MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KWENYE HALI NGUMU KIPESA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KWENYE HALI NGUMU KIPESA


Nchini Tanzania sasa hivi na Dunia kwa ujumla tunaweza tukasema kwamba hali ya kiuchumi ni ngumu sana ingawa wapo baadhi ya watu ambao bado makali hayo hawajaanza kuyahisi. Hali hiyo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na Janga kubwa la Corona/Covid 19 ingawa hata hivyo kabla ya janga hili kupiga hodi bado kulikuwa na malalamiko ya hapa na pale juu ya hali ngumu ya upatikanaji wa pesa kwa wafanyabiashara wadogo kwa wakubwa. 

Wengi wa wale waliokuwa wakilalamika hata kabla ya janga la Covid 19 walikuwa wakihusianisha hali hiyo na mabadiliko ya sera mbalimbali za serikali ambayo pia yaliletwa na mabadiliko ya kiutawala katika kipindi cha miaka zaidi ya 4 iliyopita.

Kibiashara tunaweza tukasema kwamba mabadiliko hayo yaliathiri mazingira ya biashara na hivyo biashara nyingi kuonekana hazikuwa zikienda vizuri, lakini pengine lilikuwa ni suala la muda tu na mambo yangelitengemaa yenyewe kadiri muda ambavyo nao ungezidi kwenda na watu kuzidi kuendana na mazingira hayo mapya. Hata hivyo janga la Corona ni kama limekuja kuongezea chumvi kwenye kidonda kibichi kwani limezidisha hali kuzidi kuwa tete kiuchumi kwa ujumla wake.

Iwe kuna hali ngumu kiuchumi kwa kutokana na hali yeyote ile na siyo janga la Covid 19 tu, kwa mtu mmoja mmoja au kwa taasisi na makampuni, zipo mbinu na mikakati mitano (5) ya uhakika ambayo mfanyabiashara yeyote yule anaweza akaitumia ili kupunguza makali ya hali kama hiyo, na katika somo tunalokwenda kujifunza leo tarehe 9/5/2020 kwenye magroup yetu ya masomo ya kila siku whatsap ya MICHANGANUO-ONLINE mbinu zote hizo 5 zitajadiliwa moja baada ya nyingine hivyo kama hukuwa umejiunga basi huu ndio wakati muafaka wa kujiunga ili unufaike na somo hili na mengine pia yanayotolewa kila siku kwa kiingilio cha shilingi elfu 10 tu mwaka wote wa 2020.

Programu ya masomo ya Mtiririko wa fedha na Michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa ambayo ndiyo mada zetu kuu ni ya mwaka huu mzima wa 2020 na unapojiunga tu tunakupatia access ya masomo mengine yote ambayo ulichelewa kujifunza.

Kujiunga, unalipia kiingilio chako sh. Elfu 10 kupitia namba zetu za simu ambazo ni 0712202244  au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo. 

Kisha tuma namba unayotumia wasap au anuani yako ya email katika meseji ikiambatana na ujumbe usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE NA OFFA YA VITU 7”  na sisi mara moja tutakuunganisha kwenye group muda huohuo ikiwa ni pamoja na kukutumia vitu mbalimbali vifuatavyo.

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa kiswahili

2.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

3.  Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji unga wa dona(USADO Milling) )-kwa kiswahili

4.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)-kwa kiswahili

5.  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

6.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingereza


7.  Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwa biashara yako-kwa kiswahili

Baada ya hapo utakuwa ukipokea masomo ya kila siku saa 3 mpaka saa 4 usiku pamoja na semina za michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa mara kwa mara mpaka program yetu imalizike kisha tutaanza nyingine. Wakati huo wote hutachajiwa kiasi kingine chochote tena cha fedha.

Siku ya kesho tarehe 10/5/2020 ndani ya group tutakuwana na somo la kuchanganua hatua kwa hatua mpango wa biashara ya Stationery(Steshenari). Usikose.


0 Response to "MBINU NA MIKAKATI YA KUIKWAMUA BIASHARA YAKO KWENYE HALI NGUMU KIPESA"

Post a Comment