KWANINI TUNAISINGIZIA PESA KILA TATIZO LINALOTUPATA KATIKA MAISHA YETU?

Mwanamuziki Michael Jackson na Whitney Houston
Naomba usininukuu vibaya, katika somo hili sizungumzii matatizo ya pesa yatokanayo na magojwa, ajali au kufiwa, bali ni matatizo yote ambayo mara nyingi hutokana na matakwa yetu wenyewe au matumizi ya hiyari ya pesa.

Umewahi kuwaza siku moja kwamba hata kama ungeoliongezewa mshahara mara 2 ya ule wa sasa bado usingeliweza kumaliza matatizo yako ya fedha yanayokukabili?. Kuna wakati mwingine mtu hata angepata mshahara  sawa na ule anaopata bosi wake bado ataendelea tu kuhaha kuwa matatizo hayaishi.

SOMA: Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani.

Chanzo cha hali kama hii kinaweza kikaelezwa kwa ufasaha na kanuni moja mashuhuri ijulikanayo kama Parkinson’s Law ambayo kimsingi inasema hivi; “Matumizi yanapoona kipato kinaongezeka, nayo pia huongezeka kuhakikisha yanakwenda sambamba nayo” Na hii ndiyo sababu kubwa watu wengi sana hulalamika kuwa wanapokuwa hawana pesa mfukoni hakuna tatizo lolote linalojitokeza, lakini mara tu wanaposhika kiasi fulani cha pesa mfukoni, huibuka tatizo linalohitaji kiasi kilekile cha pesa walichoshika. Ni maajabu sana haya!

Watu tunadhani yakwamba dawa ya kukomesha matatizo yetu mbalimbali  ya kimaisha basi ni kupata pesa zaidi, lakini ukweli mara nyingi huwa ni kuyazidisha zaidi matatizo hayo na hili lipo wazi kabisa kwani tuna mifano ya watu wengi tena mashuhuri Duniani na hapa Tanzania.

SOMA: Watu na pesa: yapo makundi matatu(3) duniani, je wajua wewe upo kundi gani?

Unamkunbuka gwiji wa Muziki wa Pop Duniani Michael Jackson maarufu kama Wacko Jacko, wakati fulani aliwahi kuwa Billionea mkubwa lakini huwezi kuamini mpaka siku anaingia kaburini Wacko alikuwa akikabiliwa na madeni ya kutisha, siku za mwisho za uhai wake zilitawaliwa na huzuni ya kutisha. Ni nini alichokosea au kufanya ndivyo sivyo, nitakujulisha taratibu kwenye somo hili adimu.

Naye Mrembo mweusi wa Kimarekani na Muimbaji mashuhuri Whitney Houston licha ya kuchuma mamillioni ya pesa kipindi cha uimbaji wake, baada tu ya kifo chake alikutwa na dolla elfu 29 tu katika akaunti yake ya benki huku akiwa na madeni lukuki. Hali ni hivyohivyo kwa watu wengine maarufu kama vile Marehemu Brenda Facy na wengineo wengi. Kwa upande wa hapa Bongo nisingelipenda niwataje live kwani nadhani utakuwa unawajua mwenyewe.

SOMA: Vipaji, uwezo, akili ni vitu watu wanazaliwa navyo au kujifunza?

Watu wote hawa waliwahi kushika pesa za ajabu, sasa ingelikuwa kama pesa zaidi zina uwezo wa kuondoa matatizo, watu hawa mashuhuri walishindwa vipi kuyaondoa matatizo yao hata kwa kuomba mashabiki wawachangie mia mia mpaka wakaishia kufilisika namna hii?

Ni nini suluhisho la tatizo hili na linasababishwa na kitu gani hasa? Je, unakabiliwa na madeni makubwa yaliyotokana na matumizi yako mwenyewe yasiyokuwa ya lazima? Basi somo hili litakufaa sana hakikisha leo saa 3 hulikosi ndani ya MASTERMIND GROUP LA WASAP LA MICHANGANUO-ONLINE.

Kujiunga Lipia ada ya mwaka mzima sh. Elfu 10 tu uweze kuwahi na Semina ijayo ya jinsi ya kuandaa mchanganuo wa kiwanda cha unga wa Dona(Super) siku ya ya tarehe 20/1/20200 Response to "KWANINI TUNAISINGIZIA PESA KILA TATIZO LINALOTUPATA KATIKA MAISHA YETU?"

Post a Comment