KANUNI: UNAIJUA THAMANI YA FEDHA KWA MUDA WAKO NI SHILINGI NGAPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KANUNI: UNAIJUA THAMANI YA FEDHA KWA MUDA WAKO NI SHILINGI NGAPI?


Kukadiria thamani ya fedha ya muda wako hebu jiulize swali hili, kwa mfano unapomwita fundi kutaka arepee kitu kilichoharibika ndani mwako unatumia njia ipi kujua kama utamlipa kiasi gani? Siyo tu kwamba pesa hutumika kama kipimo kwa karibu kila kitu lakini pia ni rasilimali ya kipekee.

SOMA: Je unafahamu thamani yako halisi, pesa, mali na utajiri unaomiliki? Hii hapa njia rahisi ya kukokotoa.

Wakati unapopanga maisha yako, unapobajeti muda wako unatakiwa kuzingatia kwamba unaweza ukaiongeza rasilimali hii zaidi kwa kununua muda wa watu wengine lakini na wakati huohuo uhakikishe ya kwamba unalinganisha gharama zako unaponunua muda wa watu wengine na kutumia muda wako mwenyewe. Katika yote mawili kuna kupoteza pesa zako isipokuwa kwa hilo la pili la kutumia muda wako mwenyewe huwezi kupokea fedha taslimu bali manufaa yake huja baadae.

Swali la kujiuliza hapo ni je, ni muda wa nani kati ya muda wa watu wengine na muda wako mwenyewe una thamani zaidi? Unapokuta muda wako thamani yake ni kubwa kuliko jukumu unalotaka kulifanya basi unaweza ukatumia muda wa watu wengine na kuwalipa bila shida lakini muda wako unapokuwa na thamani ndogo ni bora ukatumia muda wako huohuo. Kimahesabu ni muhimu kutumia kipimo ambacho ni Tsh/saa

SOMA:Thamani ya pesakujiandikisha kupiga kura ni shilingi ngapi?

Kila mtu hutumia muda wake tofauti na mwingine, mfano mtu anayetumia muda wake katika miradi yenye faida kubwa hupata pia pesa nyingi. Mafanikio katika eneo lolote lile la maisha hutegemea kiasi cha muda unaotumika katika eneo husika. Maeneo hayo ni kama vile, utajiri, mahusiano mazuri, uhuru zaidi, afya nk. ingawa huwa aiwezekani mtu kupata au kuwa na vitu hivyo vyote wakati mmoja. Hivyo unatakiwa ufahamu ni kipi unachotaka na kukipa kipaumbele cha kwanza cha muda wako.

SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka. 

Na kabla hujakubali kutumia muda wako katika jukumu fulani hebu jiulize kwanza kama thamani  utakayoipata inalingana na thamani ya muda wako utakaoupeoteza. Mfano unapewa kazi utakayolipwa sh elfu 5 kwa saa moja, je hiyo elfu tano inalingana na thamani ya muda wako? Pengine wewe thamani ya saa yako moja ni sh. elfu 10 basi kazi kama hiyo haikufai achana nayo. Kahiyo unapofahamu kwa saa moja wewe unaingiza kiasi gani utafanya maamuzi sahihi zaidi kwenye shughuli zako za kila siku............................

...............................................................

Somo hili tunajifunza leo hii katika Group la masomo ya kila siku la Michanganuo-online kwa hiyo bado halijaishia hapa kuna kanuni yenyewe ya kutambua thamani ya muda wako bado hujaijua. Masomo yamerudi ni kila siku na tumeongeza kipengele cha Saikolojia ya pesa.

Pia siku ya tarehe 12 tutakuwa na semina kubwa ya JINSI YA KUANDAA HESABU ZA MPANGO WA BIASHARA KWA UNDANI KABISA tafadhali  usikose.

Kiingilio ni sh. elfu 10 na hulipwa kupitia namba zetu 0765553030 au 0712202244 kisha ujumbe wa NIUNGANISHE NA GROUP LA MASOMO. Tunakupa na offa ya masomo yote tuliyojifunza mwaka jana, vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku aina zote.

Ikiwa hutumii WASAP hamna shida masomo yote tunatuma pia katika email na updates zote kila baada ya siku moja au mbili.

ASANTE SANA
Peter Augustino Tarimo
self help Books Tanzania ltd



0 Response to "KANUNI: UNAIJUA THAMANI YA FEDHA KWA MUDA WAKO NI SHILINGI NGAPI?"

Post a Comment