HATUA 6 ZA UWEKEZAJI FEDHA ZAKO USIPATE HASARA AU KUFELI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATUA 6 ZA UWEKEZAJI FEDHA ZAKO USIPATE HASARA AU KUFELI



Kwanza kabisa kabla hatujaendelea mbele ni vizuri tukafahamu tofauti iliyopo kati ya kufanya biashara na kuwekeza kwani ni vitu vinavyoonekana kufanana sana. Uwekezaji ni nini?  Uwekezaji maana yake ni kile kitendo cha kuweka fedha kwenye mradi ambao hushughuliki nao moja kwa moja ukiwa na malengo ya muda mrefu wakati kufanya biashara unaweka fedha zako katika mradi unaohitaji uwepo wako moja kwa moja ukiwa na malengo ya muda mfupi. Malengo ya uwekezaji na kufanya biashara yote yanafanana ambayo ni kupata faida, mali zaidi au utajiri.

SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

Uwekezaji wa miti kwa mfano unaweza kuona huchukua mpaka miaka kumi na kitu, tofauti na uwekezaji mtandaoni au uwekezaji wa hisa ambao unaweza ukauza hisa zako hata ndani ya wiki moja. Hivyo aina moja ya uwekezaji inaweza katika mazingira fulani ikawa ni biashara lakini katika mazingira mengineyo ikawa ni uwekezaji kulingana na muda, jinsi utakavyoshughulika nao pamoja na malengo yako katika mradi husika.

SOMA: Jinsi wanaochukua hatari kubwa kwenye biashara ya uwekezaji kwenye magari wanavyofanikiwa haraka.

Uwekezaji Tanzania unachukua sura mpya sasa tokea mageuzi makubwa ya kiuchumi kutoka uchumi wa soko hodhi kuingia katika uchumi wa soko huria, watu wengi zaidi wamejiingiza kwenye uwekezaji tofauti na miaka kadhaa iliyopita. Kwa mfano zamani kulikuwa hamna soko la hisa Dar es salaam DSE lakini sas hivi lipo, watu walikuwa hawawekezi kwenye majengo na badala yake ni serikali ndiyo iliyokuwa na jukumu hilo.

Kwa kawaida watu wengi huanzia kwenye biashara za kawaida tu kabla hawajachukua uamuzi wa kuingia kwenye miradi ya uwekezaji wa fedha zao. Siyo kwenye biashara ya uwekezaji katika soko la hisa, uwekezaji wa pamoja UTT au uwekezaji katika ardhi na majengo tu peke yale bali ni karibu katika kila biashara na uwekezaji, mjasiriamali anapaswa kuwa na umakini wa hali ya juu sana anapoamua kutumbukiza fedha zake huko, Kwanini?

Ni kutokana na sababu kwamba, tunapojiingiza kwenye uwekezaji/biashara tunashughulika na pesa, isitoshe pesa zenyewe ni zile tulizozipata kwa shida pengine baada ya kujinyima, tukifunga mikanda kwa kipindi kirefu. Hatuwezi kuwa na fedha za kupoteza hivihivi tu hata ikiwa siyo kwa kufanya anasa au vitu visivyokuwa na maana bali hata kuwekeza bila ya kuchukua tahadhari nako ni kupoteza fedha kizembe.

SOMA: Mbinu za kufanikiwa kufikia malengo katika uwekezaji wowote utakaoufanya.

Tunawekeza fedha zetu ili kuzifanya zikue, ziongezeke mwishowe tutajirike na wala siyo zipotee. Kwa hiyo kabla hujajiingiza kwenye uwekezaji ni mbinu zipi uzitumie ili kupunguza hatari ya kutokomea kwa fedha zako? Mbinu ya kwanza kabisa tena rahisi itakayokusaidia kupunguza hatari za uwekezaji ni KUJIFUNZA KWANZA KUSHUGHULIKA NA FEDHA. Hakuna asiyefahamu pesa ni kitu gani lakini mara nyigi linapokuja suala la biashara au uwekezaji katika miradi wengi maarifa yao ni karibu na sifuri. Jinsi ya kusimamia fedha ni somo kila mjasiriamali anatakiwa kulifahamu hata ikiwa hakuweza kupata elimu kubwa ya darasani. Na elimu ya namna hiyo mtu anaweza akaipata kupitia njia nyingi, mojawapo ikiwa ni kwa kujiunga na magroup kama MICHANGANUO-ONLINE, kusoma vitabu, semina, makongamano nk.

Hatua za usimamizi bora wa fedha kabla mtu hajafikia hatua yenyewe ya kuwekeza ni lazima apitie hatua muhimu 6, hatua hizo ni za matayarisho. Kwanini ni lazima kupitia hatua hizo za matayarisho hasa kwa yule anayeanza? Matayarisho yanahitajika kwa sababu karibu miradi na biashara zote zile zinazolipa kwa kiasi kikubwa unakuta pia ni lazima ziwe na hatari kubwa pia ya kuanguka/kufeli. Ikiwa basi mjasiriamali ataamua kujiingiza kwenye hatari hizo ni lazima pia afahamu ni kwa jinsi gani anaweza akajinasua huko. Kwahiyo matayarisho ni muhimu kama njia ya kuchukua tahadhari.

SOMA: Baada ya kufanya utafiti sasa naanza kufanya biashara  yangu ya ufugaji wa kuku wa mayai ya kienyeji.

Kama tulivyoona kwenye somo letu lililopita siyo miradi yote ina hatari kubwa lakini tunazungumzia ile iliyokuwa na hatari kubwa zaidi kwasababu pia ndiyo iliyo na uwezekano mkubwa wa kulipa vizuri zaidi. Sasa hebu twende kukaone hatua zenyewe ni zipi tukianza na hii hapa;

..............................................

Ndugu msomaji mfululizo wa masomo haya 30 unaendelea ndani ya group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE. Kuweza kupata somo hili kwa ukamilifu unaweza kujiunga na group hilo kwa kulipia kiingilio ambacho ni sh. elfu 10. Baada ya malipo utapokea masomo mengine yote yaliyowahi kutolewa kwa mwaka mzima wa 2018 na utaendelea kuwa mwanachama kwa mwaka wote wa 2019.

Namba za kulipia ni hizi hapa; 0765553030  au  0712202244 ambazo jina hutokea, Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma ujumbe : "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO"

Wasap ni 0765553030



0 Response to "HATUA 6 ZA UWEKEZAJI FEDHA ZAKO USIPATE HASARA AU KUFELI"

Post a Comment