BIASHARA YA MTAJI MDOGO YENYE FAIDA KUBWA ZAIDI TANZANIA ILIVYOSHANGAZA DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA


CHIPSI MAYAI MEZANI
Bada ya kutangaza tungekuwa na somo la mchanganuo wabiashara yenye faida kubwa na mtaji mdogo, darasa lilikuwa moto! Kila mtu(members) alikuwa na shauku kubwa sana (over excited) ya kufuatilia kwa umakini somo la kuandika mchanganuo wa biashara ya chipsi iliyopo eneo la stendi ya Buguruni-Muhimbili. Kwa kweli wengi walionekana kutokuamini kama biashara ya chipsi ni biasharainayohitaji mtaji mdogo sana lakini yenye kulipa faida kubwa kiasi ambacho ndani ya mwezi mmoja tu na siku tano mtaji wote uliowekeza unaweza ukarudi.

Kabla sijaenda kukuonyesha jinsi wanagroup walivyohamasika mpaka mtoa somo akaamua kuanza somo hilo saa 12 jioni badala ya saa 3 usiku, ngoja kidogo nielezee jinsi  biashara hii ya chipsi inavyolipa haraka kwa mtaji kidogo. Zipo biashara nyingi zenye faida ya haraka unazoweza ukaanzisha na mtaji mdogo lakini kulingana na utafiti tulioufanya biashara ya chipsi inashika nafasi ya juu kabisa miongoni mwa orodha ya biashara ndogondogo zenye faidakubwa mara mbili ya mtaji unaowekeza.


Biashara ya nguo kwa mfano, iwe ni nguo za mitumba au hata nguo za spesho za kushona nayo ni biashara nyingine ya uhakika isiyopitwa na wakati muda wote, kuna biashara ya duka la rejareja, hali kadhalika na biashara ya kuosha magari. Biashara zote hizi na nyingine tunazoandikia michanganuo ya biashara zake kila siku katika group letu zipo katika orodha ya biashara ndogo zinazolipa faida haraka kwa mtaji kidogo.

Biashara kama hii ya chipsi kwa mfano unatumia kiasi cha fedha chini ya shilingi milioni moja lakini faida yake kwa siku unapata hadi shilingi elfu 30. Hapo kwa haraka haraka hebu chukua tu lali 9 (900,000/=) kisha gawa kwa elfu thelathini(30,000). Hapo jibu utapata 30, maana yake ni kwamba kwa muda wa siku 30 tu zile laki 9 zinakuwa zimesharudi na faida hiyo ya elfu 30 kuipata ni rahisi sana, utauza chipsi ndoo mbili au tatu tu, kuku wasiozidi 2, mayai trei 2 na nusu, mishikaki kama kilo moja, pengine na ndizi mbili tatu tu hivi.


Katika group la masomo ya kila siku ya Fedha na Michanganuo ya biashara la MICHANGANUO-ONLINE, tumeanzisha utaratibu wa kuandika hatua kwa hatua michanganuo ya biashara ndogondogo zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo wa kuanzia. Michanganuo hiyo huwa tunaiandika kwa kutumia njia rahisi sana ambayo mjasiriamali anaweza akajifunza njia hiyo na kuweza kuandika mwenyewe mchanganuo wa biashara nyingine yeyote ile inayolipa na aipendayo.

Baada ya kuandika kwa njia rahisi pia huwa tunaonyesha jinsi ya kuandika mchanganuo huo kwa njia ile ya kawaida (traditional business plan writing) njia ya kuandika mchanganuo wa biashara iliyozoeleka na wataalamu (Business plan Experties). Kwahiyo utaratibu huu ni mzuri siyo tu kwa wajasiriamali wadogo bali hata kwa wafanyabiashara walio na mawazo mazuri ya biashara lakini wangependa andiko la biashara zao kwa njia nyepesi kwa wafadhili, benki au wabia ili kuweza kupa mitaji ya kuendeshea biashara za ndoto zao. Baada ya hayo machache sasa hebu tukaone jinsi darasa letu la whatsapp lilivyohamasika jana;


Darasa lilianza hivi;

Karibuni members kwenye darasa letu la Michanganuo,
Leo tunachambua biashara ya chipsi iitwayo AMANI CHIPS CENTRE iliyopo stendi ya Buguruni-Muhimbili. Tutaanza kwanza na mchanganuo mfupi kama trela vile, kisha baada ya hapo tutakwenda kuona mchanganuo kamili mrefu wenye vipengele vyote muhimu.


tulipokuwa tukianza


1. Utambulisho wa biashara          
Hapa kama kawaida tuielezea kwa maneno machache kabisa biashara.

Amani Chips centre ni biashara itakayotoa huduma bora za chipsi kwa madereva na makondakta katika stendi ya Buguruni Muhimbili wasio na muda wa kwenda kula majumbani

utambulisho wa biashara


Hapa ni wanagroup wakisubiri kwa shauku somo:Mchanganuo wenyewe kamili wa Amani Chips centre huu hapa;

Amani chips centre business plan

Asante sana nina ndugu alikuwa anataka kuanzisha biashara hii, mchanganuo huu utamsaidia sana;

shuhuda za wadau somo la mpango wa biashara ya chipsi


Nashukuru kaka Peter kwa mchanganuo huu. Kuna kitu kikubwa nimejifunza. Asante

shukrani

Mimi binafsi nimeupenda huu uchambuzi na mpango. umekaa vizuri na umezingatia vigezo muhimu katika mchanganuo wake;


Mimi pia nasubiria kwa hamu nimefungua kama mara mbili lakini nafeli, nataka kujua kinachonikwamisha ni nini? nasubiri somo;

mrejesho wa wadau mbalimbali kwenye group la Michanganuo-online


.....................................................

Je, unahitaji kuandikiwa mchanganuo wa biashara yako au kujifunza kwa njia rahisi namna ya kuandika mwenyewe?

1.   Tunaandika mipango ya biashara za aina zote kwa gharama nafuu sana kuanzia asilimia 1% mpaka 2% tu ya mtaji wa biashara unayotaka tukuandikie. Cha kufanya tu ni kwamba, tukishakubaliana na kututumia mahitaji ya mpango wako online, unalipia nusu ya gharama kisha tunaaza mara moja kazi kwa siku 3 – 5. Baada ya hapo tunakutumia mchanganuo wako kamili.

2.   Ukitaka kuandika mpango wa biashara yako mwenyewe pia unaweza ukawasiliana na sisi(watsap: 0765553030) tukakutumia resources zote muhimu, vitabu, seminars, templates na michanganuo ya mfano/business plan samples, za Kiswahili na kiingereza vitakavyokurahisishia kazi ya kuandika mchanganuo wako kwa wepesi.

.WASILIANA NASI KWA NAMBA:
0765553030 au 0712202244
WASAP: 0765553030
Jina: Peter Augustino Tarimo

.Kupata vitabu vyetu mbalimbali na Michanganuo tembelea Duka la vitabu mtandaoni la SMART BOOKS TANZANIA


.Kujiunga na group letu la whatsapp la masomo ya kila siku, lipia ada ya mwaka sh. elfu 10 kisha unitumie ujumbe nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia offa ya masomo, michanganuo na vitabu muda huohuo

0 Response to "BIASHARA YA MTAJI MDOGO YENYE FAIDA KUBWA ZAIDI TANZANIA ILIVYOSHANGAZA DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA"

Post a Comment