NINA MAPEPO AU NI NINI? KILA NIKIPATA PESA ZAIDI YA KIWANGO NILICHOZOEA ZINATUMIKA AU KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUSHANGAZA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NINA MAPEPO AU NI NINI? KILA NIKIPATA PESA ZAIDI YA KIWANGO NILICHOZOEA ZINATUMIKA AU KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUSHANGAZA

Somo hili la leo katika group la Michanganuo-online nitajibu swali la msomaji wetu mmoja alilouliza kama ifuatavyo;

Habari Peter,
Mimi naishi na mume wangu na kila mmoja kati yetu anapoingiza pesa nyingi kuliko kiasi kile tulichokizoea huwa tunaweka malengo mbalimbali mfano kuweka akiba kwa ajili ya kujenga nyumba yetu wenyewe, kununua gari nk. Lakini cha ajabu ni kuwa mara tu tupatapo pesa hizo, yanajitokeza matumizi  ya ajabuajabu ambayo hata hayakuwepo kabla ya kuzipata. Huibuka magonjwa, faini zisizokuwa na kichwa wala miguu ilimradi tu fedha kwa ajili ya mipango yetu zimetumika tofauti na mipango yenyewe. Imefika mahali sasa hata tunapopata hela nyingi tunaogopa kabisa kuweka lengo lolote. Hii ni hali tu ya kawaida au kuna mapepo ndani yake?

MAJIBU:
Kila mtu anacho kiwango chake cha kushika pesa na ni vigumu sana mtu kupata pesa zaidi kuvuka kiwango hicho lakini kuna njia za kuweza kufanya na kuondoa kizingiti hicho mtu ukaongeza kiwango chako cha upataji wa pesa.

Hebu fanya jaribio lifuatalo, chukua kidumu cha maji lita 5 na kisha uyajaze maji hayo ndani ya kidumu kingine lakini cha lita 1. Ni dhahiri kabisa kwamba maji hayo yataingia mle kiasi cha lita moja tu huku mengine yakimwagika chini na kulowanisha sakafu au meza unayofanyia jaribio hili. Ni wazi pia wala hautahangaika kwenda kulifanya jaribio hili kama nilivyokueleza kwani kimantiki wala haliwezi kuleta maana yeyote ile.




Katika ulimwengu wa pesa kwa kila mtu hali pia inafanana na hii, kuna kiwango fulani cha fedha kila mtu anachoweza kuingiza tu katika maisha yake kama ilivyokuwa kwa dumu la maji la lita moja. Uwezo huo wa mtu wa kupata pesa hauwezi kumruhusu aingize fedha zaidi ya kile kiwango chake alichozoea. Na hata mtu anaweza kusema  afanye kazi kwa juhudi zote na maarifa ili aongeze kipato hicho lakini kila senti itakayoongezeka juu ya kiwango kile itapotea katika mazingira yasiyoeleweka.

Jinsi ya kutambua kiwango cha uwezo wako wa kumiliki pesa na namna ya kukiongeza
Ni rahisi kutambua kiwango chako cha fedha, Kokotoa wastani wa kipato chako cha mwezi kwa miezi 6 iliyopita na jibu hilo ndiyo uwezo wako wa pesa kwa mwezi. Kiasi hiki huwa kama ndio ukanda wako wa faraja(comfort zone) na hukuwekea mipaka kwenye kiwango chako cha mapato, matumizi, madeni na matokeo ya biashara yako kwa ujumla kiasi kwamba ukipata zaidi akili ya ndani inakuzuia.

SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote kile cha pesa unazotaka maishani. 

Kila kinachoongezeka zaidi ya kiwango hicho mtu hujikuta akikipoteza, kukiweka katika miradi isiyofaa, kukopesha watu wengine au atatafuta njia yeyote ile ilimradi tu amekitumia(mfano wa maji kwenye lita 5 yanayozidi kwenye lita 1 na kumwagika sakafuni). Kuna nguvu ya ajabu huja na kuchukua kiasi kilichozidi kupitia matumizi yasiyotarajiwa.

Tatizo hili halisababishwi na nguvu za giza kama unavyofikiri bali lina mizizi yake ndani abisa ya ufahamu wetu(subconscious mind) na kuibadilisha hali hii ni lazima kwanza mtu kuingia moja kwa moja katika mawazo hayo ya ndani na kubadilisha programu tulizoziruhusu wenyewe kuota mizizi pale.

SOMA: Ukweli uliofichwa juu ya pesa, watu hawatafuti kazi bali hutafuta pesa.

Programu hizo hubeba woga, uwongo na kila aina ya mitazamo hasi inayosababisha viwango vya uwezo wetu wa kumiliki pesa visiongezeke. Usipobadilisha mitazamo hiyo daima utaendelea kubakia na uwezo uleule wa kiwango cha fedha ulio nao katika maisha yako yote. Baadhi ya njia za kuongeza kiwango cha uwezo wako wa fedha ni hizi zifuatazo;

..............................................

Somo hili zima tutajifunza leo saa 3 usiku katika group la masomo ya fedha ya kila siku wasap na email. Ukitaka kupata masomo haya kila siku kwa ukamilifu unapaswa kuwa mwanachama wa group hili ambalo kiingilio chake kwa mwaka mzima ni sh. elfu 10 tu.

Namba ya kulipia ni 0765553030 au 0712202244 baada ya malipo tuma ujumbe usemao, NIUNGANISHE NA GROUP LA MASOMO YA PESA KILA SIKU"

Washiriki hupata fursa ya kujifunza masomo kila siku, mijadala mbalimbali na semina za mara kwa mara kama ile tunayokwenda kufanya tarehe 20 mwezi huu wa 3 inayohusu JINSI YA KUANDAA MAHESABU YA MPANGO WA BIASHARA KWA KINA.

Ikiwa hupendi kujiunga na group la wasap unaweza kupata kila kitu kupitia email yako


Pia mtu anapojiunga tunamtumia masomo, vitabu, michanganuo na vitu mbalimbali tulivyowahi kujifunza siku zilizopita kama ifuatavyo;


1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.      Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.      Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.



WASAP: 0765553030
SIMU:     0712202244

JINA: Peter Augustino Tarimo


0 Response to "NINA MAPEPO AU NI NINI? KILA NIKIPATA PESA ZAIDI YA KIWANGO NILICHOZOEA ZINATUMIKA AU KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUSHANGAZA "

Post a Comment