiko ya wateja kwa wakati. 

5.3.1 Makisio ya Mauzo.

Ni kipengele kidogo cha Mkakati wa mauzo na kinashughulika zaidi na kutabiri mauzo. Hapa unakisia mauzo yako yataongezeka kwa asilimia ngapi kwa mwaka baada ya kukisia mauzo ya kila mwezi kwa miezi yote 12 ya mwaka wa kwanza. Mfano Jane kulingana na sababu mbalimbali ilikisia mauzo kwa mwaka kuongezeka kwa asilimia 10%. Unaweza pia kwa kutumia jedwali (spreadsheet) ukakisia mauzo yako kwa miezi ya miaka yote 3 kisha ukakokotoa ongezeko hilo kwa kila mwaka ni asilimia ngapi.


Chini ya makisio yako unaweza kuweka chati za mauzo kwa mwaka na kwa miezi 12 ya mwanzo.


5.4 Mpango wa uendeshaji.

Katika Uendeshaji unaelezea jinsi kazi mbalimbali zitakavyotendeka kila siku, ratiba ya matukio pamoja na watu watakaosimamia vitendo hivyo. Unaweza kuelezea pia miundombinu mbalimbali na vifaa vitakayohusika, teknolojia, vyanzo vya malighafi au bidhaa, eneo la biashara na vipimo mbalimbali vitakavyotumika kujua kama biashara inakwenda katika njia sahihi.

6.0 UONGOZI NA WAFANYAKAZI

Kwenye Sura hii ya Uongozi na wafanyakazi, huwa kunakuwa na vipengele vidogo vifuatavyo;

 

6.1 Waanzilishi wa biashara

6.2 Mfumo wa utawala

6.3 Chati ya utawala

6.4 Pengo la utawala

6.5 Mpango wa malipo

 

Sura hii huanza kama ilivyokuwa sura nyingine kwa muhtasari ambao utatakiwa uandike yale mambo muhimu kama vile waanzilishi, biashara itaajiri watu wangapi akiwemo meneja/mameneja pamoja na upungufu wa wafanyakazi kama upo na huandikwa baada ya kumaliza kuandika sura nzima kwanza.

 

6.1 Uongozi.

Katika mchanganuo huu wa Jane, tumeanza kwa kuwataja viongozi waanzilishi ambao ni Bibi Jane na Bibi Grace pamoja na wasifu wao, Ikiwa biashra ina wafanyakazi wengi unaweza kuchora chati ya utawala, Jane kwa kuwa wafanyakazi ni wachache hatutaweka chati hiyo. Kisha hufuata pengo katika uongozi kama lipo

 

6.3 Wafanyakazi.

Kipengele kidogo cha wafanyakazi unaelezea jumla ya wafanyakazi waliopo na majukumu yao wakiwemo na waanzilishi. 


6.4 Mpango wa malipo

Kwenye mpango wa malipo unaweza ukaelezea kwa maneno kisha na kufuatiwa na jedwali la mishahara kuonyesha kwa mwaka mzima wa kwanza ni mishahara kiasi gani italipwa.

Siku ya tatu kesho tutajifunza Kipengele cha Fedha pamoja na Vielelezo. Hakikisha pia unapata michanganuo yote 2 ya Jane Fast food na Jane Restaurant kwa kiingereza na kwa kiswahili


FUATILA ZAIDI HAPA

UTANGULIZI WA SEMINA

SEMINA SIKU YA 1

SEMINA SIKU YA 3

SEMINA SIKU YA 4


Kwa maswali, Simu/watsap: 0765553030  /  0712202244

0 Response to "SEMINA SIKU YA PILI: MIKAKATI, UTEKELEZAJI NA UONGOZI (JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN)"

Post a Comment