Ndani yako kuna nguvu kubwa kuliko hata ulivyo wewe
mwenyewe, serikali na hata mustakabali mzima wa maisha yako. Binadamu anayo
kawaida ya kuota, kuwa na ndoto au maono(fantasize).
Kuota au kuwa na maono ni uwezo wa kugundua mambo yajayo unaotutofautisha sisi
binadamu na na wanyama wengine.
Faida kubwa kimageuzi binadamu aliyoipata kupitia katika
mabadiliko ya historia yake ni maono(uwezo
wa kubuni vitu kabla havijatokea kuwa vitu halisi) Mfano mmoja ni pale
kabla mtu hajajenga nyumba yake hujaribu kwanza kujenga taswira ya jinsi nyumba
hiyo itakavyoonekana na wakati mwingine hata kuchora na ramani kabisa katika
karatasi ndipo sasa huja kuanza ujenzi mpaka nyumba imekamilika na kuwa kama
vile alivyofikiria mwanzoni.
Mara nyingi njozi za mwanadamu huwa ni zile zenye
kutabiri mambo mazuri na yaliyokuwa bora zaidi kuliko yale yaliyopita na
yaliyopo ndio maana katika mabadiliko ambayo yamekuwa yakitokea Duniani, vitu
huwa bora zaidi kadiri siku zinavyokwenda kuliko siku zilizopita. Kwahiyo
binadamu yeyote yule kuwa na ndoto njema juu ya maisha yake siyo jambo baya
bali ndiyo mwanzo wa mabadiliko yake katika nyanja mbalimbali za kimaisha.
Mfano mmoja mkubwa ni katika biashara zetu na ajira. Mtu
unapaswa uwe na ndoto au maono ya biashara yako au ajira yako miaka zaidi ya
mitano ijayo. Kama leo hii unafanya kazi kama mpokeaji wageni, ndoto zako siku
moja iwe ni kuja kuwa meneja au mkurugenzi wa kampuni. Na ikiwa wewe leo hii
unafanya biashara ya kuuza matikiti maji, maono yako siku moja yawe ni kuja
kumiliki mgahawa mkubwa au biashara ya usafirishaji mizigo na abiria mikoani na
nje ya nchi. Taswira yako ikuonyeshe kabisa ukiwa unamiliki vitu hivyo sasa hivi kabla hujavimiliki kiukweli.
Katika uandishi wa mpango wa biashara (Business
Plan) kuna kipengele kidogo pale mwanzoni baada ya Muhtasari tendaji
cha maono, na hata mpango wenyewe wa biashara unaweza ukasema ni maono kwani
unatabiri mambo ambayo bado hujayafanya kiuhalisia. Lakini kumbuka nimeanza kwa
kusema kuwa chanzo cha mabadiliko yote ya binadamu ni maono.
Hatuwezi kutimiza jambo lolote lile bila kwanza ya
kulifikiria akilini namna tutakavyolitekeleza. Kila mtu anayefanikiwa kwenye
biashara yake aliweka mipango madhubuti. Kinachofanya tuone kama vile watu
hawapangi ni kwamba wengi wanafanya mipango yao kichwani tu na siyo kuiandika
katika maandishi kwenye karatasi. Kwa yule anayepanga kwa maandishi ana
uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kuliko anayepanga tu kichwani.
Kozi ya namna ya kuandaa mpango wa biashara tayari tunayo
na tulishaitoa kwa wale waliojiunga tayari katika group la masomo la
MICHANGANUO-ONLINE. Masomo hayo ni rahisi sana isipokuwa tu kuna kipengele
kimoja cha FEDHA(Financial section) ambacho watu wengi hulalamika ni kigumu.
Sasa tumeandaa semina kubwa itakayohusu eneo hili tu kwa undani kabisa ili kila
mtu anayeliona eneo hili kuwa ni gumu aweze kulielewa barabara. Mtu yeyote akishazifahamu tu kanuni
zinazotumika, ugumu katika kuandaa mchanganuo wa biashara unabakia kuwa
historia kwake.
Semina hii itafanyika mnamo tarehe 20/3/2019 ndani ya
group la masomo la Michanganuo-online kupitia njia za wasap na email. Kiingilio
ni shilingi elfu 10 kwa yule ambaye bado hajajiunga na group la MICHANGANUO-ONLINE.
Mshiriki pamoja na semina yenyewe hupewa pia masomo ya pesa, vitabu, semina na
michanganuo yote tuliyokwishaijadili katika group hilo siku zilizopita tangu
mwaka jana uanze katika mfumo wa softcopy.
SOMA: Sababu 4 kwanini kipengele cha fedha ni moyo wa mpango wa biashara(The heart of a business plan)
Namna za malipo kwa yule ambaye bado hajajiunga ni;
0765553030 au 0712202244 Baada ya malipo tuma ujumbe wa sms au wasap usemao,
“NIUNGANISHE NA GROUP LA SEMINA”
Ikiwa hupendi kujiunga na Magroup ya wasap unaweza
kujiunga na masomo tukakutumia kupitia email yako(Barua pepe)
Ikiwa pia unaona ni vigumu kutoa kiingilio hiki sh. elfu
10 kwa mara moja ni vizuri kuanzia leo hii ukaanza mpango wa kuweka sh. Elfu
moja moja kila siku kwa siku 7 kisha siku nyingine 7 ukaweka sh. 500 kila siku,
baada ya wiki 2 utakuwa umetimiza kiasi chote sh. Elfu 10.
Unaweza ukajiunga mapema kabla ya siku ya semina
ukaendelea kushiriki masomo ya kila siku
ya fedha pamoja na mijadala mingine mbalimbali ndani ya group kuhusiana na
ujasiriamali, biashara na maisha kwa ujumla. Group lina watu makini sana wanaojitambua
na walio na fani mbalimbali katika biashara na kazi.
Dondoo zaidi za semina hii, yaliyomo na ratiba kamili
nitaendelea kukujuza siku hadi siku mpaka tarehe ya semina itakapofika. Hii si semina
ya kukosa kwani haijawahi kuwepo semina nyingine ya namna hii inayochambua
kipengele cha fedha katika mpango wa biashara kwa vitendo na si kwa maelezo
matupu kama wafanyavyo wakufunzi wengi katika mitandao mbalimbali.
WASAP 0765553030
SIMU: 0712202244
Peter Augustino Tarimo
0 Response to "MAONO YAKO NDIYO CHANZO CHA MABADILIKO YAKO (YOUR FANTASIES ARE THE SOURCE OF YOUR CHANGES)"
Post a Comment