2020 UKIONA DALILI HIZI 5 BASI UJUE NI MUDA SAHIHI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO MWENYEWE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

2020 UKIONA DALILI HIZI 5 BASI UJUE NI MUDA SAHIHI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO MWENYEWE

MJASIRIAMALI WA BIASHARA YA DUKA LA VIPODOZI
Ni kauli maarufu na iliyozoeleka na watu wengi kwamba ili mtu aweze kuanzisha biashara yake mwenyewe hitaji kubwa ni mtu huyo kwanza kuwa na sifa zote za ujasiriamali. Kauli hii kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiwafanya wajasirimali wengi wachanga kujawa na hofu ya kuchukua hatua ya kuanzisha biashara zao na kuendelea kubakia kwenye ajira zinazowabana muda wote wa maisha yao au kuendelea kufanya shughuli zinazowawezesha kupata mlo wa siku tu ilimradi maisha yanasonga mbele.

SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.

Lakini tunaporudi katika uhalisia wa mambo, siyo rahisi kwa mtu anayetaka kuanzisha biashara aweze kuwa na sifa zote kamili za ujasiriamali. Ndio maana basi katika Makala hii nimejaribu kuziorodhesha dalili muhimu ambazo pindi uzionapo na wewe ni muajiriwa mahali, basi ni muda muafaka kwako wa kufikiria kuanzisha biashara yako mwenyewe na wala usianze tena kufikiria juu ya kutimiza vigezo vyote vya kuwa mjasiriamali bora ndio uanze. Utatimiza mbele kwa mbele

SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri mwenyewe?

Si lazima uachane na kazi yako ghafla hapana, unaweza kuanza kidogo kwa kufungua biashara ya ndoto yako lakini katika ngazi ya awali kabisa huku ukijpanga mdogomdogo(Start small but keep thinking big), mfano mzuri ni pale mtu anapoanzisha café ya kuuza maziwa, chai na vitafunwa kumbe yeye lengo lake kichwani ni kuja kumiliki mkahawa mkubwa kama wa Mc Donald’s. Si kama fedha za kufungua mkahawa anakuwa hana, ila anataka kwanza apate uzoefu wa biashara ya vyakula kabla hajajiingiza mzimamzima.

Kuna biashara za aina nyingi, nyingine ni za uwekezaji usiohitaji muda wako hata sekunde moja ukishawekeza mfano uwekezaji katika hisa, mifuko ya fedha nk, achilia mbali kwenye ardhi na majengo. Kwa hiyo hapa hamna “excuse” hata kidogo ikiwa unakumbana na dalili hizi nitakazokwenda kuzielezea hapo chini.

SOMA: Hatua 6 za uwekezaji fedha zako usipate hasara au kufeli.

Tena isitoshe basi suala la uwekezaji si lazima uache ajira yako ndipo uwekeze, unaweza ukaitumia nguvu hii ya ajabu matajiri wengi waliyowahi kuitumia kama inavyofafanua makala ya kipekee(exclusive report) tutakayojifunza leo Januari tarehe 11 usiku saa 3 kwenye Mastermind group la wasap la Michanuo-online isemayo, “AJABU LA 8 LA DUNIA: NGUVU YA KUSHANGAZA IWEZAYO KUMTAJIRISHA MTU BILA YA KUTOA JASHO” .

Kimsingi kabisa ni kwamba ajira siyo kitu kibaya hata kidogo kama watu wengi wanavyodhania, bali katika mzunguko wa maisha ya binadamu ajira inapaswa tu iwe ni daraja la kuvukia kuelekea katika biashara au uwekezaji binafsi(Uhuru wa kifedha).

SOMA: Ajira siyo laana, bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.

Katika maajabu hayo ya 8 ya dunia, nguvu kuu inayotajwa hutegemea sana vigezo au vitu vingine muhimu 3 na kimoja kati yake ni MUDA. Ndiyo maana katika somo hilo nakushauri kama wewe ni kijana jitahidi sana usilikose somo hilo kwani lina ujumbe mzito na muhimu mno kwako, sina maana wazee au wenye umri mkubwa haliwahusu hapana, bali vijana lina umuhimu wa kipekee zadi kwao somo hili adimu.

Baada ya hayo machache hebu tuzione dalili hizo kuu 5 ambazo kama mwanzoni mwa mwaka huu wa 2020 unaziona katika eneo lako la kazi/ajira, basi hujachelewa, chukua hatua kungali mapema.

1. Hakuna tena kupandishwa daraja wala promosheni.
Na hata kama kukikiwepo basi kunakuzidishia tu msongo wa mawazo badala ya kukupa faraja. Usikubali katika ajira yako uishi na msongo wa mawazo (stress) au karaha, labda tu iwe wewe ndiye mtu unayelipwa pesa nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote katika kampuni/biashara hiyo.

SOMA: Stress za pesa zinavyoweza kuzima kabisa ndoto za mtu na hatua za kuchukua haraka.

2. Sasa unao uwezo wa kufanya vitu kwa weledi zaidi.
Ukiona dalili kwamba uwezo wa utendaji wako wa kazi unazidi hata ule wa bosi wako, basi fahamu ni muda muafaka kwako wa kuanzisha biashara yako mwenyewe  kwani bosi wako au mabosi wako kamwe hawataweza kukupatia nafasi ya kuonyesha unawazidi kiutendaji.

3. Una mawazo mazuri.
Unajaribu kutoa mawazo mazuri jinsi ya kuboresha biashara lakini kwa bahati mbaya, si bosi wako wala meneja anayehangaika kulitambua hilo. Watu pekee wanaotamba juhudi zako wanabakia kuwa ni wale wateja unaowahudumia tu.

SOMA: Unapoajiri au kuajiriwa zingatia umuhimu wa kujua ni nini unachokitaka.

4. Unahisi kuchoshwa na mwenye kukosa hamasa.
Ujuzi na taaluma yako hauvitumii ipasavyo na wala havithaminiwi tena kama inavyostahili na mabosi wako. Unaona kabisa uzoefu wako unapotea bure na wewe huna tofauti na wale wafanyakazi wanaofanya mazoezi bure(internship). Uonapo dalili hii, usiendelee kupoteza muda, ni wakati wako muafaka sasa na wewe kwenda kuitwa Mkurugenzi(CEO)

5. Baada ya kunyimwa promosheni na maslahi uliyostahili.
Sasa umehamishiwa ofisi nyingine nje kabisa ya mji au iliyopo mkoa wa mbali. Hapa huna chaguo jingine zaidi ya kuanzisha Biashara/Kampuni yako mwenyewe

mwisho
……………………………………………….


TAARIFA MUHIMU SANA!

1. MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP 2020
Napenda kukufahamisha mpenzi msomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali kwamba Group lako la MICHANGANUO-ONLINE kwa mwaka 2020 ndio linaanza rasmi leo tarehe 11 Januari, saa 3 usiku baada ya kazi ya kusajili wanachama upya.

Somo la leo saa 3 usiku linasema hivi;
“AJABU LA 8 LA DUNIA: NGUVU YA KUSHANGAZA IWEZAYO KUMTAJIRISHA MTU BILA YA KUTOA JASHO”

Utaratibu rasmi wa ratiba zetu utatolewa kwenye group lakini kwa ujumla tu ni kwamba mwaka huu kaulimbiu yetu kuu bado ni ileile ya Viwanda ila tumebadili  kidogo maneno na kuiita, “THE 2020 TANZANIA INDUSTRIAL REVOLUTION IS POSSIBLE, PLAY YOUR PART” Mwenyezi Mungu akipenda tunatarajia 2020 hii tufanye mambo makubwa sana katika sekta hii ya viwanda vidogo.

Tutaaanza kwanza na kumalizia kiporo cha michanganuo ya viwanda bunifu vitatu(3) vya mwaka jana ambayo hatukuweza kuimalizia kutokana na muda mwingi kuishia katika maandalizi ya kiwanda changu nilichotarajia kuwaonyesha lakini kwa bahati mbaya muda tuliokadiria haukutosha, kazi likuwa nzito.

Kisha baada ya hapo tutakuwa na uzinduzi wa hicho kiwanda chenyewe ambacho kama nilivyoahidi tangu 2019 kitakuwa ni cha ubunifu wa kipekee sana na nitawaonyesha wadau kwa njia ya picha za video jinsi kilivyoundwa A – Z, na ni kwa namna gani kinavyofanya kazi. Mpaka sasa hivi kimeshaanza uzalishaji wa awali na bidhaa zipo sokoni.

Nikuibie tu siri kidogo, ni kwamba kiwanda hicho kinatumia mtaji mdogo sana wa pesa, sehemu kubwa ni nguvu na utaalamu binafsi tu vinavyohitajika. Ni teknolojia ambayo hapa Tanzania sijapata kuiona na hata katika baadhi ya nchi zingine ipo lakini haijarahisishwa kama tulivyofanya sisi. Kwahiyo ni kitu cha kipekee sana hapa Tanzania.

2. SEMINA YA KUANDAA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA CHA UNGA SUPER WA DONA TAREHE 20/01/2020
Semina hii pamoja na nyingine za viwanda tofauti 2 zilikuwa zifanyike toka mwaka jana 2019 lakini hatukuweza kutekeleza na tarehe 20/01/2020 ndiyo siku tutakayofanya semina hii ndani ya group letu halafu semina nyingine zitafuata siku zijazo.

JINSI YA KUJIUNGA NA GROUP
Ili mtu uweze kujiunga na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE na kufaidi masomo ya fedha kila siku pamoja na semina hizi za mara kwa mara za viwanda bunifu unatakiwa kulipa ada ya mwaka mzima ambayo ni shilingi 10,000/=(Elfu kumi tu)

Namba zetu unazoweza kulipia ni; 0765553030  au  0712202244  na jina ni Peter Augustino Tarimo. Ukishalipa nitumie ujumbe wa watsap au sms kwenye 0765553030 usemao, NIUNGE NA MASTERMIND GROUP 2020. Nitakuunganisha ndani ya dk. 3 tu pamoja na kukutumia offa ya masomo yote yaliyopita bure.

Wahi pia na offa ya kupata masomo, semina na michanganuo yote iliyopia  2019 kabla ya tarehe 15 kupita. Tarehe 15 ikipita ofa hii itakuwa imeisha muda wake na utaweza kujiunga na group na kupata masomo na semina za 2020 tu peke yake.

Aidha nafasi za group zilizobakia pia siyo nyingi, hivyo ni vizuri kuwahi ili zisijekujaa ukakosa nafasi yako 2020 na mambo yote mazuri tuliyoandaa.

ASANTE NA KARIBU SANA KUNDINI

Mwanaviwanda wako/Industrialist
PETER AUGUSTINO TARIMO

WATSAP: 0765553030
SIMU: 0712202244  

0 Response to "2020 UKIONA DALILI HIZI 5 BASI UJUE NI MUDA SAHIHI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO MWENYEWE"

Post a Comment