NI KWELI UNAWEZA KUTENGENEZA PESA NYINGI HARAKA KWA BIASHARA YA MTANDAO, MULT LEVEL MARKETING? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI KWELI UNAWEZA KUTENGENEZA PESA NYINGI HARAKA KWA BIASHARA YA MTANDAO, MULT LEVEL MARKETING?

Wana biashara ya mtandao

Bila shaka umewahi kusikia au hata kualikwa kwenye mikutano ya wanabiashara za mtandao maarufu kama Netwok Marketing au Mult-level Marketing(MLM). Biashara za namna hii zimeenea karibu mabara yote Duniani huku zikihusisha biashara ya mamilioni ya pesa.

 

Maana hasa ya biashara ya Mtandao/Mult-level marketing au network marketing

Biashara hii imekuwa ikipewa maana nyingi na hivyo pia kumekuwa na majina tofauti yanayoielezea. Wapo wanaoiita Network marketing, wengine Direct selling na wengine, Multlevel marketing. Biashara ya mtandao pia imekuwa ikinasibishwa na upatu ujulikanao kwa kimombo kama Ponzy cheme au Pyramid schemes jambo linaloifanya biashara hii kutiliwa mashaka na watu wengi japo ni halali na inayokubalika kimataifa.

 

Ili kutofautisha mbichi na mbivu, hebu kwanza tuone maana halisi ya dhana hizi mbili, biashara halali ya mtandao(Mult-level Marketing) au Network Marketing na ile isiyokuwa halali ya upatu wa Pyramid scheme.

 

Biashara ya mtandao maana yake ni biashara inayohusisha watu wengi katika kuuza bidhaa ama huduma na mara nyingi huwa ni bidhaa za afya, urembo, chakula na hata  vitabu. Mshiriki anaweza akaingiza pesa kwa njia mbili, yakwanza kwa kuuza bidhaa au huduma lakini ya pili ni kila pale anaposhawishi mwanachama mpya kujiunga hukatiwa kamisheni.

 

Upatu wa pyramid/ponzy scheme kwa upande mwingine ni biashara haramu ya kitapeli ambayo malengo yake makuu siyo kuuza bidhaa au huduma bali wanaingiza pesa kwa kuwahadaa wanachama wapya wanaojiunga na kampuni kuwa watavuna gawio kubwa pasipo hatari yeyote ile. Wakati huohuo kiingilio chao kikitumika kuwalipa gawio wale wanachama waliotangulia kujiunga. Kampuni inaweza kuzuga hata inauza bidhaa au huduma lakini kumbe hilo siyo lengo lao kuu.

 

Hapa unaweza ukaona kwamba kuna makampuni mengi yanayokuja kwa mgongo wa network marketing lakini kumbe agenda yao kubwa ni kuendesha upatu wa pyramid/ponzy scheme biashara ambayo mwisho wake ni kuanguka na wanachama wengi wale wa mwisho kuambulia kupoteza fedha zao zote walizowekeza kama mtaji baada ya kudanganywa wangevuna faida mara mbili(2)au hata mara kumi ya mtaji waliowekeza.

 

Utaitambuaje kampuni ya biashara mtandao kama ni halali au ni matapeli wa upatu wa Pyramid scheme?

·       Kampuni halali huwa haitoi ahadi za mtu kupata utajiri wa haraka, ukiona wawakilishi wa kampuni wakikukazaia ujiunge kwa ahadi ya kutajirika ghafla(kuwa milionea siku moja au mbili), fikiria mara mbilimbili kujiunga.

 

·       Kampuni halali wanachama wake wanategemea zaidi katika uuzaji wa bidhaa/huduma na wala siyo kuingiza watu wapya. Kipato kutokana na kuingiza watu wapya kwao ni kama ziada tu.

 

·       Kampuni Itakutaka kununua bidhaa za kuanzia, kifurushi hicho cha kuanzia huwa kimebeba pia na matangazo yatakayotumika kuvutia wateja

 

Mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajiunga na kampuni ya mtandao;

·       Zingatia gharama za kununulia bidhaa za kuanzia kama ni shilingi ngapi, ikiwa ni kubwa sana, jiulize utazirudisha  vipi?

·       Ni mauzo kiasi gani utakayofanya ili kurudisha kianzio chako ulichotoa?

·       Je mauzo ni kweli yanawezekana? bidhaa au huduma ni vitu vinavyoweza kuhitajika na jamii inayokuzunguka?

·       Utahita muda kiasi gani kuingiza faida, je muda huo ukilinganisha na kazi au biashara zingine kweli kuna tija?

·       Ili kutengeneza pesa ni lazima uingize wanachama wapya?

·       Je upo tayari kushawishi ndugu na jamaa zako wa karibu kujiunga na kampuni hiyo bila hatari ya kuja kutokea ugomvi au kutokuelewana hapo baadae?

·       Zingatia athari zozote zinazoweza kuja kukupata katika mahusiano yako na ndugu, jamaa na marafiki.

 

Biashara ya mtandao (MLM) ni kweli inaweza kumpa mtu kipato cha uhakika na haraka?

Ukiachana na ahadi nyingi hasa…………….

.................................................................. 

Ndugu msomajia somo hili bado halijafika mwisho hapa, litaendelea kwenye group la Michanganuo-online leo hii usiku. Kujiunga na group hili la masomo ya fedha kila siku kuna kiingilio sh. elfu 10 ada ya mwaka mzima. Pamoja na masomo ya kila siku lakini pia kuna semina za mara kwa mara juu ya uandishi wa michanganuo ya biashara zinazolipa. Ukijiunga pia unapata papo hapo vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara iliyoandaliwa tayari.


Kulipia namba zetu ni 0765553030 au 0712202244 jina: Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma ujumbe watsap 0765553030 usemao; "NIUNGE MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE2021"

0 Response to "NI KWELI UNAWEZA KUTENGENEZA PESA NYINGI HARAKA KWA BIASHARA YA MTANDAO, MULT LEVEL MARKETING?"

Post a Comment