BIASHARA HII WATU WENGI HUIDHARAU LAKINI INA FAIDA KUBWA NA NZURI,MTAJI LAKI 1 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA HII WATU WENGI HUIDHARAU LAKINI INA FAIDA KUBWA NA NZURI,MTAJI LAKI 1

BIASHARA YENYE FAIDA KUBWA NA NZURI
Kwenye mfululizo wetu au kipengele  cha biashara zilizosahaulika au kwa jina jingine biashara ndogo ndogo zisizopewa kipaumbele kikubwa na watu kumbe zina uwezo wa kuzalisha faida kubwa na nzuri, katika pita pita yangu mitaani wiki hii nilikutana na habari za biashara hii ya makopo yaliyotupwa ambapo kwa kweli niliwahi kuiandikia makala nyingine nikasema, Si kila muokota makopo ni kichaa, wapo wanaotengeneza noti kushinda hata karani wa benki. Ila hii ya leo ina tofauti kidogo.

Unapotaja aina za biashara ndogondogo zinazotengeneza faida nono kama wewe ni mtu unayezifahamu fursa huwezi ukaacha hata kidogo kuorodhesha biashara ya kununua na kuuza kwa jumla vitu chakavu vinavyopatikana katika mazingira na ambavyo huchafua mazingira ikiwa vitaachwa vitapakae ovyo ovyo, lakini kwa kuvikusanya na kuvirudisha kiwandani unakuwa unaboresha mazingira ili yaweze kuwa safi zaidi.


Biashara hii licha ya kuwa ni nzuri kifaida lakini pia ni halali kwani serikali inaunga mkono kikamilifu watu wanaohakikisha mazingira yanakuwa safi na kubakia katika hali yake ya uasili. Hebu fikiria ni kitu gani kingelitokea katika mazingira ya nchi na Dunia kwa ujumla kama kusingelikuwa na kurudishwa viwandani vitu chakavu. Kuna chuma, plastiki, mabati na vitu chungu nzima vinavyotoka viwandani ambavyo vingesababisha bahari na nchi kavu kugubikwa na takataka za kutisha ambazo siyo kero tu kwa binadamu bali hatari kwa afya za wanyama na viumbe hai vinginevyo vyote ikiwemo mimea samaki na hata wadudu. Tanzania inapoelekea katika uchumi wa viwanda vitu chakavu kama plastic vitakuwa ni dili kubwa wakati ujao

Si nia yangu leo kuzungumzia takataka zote kwa ujumla, japo karibu kila takataka duniani ni fursa mojawapo ya biashara. Wakati wewe ukilia ni uchafu, wenzako wanazigeuza kuwa pesa kwa namna moja ama nyingine. Kama ilivyokuwa ada mimi huwa napenda kuibua fursa mitaani ambazo watu wengi hawajazishitukia lakini wale wachache waliokwishazigundua wanapiga hela kimya kimya utadhani wanamfukuza mwizi aliyebeba fuko la noti vile.

SOMA: Biashara ndogo rahisi kwa wajasiriamali zinazoendana na wakati tulio nao.

JINSI BIASHARA YA KUNUNUA NA KUUZA CHUPA CHAKAVU ZA PLASTIKI KWA JUMLA ILIVYO NA FAIDA NUSU KWA NUSU

Nilikutana na dada mmoja anayefanya biashara ya kuokota chupa chakavu za plastiki na kisha kwenda kuziuza, kwa maana nyingine dada huyu yeye hufanya biashara ya chupa chakavu kwa rejareja. Baada ya kuziokota maeneo mbalimbali yeye huzipeleka kuuza kwa wafanyabiashara wanaonunua kwa jumla na kisha kupeleka kuuza kiwandani. Katika mazungumzo yetu dada huyu alikuwa akinisisitizia juu ya faida kubwa wanayopata wafanyabiashara wale wanaonunua na kuuza kiwandani kwa jumla pamoja na urahisi uliopo katika biashara hiyo. Alikuwa akijaribu kunishawishi kama ninao mtaji niingie katika biashara ile au tuingie hata ubia.

“Kaka biashara ya kununua  makopo na kuyauza kiwandani nimeshaichunguza kwa muda mrefu ina faida kwani unapata kiasi mara mbili cha bei unayonunulia unapokwenda kuwauzia kiwandani, isitoshe wewe huna gharama kubwa kwani wao wenyewe kiwanda ndiyo wanaotuma watu wao na usafiri kuja kuchukua mzigo baada ya kufikisha tani kadhaa.” Alinisimulia dada huyu anayependa kuvaa kama mwanaume awapo kazini, huvaa kofia pama, Tshirt na suruali ya jeans


“Ukiwa na mtaji kama laki moja na elfu 90 peke yake unatosha kwani utanunua mzani wa mtumba ambao hauwezi kuzidi shilingi elfu arobaini (40), na mtaji wenyewe kwa ajili ya kununulia mzigo shilingi laki moja na nusu tu ambao utanunua tani moja ya makopo. Kuhusiana na eneo, halina shida kubwa, unaweza ukatafuta eneo lolote lile la wazi kwani serikali huwa haihangaiki sana na kuondoa biashara za muda mfupi, makopo ya plastiki ukishafikisha tani moja au mbili wanakuja kuchukua hayakai muda mrefu.

Na hata ukiamua kununulia eneo hatarishi kama vile maeneo ya mabondeni, unaweza ilimradi tu uhakikishe siyo msimu wa mvua na pia usalama wa makopo yenyewe kwani wale waokotaji makopo wenyewe wanaweza kuja usiku au muda wewe haupo wakayaiba na kuja kukuuzia tena kesho yake.” Alimalizia dada huyo aliyeonekana kuijua vizuri biashara hiyo lakini anakosa mtaji wa kuweza kuianza.


Kwa mujibu wa maelezo ya dada huyu, kilo moja ya makopo chakavu ya plastiki wanauza shilingi 150/= kwa plastiki laini na plastiki ngumu na PVC hufika mpaka shilingi 350/= kwa wanunuzi wa jumla wanaonunua kwa ajili ya kwenda kuuza kiwandani. Bei wanayokwenda kuuza kiwandani anasema hufika mpaka kiasi mara mbili ya bei wanayonunulia. Hii ni kusema kwamba ukinunua tani moja ya makopo kwa shilingi laki moja na nusu utaenda kupata shilingi laki tatu kiwandani, ukiondoa gharama za manunuzi na nyinginezo unabakiwa na shilingi karibu laki moja na kitu hivi. Kwa hiyo ni biashara iliyokuwa na faida nzuri na isiyokuwa na gharama nyingi wala changamoto za kutisha.

………………………………………………………………….

Mpenzi msomaji mwaka huu ndio unamalizika, hivyo katika kampeni yetu tuliyoianza pamoja mwanzoni mwa mwaka huu iliyoitwa, MAKE YOURSELF GREAT AGAIN AU JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA, tuliahidiana sote kwamba ifikapo kipindi kama hiki kila mmoja wetu ahakikishe anapima ni kwa kiasi gani ameweza kutimiza malengo yake aliyojiwekea hususani yale ya kiuchumi na maisha kwa ujumla. Sisi kama Self Help Books Publishers tulijiwekea lengo la kumalizia kutafsiri kitabu cha Think & Grow Rich katika lugha ya kiswahili na tunashukuru lengo hilo tumeshalikamilisha, kilichobakia sasa ni kumalizia tu kukichapisha katika blogu yenu hii ya jifunzeujasiriamali kazi inayoendelea.

Je, na wewe ni lengo lipi umeweza kulitimiza? Si lazima uliweke wazi hapa unaweza kujijibu mwenyewe tu na malengo siyo lazima iwe kila ulichoazimia kufanya basi umetimiza kila kitu hapana, unapoweka malengo kuna malengo mahsusi na malengo yale madogomadogo(rejea kitabu cha Mifereji 7ya pesa uk. wa 16.), hivyo angalia yale malengo yako makubwa ni lipi uliloweza kutimiza kikamilifu?


Kuna mambo mengi na makubwa tuliyokuandalia mwezi huu wa Disemba mwishoni mwa mwaka huu wa 2017 kuelekea Januari mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2018 usikae mbali, lakini juu ya kila kitu nakusihi sana kama ulikuwa hujasoma kitabu mahsusi kwa ajili ya mtu anayetaka kujiwekea malengo kikamilifu, kitabu kiitwacho, MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA basi utafute kitabu hicho kwani ni kizuri mno hasa nyakati hizi za mwanzo wa mwaka watu wanapoweka malengo mbalimbali ya maisha.

malengo yako 2018

Ukikisoma huwezi hata siku moja ukaja kujuta pale mwaka unapoisha, eti hujatimiza malengo uliyojiwekea. Kitabu hiki ni shilingi elfu 3 tu softcopy na unatumiwa kwa njia ya E-mail unadownload kwenye simu au kompyuta yako. Tuma pesa katika namba 0712202244  au 0765553030 jina: Peter Augustino Tarimo,  pamoja na anuani yako ya email kwa njia ya meseji, utatumiwa kitabu mara moja muda huohuo. Unaweza pia kuwasiliana nami kupitia ujumbe wa Whatsapp kwa namba 0765553030

ASANTE SANA
Peter A. Tarimo

self help books Tanzania  

0 Response to "BIASHARA HII WATU WENGI HUIDHARAU LAKINI INA FAIDA KUBWA NA NZURI,MTAJI LAKI 1"

Post a Comment