WATU NA PESA: YAPO MAKUNDI MATATU(3) DUNIANI, JE WAJUA WEWE UPO KUNDI GANI?


masikini na tajiri
Michezo ya redioni, luninga na hata simulizi mbalimbali za mazombi zilizokuwa zikisimuliwa  tokea enzi na enzi na Wahenga, nyingi zimekuwa zikitoa ujumbe unaohusisha utajiri wa pesa na mambo mbalimbali mabaya kama vile kafara, wizi, unyanganyi, chinjachinja, ushirikina na mambo mengine mengi ya kutisha, wakati umasikini wa pesa umekuwa ukionyeshwa katika upande wa picha ya unyoofu kama vile kwenda peponi baada ya kifo na mambo mengine yote ya kimaadili katika jamii.

Tatizo hili la kupandikiza akilini mwa watu wengi picha hizi mbili huanzia tangia utotoni pale watu katika akili zao za ndani(Subconscious mind) wanapoamini kwamba pesa siyo kitu kizuri bali ni ibilisi, matokeo yake huja kurithisha imani hiyo kwa watoto wao na kuzidi kujenga hali ya umasikini kizazi hata kizazi jambo linalosababisha pia baada ya muda kupita iwe vigumu mno kuing’oa imani hii vichwani mwa watu.

SOMA: Elimu ya pesa a umuhimu wake 2019 njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.

Wakati wote hapa duniani, pesa zimekuwa na umuhimu mkubwa na hasahasa katika zama hizi tulizokuwa nazo karibu kila kitu muhimu maishani huwezi ukakipata ikiwa huna pesa. Pesa imekuwa kama alama ya uwezo/nguvu na njia ya kutengeneza matabaka miongoni mwa binadamu. Pesa pia inaweza ikafananishwa hata na madawa ya kulevya kwa baadhi ya watu kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakizifukuzia na kushindwa kuishi bila ya pesa.

Katika upande huu wa mgawanyo wa pesa kwa watu usiokuwa sawa kuna makundi makubwa matatu (3), wapo wasiokuwa na pesa(Masikini wa kutupa), wale wenye kuwa nazo(matajiri wa kutupa) na wale waliokuwa katikati(hawana pesa nyingi lakini pia siyo masikini)

SOMA: Njia saba7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka

Inavyoonekana ni kwamba baadhi ya watu, pesa zimekuwa zikiwakwepa  kama pande 2 za sumaku zinazofanana wakati kuna wengine wanapozisogelea tu pesa hivi, huwafuata zenyewe mithili ya mbwa amuonapo chatu. Jambo hili limekuwa likiumiza vichwa vya watu wengi sana na kuhoji haki ipo wapi juu ya mazingira haya ya pesa kutoa matokeo tofauti hata pale makundi yote haya 3 yanapoonyesha juhudi sawa katika kuzitafuta. Mpaka wengine wamediriki kusema kwamba pengine hali hii inachangiwa na wao kutokuwa na bahati ya pesa.

Lakini ukweli ni kwamba siyo swala la bahati hata kidogo, katika ulimwengu huu tunamoishi kila jambo hutokea sawasawa  na vile mtu alivyolifikiria kabla. Kila mtu anafahamu kwamba mawazo/fikra ni kitu halisi. Na hii pia hufanya kazi katika mtazamo wa mtu kuhusiana na hali yake kifedha na ndiyo husababisha hasa mgawanyo usiokuwa sawa kwenye umiliki wa pesa duniani.

SOMA: Ufahamu wa pesa ni lazima ujengwe kwa kutaka isipokuwa tu labda mtu azaliwe nao.

1.Watu wa kipato cha kati.
Nitaanza na kundi hili la katikati, watu wa kipato cha wastani, watu hawa katika mawazo yao wanaamini vitu vifuatavyo;
·       Pesa huhitaji mwelekeo wa fikra uliokuwa  wa kadri
·       Pesa hazihitaji kutafutwa  kwa sababu za wivu au husuda  kwamba kwaninin fulani amezipata basi  na mimi ni lazi  nizipate ili nimuonyeshee, iwe isiwe.
·       Pesa hazipaswi kuwa ndio lengo kuu maishani
·       Katika akili ya ndani ya watu hawa huzichukulia pesa kwa mtazamo wa kadiri, huwa hawafukuzani na pesa kupita kiasi  wala hawakai nazo mbali sana.

2.Masikini wa kutupa.
·       Mwelekeo wao wa kifikra kuelekea pesa siyo wa kadiri bali ni hasi kupindukia.
·       Kutokana na kukosa pesa kwa muda mrefu  na vikwazo mbalimbali vya kimaisha wameamua kuzichukia pesa mno katika akili zao za ndani.
·       Tunaweza tukasema watu hawa wameshakubaliana na hali halisi ya kukosa pesa au kupata pesa kidogo sana maisha yao yote na hata vizazi vyao na wala hawana tena haja ya kuhangaika kuzitafuta.
·       Mtazamo wao kuelekea pesa ni wa kinyonge na usiokuwa shindani kabisa.

·       Hawa wana mtazamo ulio kinyume kabisa na ule wa masikini wa kutupa
·       Utajiri wao wengi wameupata kupitia nguvu zao wenyewe pasipo kurithi wala kusaidiwa na ndugu, jamaa na marafiki
·       Katika akili ya ndani kabisa ya watu wa aina hii, mtu hujiwekea lengo kubwa na muhimu la kifedha maishani mwake
·       Wakati mwingine lengo hilo hulihusudu hata kushinda vile linavyostahili
·       Kutengeneza faida kwake inaweza kuwa ni wazo lenye thamani kubwa kwake na lengo kuu maishani
·       Mara nyingi watu wa kundi hili wana mafanikio makubwa kifedha maishani kushinda makundi mengine yote 2
·       Wana wivu balaa wa kimaendeleo, huwa hawakubali wanapoona fulani kafanikiwa mpaka na wao wamefanikiwa.

Yote yaliyoelezwa hapo juu ni asili tu ya mgawanyo wa pesa ulivyo kati ya hayo makundi 3 lakini bado hakuna mapendekezo yeyote yale  ni kwa njia gani basi watu walioko katika makundi mawili ya mwanzo, lile la kati na la masikini wa kutupa wanavyoweza wakajinasua kutoka katika makundi waliyopo na kuingia katika kundi la tatu la Matajiri.

SOMA: Kwanini kufanikiwa kifedha si dhambi na kila mtu anastahili afanikiwe?

Na ukumbuke pia kujitoa katika makundi hayo ni shughuli pevu, ni sawa tu na ku “Uninstall” programu mbaya(virus) kwenye kompyuta ili uweze ku “Install” programu nzuri isiyokuwa na kirusi kwenye kompyuta hiyo. Wakati mwingine  Antivirus’ za hivihivi tu huwa zinagoma na unalazimika kuweka Window upya. Sasa utatumia antivirus gani kuondoa fikra hasi zilizopandikizwa katika akili za watu za ndani kabisa tokea vizazi na vizazi?

.....................................................................

Tuungane kwenye somo hili zima katika group la masomo ya kila siku yahusuyo pesa watsap, la Michanganuo online. Utapata na masomo mengine mengi ya fedha yaliyofundishwa siku zilizopita na ambayo huwezi ukayapata mahali kwingine kokote kule.

Kujiunga na group au masomo haya kwa njia za wasap au Email lipia kiingilio sh. Elfu 10 kisha tuma ujumbe usemao, “NIUNGANISHE NA MASOMO YA FEDHA YA KILA SIKU”
Nitakutumia masomo, semina na vitabu kisha kukuunganisha na group kwa ajili ya masomo ya kila siku yajayo.

Semina ya hivi karibuni kabisa utakayopata pamoja na mchanganuo kamili wa biashara ni ile ya BIASHARA YA KIWANDA KIDOGO CHA TOFALI ZA SARUJI(KILUVYA QUALITY BRICKS) Vitu vingine ni hivi vifuatavyo na offa yake ni ya muda mfupi sana karibu itamalizika;1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Mchanganuo na semina ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara ya mgahawa(JANE FAST FOOD & JANE RESTAURANT)

13.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.


14.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.


Ili kuweza kujinyakulia OFFA hizi zote pamoja na kuendelea kupata masomo kamili ya kila siku yenye maudhui ya pesa lipia kiingilio chako shilingi 10,000/=(ELFU KUMI) kisha tuma ujumbe wa watsap au meseji ya kawaida kupitia namba 0765553030 usemao, "NITUMIE MASOMO YA FEDHA NA OFFA ZAKE"


*Ikiwa hutumii watsap, hamna shida EMAIL inatosha, nitakutumia kila kitu kwa email.*

0 Response to "WATU NA PESA: YAPO MAKUNDI MATATU(3) DUNIANI, JE WAJUA WEWE UPO KUNDI GANI?"

Post a Comment