SEMINA SIKU YA 3 MASUALA YA FEDHA : HATUA KWA HATUA MPANGO WA BIASHARA YA JANE RESTAURANT | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEMINA SIKU YA 3 MASUALA YA FEDHA : HATUA KWA HATUA MPANGO WA BIASHARA YA JANE RESTAURANT

Chipsi yai na mishikaki

Kwa marejeo na mwendelezo mzuri wa makala hizi hakikisha unacho kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na michanganuo 3 ya Jane Fast Food na Jane Restaurant kwa Kiswahili na Kiingereza.


7.0 MPANGO WA FEDHA.

Ingawa huko nyuma tumewahi kuona baadhi ya maeneo yanayogusa hesabu lakini katika sura hii ndipo majumuisho ya hesabu zote ndogondogo mfano mauzo na gharama zake, gharama za uendeshaji za kudumu pamoja na mpango wa malipo kwenye Uongozi na wafanyakazi. Vipengele vidogo katika Sura hii ni hivi vifuatavyo,

7.1 Makisio muhimu
7.2 Mauzo yatakayorudisha gharama zote (break even sales)
7.3 Makisio ya Faida na Hasara
7.4 Makisio ya Fedha taslimu
7.5 Makisio ya mali na madeni (Mizania ya biashara)
7.6 Uwiano wa Sehemu muhimu za biashara


7.1 Makisio muhimu

Hizi ni dhana za makisio zitakazokuongoza kwenye makisio
yako. Ni vigezo vitakavyotumika kukisia hesabu na katika mgahawa wa Jane dhana au makisio muhimu ni haya;

·       Tunakisia uchumi imara usiokuwa na misukosuko mikubwa.

·       Hatutanunua wala kuuza kwa mkopo, kila bidhaa na huduma italipwa kwa fedha taslimu.

·       Asilimia ya gharama za mauzo = 40%

·       Wastani wa bei ya mlo mmoja ni shilingi 2,600

·       Eneo la biashara ni meta za mraba 300

·       Kutakuwa na meza 6 zenye viti 6 kila moja, jumla ni viti 36 pamoja na eneo la kutosha la kuegesha magari ya wateja.

·       Jumla ya wafanyakazi: 10.

·       Ongezeko la mauzo kwa mwaka ni asilimia: 10%

·       Riba ya mkopo wa muda mfupi: 10%

·       Kiwango cha kodi asilimia: 30%

7.2 Mauzo yatakayorudisha gharama zote (break even sales)

Maana yake ni pale jumla ya mauzo inapolingana na jumla ya gharama zote zilizotumika. Kanuni ya kukokotoa mauzo hayo ni hii hapa; Mauzo ya kurudisha gaharama

 

= Gharama za kudumu ÷ 1- (Gharama zinazobadilika ÷ mauzo)

 

Vitu vyote unakuwa umeshavipata katika hesabu ndogondogo huko nyuma wakati wa kukisia mauzo, gharama za mauzo na bajeti (gharama za kudumu)

 

Kuchora chati ya Break even sales tutatumia kanuni hii kutengeneza jedwali letu la data;

 

FAIDA = MAUZO – GHARAMA ZA MAUZO – GHARAMA ZA KUDUMU

 

Ambapo; GHARAMA ZA MAUZO = asilimia40% ya MAUZO

 

7.3 Makisio ya Faida na Hasara

Taarifa hii ni rahisi na ambayo ndiyo msingi wa taarifa nyingine zote mbili zilizosalia, ile ya mtiririko wa fedha na mizania ya biashara. Unaikokotoa ukitumia namba ambazo tayari tulishazipata huko nyuma kwenye makisio ya mauzo, gharama za mauzo na gharama za kudumu. Pia kodi inajulikana ni asilimia 30% na riba mkopo asilimia 10% kwa mujibu wa makisio yetu muhimu pale mwanzoni mwa sura hii ya fedha. Ili kupata faida halisi unachukua Mauzo na kutoa gharama za mauzo kisha unatoa gharama za kudumu za uendehaji pamoja na kodi na riba ya mkopo............Inaendelea, 


Kupata mfululizo mzima wa semina hii pamoja na Michanganuo yenyewe kamili kwa Kiswahili na Kiingereza jiunge na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE ambapo kila siku tunajadili michanganuo ya biashara zinazolipa Tanzania na masomo ya mzunguko wa fedha. Kiingilio ni Tsh. 10,000/= kwa mwaka unapata na vitabu bure. 


 FUATILA ZAIDI HAPA

UTANGULIZI WA SEMINA

SEMINA SIKU YA 1

SEMINA SIKU YA 2

SEMINA SIKU YA 4


Kwa maswali, Simu/watsap: 0765553030  /  0712202244

0 Response to "SEMINA SIKU YA 3 MASUALA YA FEDHA : HATUA KWA HATUA MPANGO WA BIASHARA YA JANE RESTAURANT"

Post a Comment