JE, ULIKOSA SEMINA YETU YA KWANZA YA VIWANDA MWEZI AGOSTI?

Katika mfululizo wa semina za kuandaa mipango ya biashara za viwanda bunifu vinne 2019 tulianza rasmi mwezi huu wa Agost tarehe 15 na tutaendelea mpaka Novemba kila mwezi. Semina yetu hiyo ya kwanza ilikuwa inahusu kiwanda cha kuyfatua tofali za block Kiluvya Mkoani Pwani, na ratiba yake ilikuwa kama ifuatavyo;

SIKU YA KWANZA
Tulijifunza namna utafiti wa biashara hii ulivyofanyika hatua kwa hatua.

SIKU YA PILI
Tukaanza kuandika hatua kwa hatua Sehemu zote 8 za mpango wa biashara hiyo

SIKU YA TATU
Tulijifunza kwa kina na kuandika Kipengele cha fedha(Makisio ya faida na hasara, Break even Point, Pay back Period, Makisio ya mtiririko wa fedha, Mizania ya biashara na Sehemu/Ratios)
Semina hii ilikuwa nzuri na kila mtu aliyeshiriki alinufaika kwani baada tu ya kumalizika watu wengi walianza kuchukua hatua za maandalizi kwa ajili ya viwanda vyao vidogovidogo walivyokuwa wakiota siku nyingi kuvianzisha lakini bila mafaniko. Hatua ya mwanzo kabisa ya kuanzisha kiwanda ni kuandaa mpango utakaokuwezesha kujua unahitaji kitu gani na kwa gharama zipi.

Lengo kuu la semina hizi ni kuchochea moyo wa kuanzisha viwanda nchini, kuunga mkono juhudi za Taifa hili la Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Vilevile ni ili kusaidia wajasiriamali wadogo kuweza kujifunza mbinu mbalimbali za uendeshaji wa biashara za uzalishaji wa bidhaa badala tu ya kung’ang’ania biashara za uchuuzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi ambazo faida yake ni kidogo na haziwezi kuwatoa watu wengi kwenye umasikini.

Ikiwa basi ulikosa semina hii na ulipenda kushiriki, bado kuna fursa ya kuweza kuipata. Tumeweka muda wa wiki moja kwa ambaye hakuweza kushiriki kuipata semina hiyo iliyowekwa katika mfumo wa PDF kupitia email. Pia kwa kulipia semina hii moja kwa moja utashiriki semina nyingie zote 3 zilizobakia.

Siyo lazima uwe Whatsapp ndipo ujiunge na semina hizi, unaweza kujiunga hata kama unatumia Email peke yake kwani tunatuma pia kila kitu kupitia Email.

CHA KUFANYA, KAMA UNAHITAJI TU LAKINI !

Lipia shilingi elfu 10 kupitia namba zetu, 0765553030 au 0712202244 kisha tuma ujumbe wasap 0765553030 au sms ya kawaida usemao, “NITUMIE SEMINA YA KIWANDA CHA TOFALI”

Nitakutumia mara moja Mchanganuo mzima wa biashara hiyo ya tofali pamoja na Semina yote kama tulivyojifunza.

Lakini pia nitakutumia offa ya masomo na vitabu mbalimbali kama ifuatavyo; *(Offa hii maarufu ya vitu 13  bado kidogo sana itaisha muda wake)*

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.


HAPA CHINI NIMEWEKA MUHTASARI WA MPANGO WA BIASHARA HIYO YA TOFALI (KILUVYA QUALITY BRICKS)


1.0 MUHTASARI
Kiluvya Quality Bricks ni kampuni itakayozalisha na kuuza tofali za saruji pamoja na vifaa vingine mbalimbali vya ujenzi vilivyo na ubora wa hali ya juu kwa bei rafiki kwa mteja. Malengo yake makubwa ni pamoja na kufikisha wastani wa mauzo ya shilingi milioni 12 kwa mwezi, kuongeza idadi ya mashine 2 mwaka wa 3 pamoja na kutoa ajira ya kudumu kwa watu watatu. Wamiliki wa biashara ni Bwana Ahmed Yusuph   na Grayson Moris ambao kila mmoja atatoa kiasi cha shilingi milioni 6.5 kama kianzio.

Eneo la biashara lipo katka mtaa wa Kiluvya madukani wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani. Tutaanza na uzalishaji wa tofali na hali ya kifedha ikiimarika tutazalisha bidhaa nyinginezo kama vile, paving blocks, makalavati, nguzo na mifuniko ya majitaka. Soko letu tumeligawa katika makundi 2, Watu binafsi na Taasisi lakini kipaumbele chetu kikubwa ni katika kundi la watu binafsi kutokana na kufikika kwa urahisi na kwa gharama kidogo. Mahitaji makubwa ya tofali na vifaa vya ujenzi katika eneo la Kiluvya yanatokana na wakaazi wengi wa jiji la Dar es salaa kuhamia maeneo ya pembezoni hasa mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanzisha makazi. Sababu nyingine ni ujenzi wa barabara ya Morogoro.

Ingawaje sekta ya ujenzi imeonyesha kushuka kidogo mwaka huu toka asilimia 15.6 mwaka jana mpaka asilimia 13.2 lakini bado sekta hiyo imeendelea kuongoza katika kuchangia pato kuu la Taifa. Washindani wetu wakubwa waliopo ndani ya umbali wa kilometa 10 wapo wawiili ambao ni Kiluvya Traders na Bambam blocks & Bricks. Lakini washindani hao wana udhaifu katika bei, ubora, usimamizi, teknolojia na kiwango cha uzalishaji kwa siku.

Ili kuweza kutimiza mahitaji yote washindani wetu waliyoshindwa kuwatimizia wateja tutatumia mikakati mbalimbali ikiwemo, eneo letu la kimkakati, bei wateja wanayoimudu, kukuza jina letu sokoni pamoja na kujenga ukaribu na mafundi wajenzi. Uendeshaji wa shughuli za kila siku utasimamiwa na mwanzilishi mwenza Grayson Moris Jumatatu mpaka Jumamosi. Gharama ya kuzalisha tofali moja ni sh. 738 na kwa siku zinatarajiwa kuzalishwa tofali 400.

Viongozi wa kampuni watakuwa ni waanzilishi wenyewe lakini pia watashiriki moja kwa moja katika majukumu mengine ya kila siku. Wafanyakazi wa kudumu watakuwa 3 huku wengine wakiwa ni vibarua watakaolipwa kwa siku. Kiluvya Quality inakisia faida kwa mwaka kuwa ni shilingi milioni 20.6, Mauzo ya kurudisha gharama shilingi milioni 3 au tofali 3085 kwa mwezi na muda mradi utakaporudisha fedha zote za kuanzia ni miezi 7.  
…………………………..

Peter A. Tarimo
Mwandishi na mhamasishaji.

0 Response to "JE, ULIKOSA SEMINA YETU YA KWANZA YA VIWANDA MWEZI AGOSTI?"

Post a Comment