JINSI YA KUKWEPA MITEGO INAYOKUVUTIA KWENYE MATUMIZI MABAYA YA PESA ZAKO (PART-1)

mtego wa pesa, chambo

Pesa siyo kila kitu lakini pia bila pesa maisha katika zama hizi yangelikuwa ni magumu sana. Kwahiyo ni muhimu sana mtu kuzijua mbinu mbalimbali zitakazokusaidia kuitunza pesa na kuitumia kwa uangalifu mkubwa kwani pesa itabakia kuwa rasilimali adimu milele na milele au mpaka mwisho wa Dunia hii.

Ni muhimu pia kufahamu athari za pesa katika namna akili zetu zinavyofikiri kusudi tuweze  kufanya kwa uzuri na kwa utulivu maamuzi mengine yasiyohusiana na fedha kama vile, matumizi bora ya muda, mahusiano, mipango ya ajira, kujitengenezea furaha na kujifunza kwa lengo la kuufahamu zaidi Ulimwengu tunamoishi.

SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha. 

Kwa kuhakikisha unakuwa uko vizuri kiuchumi, unajihakikishia uhuru kamili wa kutatua karibu matatizo mengine yote hapa duniani ikiwemo kuvipata vile vitu unavyovipenda kwa urahisi kabisa kasoro tu yale mambo ambayo Mwenyezi Mungu ndiye mwenye mamlaka ya kushughulika nayo mwenyewe, mfano ni kama vile kifo nk.

Bila ya kuchelewa sasa hebu tukaone ni jinsi gani tunavyoweza kuikwepa mitego hiyo iliyojaa kila mahali kuhakikisha inatuziba tusiwe vizuri kiuchumi;

1. Usiendekeze kupita kiasi matumizi ya vitu vifuatavyo;

·      Kadi za ATM
·      Credit Cards
·      Kukopa vitu na kuja kulipa baadae
·      Malipo ya bidhaa au huduma kwa simu za mkononi
·      Michezo ya Kamari na bahati na sibu
·      Kulipia bidhaa kidogokidogo kabla hujaichukua
·      Kulipia kitu fedha zote kabla hujakichukua

Vitu vyote nilivyovitaja hapo juu havina tofauti na mitego au chambo kinachokusababisha wewe uvutike kufanya matumizi hata mengine usiyokuwa na umuhimu nayo, wakati mwingine hata unanunua vitu usivyovihitaji. Unaponunua kitu mfano ukitumia kadi ya ATM au Credit card huwa huwezi kuhisi maumivu sawasawa na kama vile unavyonunua kwa kutumia pesa taslimu (cash) mfukoni, matokeo yake unajikuta unatumia pesa nyingi bila kujijua.

SOMA: Pesa tuonazo ni makaratasi tu, jifunze njia ya kupata pesa halisi za ukweli.

Halikadhalika muuzaji wa chupa ya chai(thermos) kwa kukopesha anaweza kuja akakuambia, “wewe chukua tu hiyo chupa ya chai utalipa kidogokidogo” matokeo yake hata akikutajia bei mara mbili ya bei halisi huwezi ukapinga, na akili yako itaona ni sawasawa tu kwa kuwa tayari ameshakufanyia hisani(favour) ya kukukopesha.

Imedhibitika kote duniani pasi na shaka kwamba, kufanya manunuzi kwa kulipia ukitumia njia ya fedha taslimu(cash) hupunguza kwa kiasi kikubwa sana matumizi mabaya ya fedha au yale yasiyokuwa ya lazima.

SOMA: Nina mapepo au ni kitu gani, kila nikipata pesa zaidi ya kiwango nilichozoea zinatumika au kupotea kimiujiza katika mazingira ya kushangaza.


2. Wakati mwingine Offa na vijizawadi vya bure hutuponza.
Dunia ni kama  CASINO kubwa lililojaa kila aina ya vivutio  vinavyowafanya watu kutumia pasipo kujijua pesa zao, muda na hata umakini wao kwa vitu ambavyo wakati mwingine hata havina umuhimu kivile.

Unapoingia kwenye Casino utakutana na michezo mbalimbali kwenye mashine za kamari, michezo ya kompyuta na simu pamoja na vitu vingine mbalimbali vyenye mvuto wa ajabu lakini kiuhalisia vitu hivyo vyote vinakufanya tu utoe pesa zako halisi mfukoni kwa ahadi hewa ya kupata zawadi au ushindi mnono usioweza kutabirika kiurahisi.

SOMA: Kwanini wananaosema nikishinda bahati na sibu millioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya kinyume chake?

Binadamu tuna tabia ya kupenda sana vitu vya bure na zawadi hata kama vitu hivyo si muhimu kwetu na kusababisha wakati mwingine “tupigwe” kiurahisi kabisa. Kwa hiyo jambo jema ni kukaa mbali na wale wote wanaoahidi kukupa zawadi nono au offa zisizoweza kutabirika huku wakikutaka kwanza ulipie kiasi fulani cha fedha halisi toka mfukoni mwako.


3. Usipuuzie taaluma na Uzoefu, rahisi mara zote itakugharimu zaidi.
Hebu tuchukulie mfano umepoteza funguo za milango 2 ya nyumba yako inayofanana kwa kila kitu, ukaita mafundi wawili, fundi wa kwanza anatumia dakika 5 tu kuufungua mlango tena bila ya kuuvunja. Fundi wa 2 anatumia masaa 5 akijaribu njia mbalimbali mpaka anafanikiwa kuufungua.

Kwa tabia za binadamu tulivyo, mtu atakuwa tayari kumlipa pesa nzuri yule fundi wa pili aliyetumia masaa 5 kwa imani kwamba amefanya kazi kubwa zaidi na kwa muda mrefu akisahau kwamba yule fundi aliyetumia dakika 5 anao uzoefu na taaluma ya kutosha aliyoisotea pia kwa muda mrefu na kwa gharama, habahatishi kazi.

SOMA: Kanuni: Unaijua thamani ya pesa kwa muda wako ni shilingi ngapi?

Penda kutafuta ufumbuzi wa matatizo yako kutoka kwa wenye taaluma stahiki na uzoefu utaokoa muda na fedha nyingi kuliko kuwafuata watu wa bei chee watakaozidi kukuharibia vitu au kukupotezea muda wako wa thamani ukapata hasara. Nyuma ya taaluma au ujuzi fulani kuna nguvu zilizojificha usizoweza kuziona harakaharaka.

Mpenzi msomaji wa makala hizi, sehemu ya pili ya somo hili ni nzuri kupita hii na itapatikana katika group la MICHANGANUO-MASTERMIND tu. 

Kwa sehemu hiyo ya pili na mamia ya makala nzuri kama hizi zilizowahi kutolewa katika group hilo miaka iliyopita, jiunge kabla ya siku ya tarehe 15 January. Baada ya hapo fursa pekee itakayokuwepo ni kujiunga na kupata masomo mapya tu, hayo ya zamani yatakuwa yameshafungwa.

ILI KUJIUNGA TAFADHALI LIPIA ADA YAKO YA MWAKA MZIMA WA 2020 SH. 10,000/= TU KISHA NITUMIE UJUMBE WATSAP AU WA KAWAIDA USEMAO; 

"NIUNGANISHE NA MASTERMIND GROUP PAMOJA NA OFFA INAYOMALIZIKA MUDA WAKE"

Namba ya malipo na kutuma ujumbe ni;  0765 553030  jina ni Peter Augustino Tarimo

0 Response to "JINSI YA KUKWEPA MITEGO INAYOKUVUTIA KWENYE MATUMIZI MABAYA YA PESA ZAKO (PART-1)"

Post a Comment