USIRI WA PESA KWENYE MAHUSIANO YA NDOA, CHANZO, ATHARI NA SULUHISHO LAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

USIRI WA PESA KWENYE MAHUSIANO YA NDOA, CHANZO, ATHARI NA SULUHISHO LAKE

Katika utafiti mmoja uliofanywa na wanasaikolojia, imebainika kwamba asilimia 23% ya watu waliokuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi kila mmoja humtuhumu mwenzi wake kwamba anaficha siri za fedha. Usiri kwenye masuala ya fedha unaweza kuwa mkubwa kupindukia, wakati mwingine hata mume au mke anaweza akaficha deni la mamilioni ya shilingi alilokopa mahali. 


Dalili za ukosefu wa uaminifu kwenye fedha (usiri wa fedha) huanza mapema kabisa kabla hata wachumba hawajaamua kuoana na kuwa wanandoa kamili. Changamoto kama hizi kwenye mahusiano yafaa wahusika kuzibaini mapema na kuzitafutia suluhisho kama tutakavyoenda kuona mwishoni mwa somo hili. 

SOMA: Mwanaume kupungua nguvu za kiume, pesa na maisha magumu yanavyochangia

Kuna kisa kimoja cha kweli kiliwahi kutokea, mwanamke alijenga nyumba mpaka ikakamilika mumewe hana habari, mume alipokuja kugundua ulizuka ugomvi mkubwa! Hali ni hivyohivyo ilivyo kwa baadhi ya wanaume, wengine hujenga nyumba mpaka imekamilika mwanamke anakuja tu kuambiwa siku wanahamia.

 

Katika utafiti huo pia, watafiti waligundua kwamba nusu ya wale waliokuwa kwenye mahusiano (45%) walikuwa na mikopo ambayo wenza wao hawakuwa na taarifa yeyote kuihusu.

 

Sasa basi ni kwanini tunapenda kuwaficha wenzi wetu masuala yanayohusiana na pesa? Usije ukadhania kwamba jambo hili (usiri wa fedha kwa wanandoa) umeanza leo au jana hapana, ni tabia ambazo tumekuwa tukirithishana vizazi na vizazi tokea mababu na mabibi. Tulipokuwa watoto tulishuhudia wazazi wetu walivyokuwa wakisimamia maswala yao ya fedha, ikiwa walikuwa wawazi kuhusiana nalo au walikuwa wasiri. Bila shaka utakumbuka wakati fulani hivi mama alipotumiwa pesa na dada au kaka aliyeishi mjini kisha akawaambia wewe na wadogo zako hivi, “ Msimwambie baba yenu kaka katuma kiasi hiki” au mama alipokuwa akikuambia, “Usije ukasema kwa babaako nimekununulia hiki na kile”


 SOMA: Wanawake na hisia za usaliti: zijue dalili zake!!

Kauli kama hizo zina uwezo wa kupandikiza kwenye akili ya mtoto utovu wa uaminifu katika suala zima la fedha jambo litakalokuja kumuathiri mpaka ukubwani. Leo hii tunaweza tusifahamu ni kwanini tunapenda kufanya usiri kwenye pesa lakini kumbe tunasahau kile tunachokifanya ni kukopi /kusoma chapa iliyochorwa akilini tangia utoto wetu mithili ya vile uonavyo nyimbo au video zinavyorekodiwa katika memory card au flash

 

Tabia za fedha mtu anazoonyesha ukubwani zilianza kujitengeneza akilini mwake tangu pale ulipokuwa na umri wa miaka 3 na kufikia ukomavu wake katika umri wa miaka 7. Tukiwa wadogo pia tulizoea kusikia wazazi wetu wakitamka maneno kama vile; “Hatuwezi kununua kitu fulani  au “Unatakiwa kuweka akiba fedha yako ya shule unayopewa asubuhi badala ya kwenda kula pipi” Kauli hizi zinamaanisha kukukataza , kukuambia huwezi kutosheleza shauku yako mwenyewe na kwamba uwezo huo wanao wakubwa tu


SOMA: Kwanini huruma na upendo wa wazazi wengi kwa mtoto hupita kiasi? 


Matokeo yake ni kwamba tunapokuja kuwa watu wazima na kupata pesa zetu wenyewe sasa tunashawishika kuzitumia kwa mbwembwe kutimiza ule uhuru tulioelezwa na wazazi wetu kwamba wanao wakubwa tu peke yao, Huwa tunasahau kabisa kama kuna suala tena la kuweka akiba. Zile sauti za “Hapana, usifanye hiki au kile” hatimaye zinatufanya tunakuwa wasiri kwa wenza wetu kuhusiana na suala zima la matumizi ya fedha.

 

Tunajihisi kuwa ni wenye hatia au kuogopa kwamba tutaonekana ni watu walafi au wabinafsi. Katika mahusiano ni dhahiri kabisa kwamba wenza wote wawili watakuwa na tofauti kubwa katika uzoefu kwenye makuzi yao linapokuja suala la usiri wa pesa, hii humaanisha wenza wanaweza wakakwepa kuzungumza kwa uwazi kuhusu pesa zao na mara nyingi watatunza siri zao kuhusiana na maswala ya pesa au mkopo................................................


Somo hili bado linaendelea halijaisha, kulifungua somo zima unatakiwa kujiunga na Mastermind group la MICHANGANUO-ONLINE2021 ambalo kiingilio kwa mwaka mzma ni sh. 10,000/= tu. Mtu anapojiunga tunamtumia vitabu na michanganuo ya biashara hapohapo kisha anaweza kudownload masomo mbalimbali yaliyopita kwenye channel yetu ya Telegram. Katika group pia tunakuwa na Semina za mara kwa mara juu ya uandishi wa michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa haraka.


Kujiunga, lipia kiingilio chako kupitia namba zetu, 0765553030 au 0712202244 na jina ni Peter Augustino Tarimo. Kisha nitumie ujumbe kwa watsap 0765553030 au SMS ya kawaida usemao. "NIUNGE MASTERMIND GROUP NA CHANNEL YA MICHANGANUO-ONLINE2021". Baada ya hapo nitakuunga mara moja pamoja na kukutumia kila kitu huku ukipata masomo ya fedha kama hili kila siku saa 3 usiku.


Imeandikwa na: 

Peter Augustino Tarimo

Mwandishi, mjasiriamali na mhamasishaji viwanda.


0 Response to "USIRI WA PESA KWENYE MAHUSIANO YA NDOA, CHANZO, ATHARI NA SULUHISHO LAKE"

Post a Comment