Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume huwezi
ukasema lina chanzo kimoja tu. Zipo sababu nyingi zikanazoweza zikasababisha
hali hiyo kumtokea mwanaume yeyote yule katika umri wowote ingawa inawakumba
zaidi wanaume waliopita umri wa miaka 40.
Kufanya tendo la ndoa na mwanamke au kitendo cha kufanya
mapenzi kati ya mume na mke kunahitajika wote wawili kuwa na utulivu wa akili
achilia mbali afya ya kawaida ya kimwili, mtu anaweza akafanya mapenzi wakati
akiwa na malaria lakini siyo akiwa na msongo wa kimawazo. Hamu ya kufanya tendo
la ndoa hutegemea sana vichocheo vilivyoko mwilini ambavyo utendaji kazi wake
nao hutegemea amri zinazotolewa moja kwa moja katika ubongo wa mtu.
Kuna mahusiano makubwa kati ya tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume na tatizo jingine la pesa. Na wanaume ndiyo wahanga wakubwa sana
wa matatizo haya mawili kuliko hata vile ilivyokuwa kwa wenzao wanawake. Uchumi
wa familia kwa mfano unapotetereka mtu wa kwanza kuangaliwa ni mwanamme.
Imejengeka akilini mwa watu wengi kuwa mama na watoto
wanatakiwa kumtegemea baba. Hivyo hali ya pesa inapokuwa ngumu baba huathirika
sana kisaikolojia. Mama atajitahidi kumpa maneno matamu ya mahaba usiku wawapo
kitandani sambamba na staili za mapenzi za kila aina lakini katu mwanaume akili
yake muda wote inakuwa ikiwaza pesa, ni namna gani atakavyoweza kukabiliana na maisha ambayo
familia inamtegemea yeye. Hata siku ya Valentine unaweza kuwakuta wapenzi beach wakifurahia mithili ya picha unayoiona mwishoni mwa makala hii lakini ajabu ni kwamba ungeweza kuwachungulia usiku wawapo chumbani picha utakayoishuhudia ni kama ile unayoiona mwanzoni kabisa mwa makala hii.
Hufika hatua kwa wanawake wengine wasioelewa tatizo hili
kwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta dawa ya mapenzi wakihisi ndoa zao
kukumbwa na jinni mahaba au hata uwezekano wa mume kuwa na nyumba ndogo au
vimada nje ya ndoa, lakini kumbe hawajui ndio wanazidisha mambo kuwa mabaya
zaidi kwa kuchukua pesa kidogo kwa ajili ya matumizi ya familia na kwenda
kuwapelekea waganga matapeli.
Kwa mwanamke asiyekuwa mvumilivu wala kujua chanzo cha
tatizo la mwanamume kupungukiwa nguvu za kiume
anaweza akachanganyikiwa sana kiasi cha kuamua kutoka nje ya ndoa yake
na kwenda kulala na wanaume wengine kumbe ilikuwa ampe tu ushirikiano waweze
kuondokana na hali ngumu ya kiuchumi na mambo kurudi kama zamani.
Vichocheo vinavyosababisha ashiki ya mapenzi kwa mwanaume
kama testosteron huathiriwa kwa kiasi kikubwa na msongo wa mawazo. Wanaume
wengi wanapokuwa na hali kama hiyo, huzidisha mashaka na kutojiamini huku
akihisi kama vile tayari ameshageuka hanithi, ikishafikia hatua kama hii
mwanaume inakuwa vigumu hata kumfikisha mkewe kileleni wakati wa tendo la ndoa
huku na yeye akiwahi kufika kileleni isivyokawaida wakati wa tendo hilo.
Uwezo wa mwanaume kumpa mwanamke mimba unaweza
usiathirike sana lakini hata hivyo wakati mwingine unaweza kupungua kutokana na
ukweli kwamba ili mwanamke aweze kupata ujauzito, mbegu ya mwanaume na yai la
mwanamke ni lazima viungane katika mji wa mimba lakini kwa bahati na sibu,
hauwezi ukasema kwa uhakika kabisa kwamba leo hii X na Y wakijamiiana basi
mimba lazima itunge japo tunaweza tu kubashiri.
Kwa hiyo mimba ili itunge wanandoa au wapenzi hawana budi
kujamiiana mara nyingi zaidi siku wanazobashiri kutafuta ujauzito. Sasa utaona
kwamba baba kama anakuwa na tatizo hili la msongo wa mawazo kutokana na
matatizo ya kifedha basi hataweza kushiriki kitendo hicho mara nyingi kama
inavyotakiwa na moja kwa moja kupelekea pia tatizo la mwanamke kushika mimba
kuweza kutokea.
Wanaume wengi wanaopatwa na tatizo hili badala ya kusaka
suluhisho la kudum , hujidanganya kwa utatuzi wa muda mfupi kwa mfano kutumia
dawa za kutibu upungufu wa nguvu za kiume kama Viagra, dawa za kienyeji mfano
mkuyati na mitishamba ya kila aina, dawa za kichina zinazotibu upungufu wa
nguvu za kiume, pamoja na vilevi mbalimbali mfano pombe zenye spiriti kama vile
viroba serikali ilivyopiga marufuku na hata pombe nyinginezo za chupa
zinazotumika mpaka sasa.
Hutumia pia kwa wingi sana vyakula kama vile, mihogo
mibichi, nazi, karanga mbichi, mlenda, mayai, vyakula vya baharini kama pweza,
ngisi, supu au mchuzi wa pweza, samaki nk. Vyakula hivi na madawa kweli vina
uwezo wa kumpa mtu nyege au ashki ya muda mfupi lakini haviwezi kuwa na uwezo
wa kumuondolea tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume moja kwa moja kama chanzo
chake ni msongo wa kimawazo.
Ikiwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa mwanaume
linatokana na sababu za msongo wa mawazo unaosababishwa na matatizo ya pesa au
shida za kiuchumi inafaa zaidi mwanamume na hasa ikiwa kama ameoa, yeye na mke
wake wakae chini na kuanza kulitafakari tatizo lililokuwa mbele yao na kubuni njia za kuweza kulitatua. Wanandoa
wanaweza wakaazimia kubuni miradi midogomidogo kama ile iliyoelezwa katika
kitabu hiki cha MIFEREJI 7 YA PESA, ili kuongeza zaidi kipato cha familia
badala ya kutegemea tu shughuli zao za kawaida za msingi walizozoea.
Kwa njia ya majadiliano kati ya mwanaume na mwanamke,
tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza hata likatoweka lenyewe bila ya
matibabu au hata kabla ya kuanza kuchukua hatua za kusaka utatuzi wenyewe wa
kiuchumi kwani matatizo ya nguvu za kiume mara nyingi huchangiwa zaidi na
sababu za kisaikolojia kuliko hata sababu nyingine zote kwa pamoja. Mwanamume
inawezekana wakati mwingine hata ni sababu za hofu tu ya kuona labda mkewe
atamfikiriaje pindi anapokuwa na dalili za tatizo hili, ndiko kunakosababisha
tatizo lizidi kuwa kubwa.
……………………………………….
Mpenzi msomaji, Nakukaribisha katika Group letu la masomo
ya kila siku ambapo tunajadili, jinsi ya kuboresha mizunguko ya pesa kwenye biashara
zetu pamoja na kuchambua michanganuo ya biashara bunifu zilizo na fursa kubwa
ya kutengeneza faida. Tunapata pia wasaa wa kushirikishana wenyewe fursa
mbalimbali za kimasoko kwa biashara zetu.
Mbali na masomo hayo ya kila siku pia mara ujiungapo tu
hivi tunakutumia offa ya vitu vifuatavyo bila malipo ya ziada;
1. Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI katika lugha ya kiswahili.
2. Kitabu maarufu zaidi cha
michanganuo" HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa kiingereza.Kinatumiwa na
karibu vyuo vikubwa vyote duniani.
3. Templates/Vielezo kwa ajili ya
kurahisisha kazi ya kuandika mpango wako wa biashara, unajaza tu taarifa kuhusu
biashara yako basi umemaliza.
4. Kifurushi chenye michanganuo kamili 3,
kuku wa mayai wa kisasa, kuku wa mayai wa kienyeji na kuku wa nyama wa kisasa,(ofa
yake ni ya muda mfupi sana kitaondolewa karibuni)
5. Masomo yote ya semina zilizopita.
Ada ni shilingi elfu 10, namba za malipo ni 0712202244 au
0765553030 jina Peter Augustino Tarimo
Whatsapp: 0765553030, tuma ujumbe NIUNGANISHE GROUP LA MICHANGANUO
ONLINE Baada ya kulipia. Usisahau na anuani ya GMAIL kwa ajili ya kukuunganisha
na blogu ya private.
Ikiwa hutumii whatsapp hamna shida kwani masomo haya pia
yanatumwa kwa njia za email na katika blogu ya private kea ajili ya wanagroup.
0 Response to "MWANAUME KUPUNGUA NGUVU ZA KIUME PESA NA MAISHA MAGUMU YANAVYOCHANGIA"
Post a Comment