NJIA 5 ZA KUKUZA MAPATO YA BIASHARA NDOGO KWENDA HATUA YA JUU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NJIA 5 ZA KUKUZA MAPATO YA BIASHARA NDOGO KWENDA HATUA YA JUU

Mtu kuanzisha na kuendesha biashara ndogo toka mwanzo ni jukumu zito na linalogharimu kutokana na majukumu mengi yanayokukabili wewe mwenyewe kama vile, kufikiria wazo la biashara itakayofaa, kutafuta mtaji wa kuanza biashara, kuajiri wafanyakazi au mfanyakazi, kumfundisha mfanyakazi/wafanyakazi nk. 

Mambo hayo yote yanahitaji uangalizi wako kwa wakati mmoja. Na tena isitoshe basi mambo hayo huhitaji muda na pesa, rasilimali ambazo zote huwa adimu mno katika hatua za awali kabisa za biashara inayoanza moja. Hata hivyo mbinu au njia zifuatazo zina uwezo wa kumuwezesha mtu yeyote anayejikuta katika hatua za kuanzisha biashara kuweza kujibana katika kila rasilimali aliyokuwa nayo kusudi mambo yaweze kwenda vizuri.

1. Anza na kile ulichokuwa nacho kwanza.
Kabla hujaanza kufikiria utumie pesa kidogo ulizokuwa nazo kwa ajili ya vitu mbalimbali vya kuanzia mfano sehemu ya kufanyia biashara au chumba, fikiria njia zingine mbadala kwa mfano, kutumia chumba cha ziada nyumbani au hata chumba chako mwenyewe cha kulala, sebule nk. badala ya kupanga chumba cha gharama kubwa.

Hata ikibidi ni lazima upange chumba kwa ajili ya biashara hiyo, basi kipambe kwa kutumia fenicha za ziada za nyumbani na hata vitu kama kompyuta au simu tumia kwanza vile vyakwako binafsi. Elekeza nguvu zako zaidi katika mauzo badala ya muonekano wa ofisi na fenicha, vitu vinavyotakiwa kuja baadae.

SOMA: Soma vitabu hivi vya maisha na mafanikio. 

2. Jiepushe na utititiri wa njia za mawasiliano.
Mara nyingi biashara inayoanza huwa na mtu mmoja au hata wakiongezeka sana labda ni wawili, sasa kitendo cha mtu mmoja kuanza mara kusikiliza simu iliyopigwa, mara kuangalia meseji ya simu iliyoingia, akigeuka huku email imeingia, huku simu imeita tena, facebook, twitter, instagram, whatsapp nk. vyoote hivyo vitakupotezea muda wako mwingi na hata pesa kwa ajili ya mabando ya kila mara. Badala yake waelekeze wateja wako katika jukwaa moja tu la mawasiliano au mawili na utaokoa muda mwingi na fedha.

3. Chukua wafanyakazi wa muda badala ya wale wa kudumu.
Unapoona majukumu yamekuwa mengi na unahitaji mtu wa kukusaidia, tafuta mtu mwenye utaalamu husika lakini kwa mkataba wa muda mfupi au kazi fulani tu, na akishaimaliza basi unamlipa mnaachana, badala ya kuajiri mfanyakazi wa kudumu ambaye ni gharama kubwa kuwa naye kila mwezi.

4. Nunua bidhaa/malighafi au vifaa vya ofisi kwa bei ya jumla.
Kitu chochote kile katika biashara yako unachojua utakuja kuhitaji kukitumia mara kwa mara kwa mfano hata vitu kama kalamu, karatasi nk. vinunue kwa bei ya jumla kusudi kupunguza gharama utakayokuja kulipa ukinunua kimoja kimoja.

5. Tumia teknolojia ya kisasa kama vile, intaneti, mashine za kielectroniki za risiti na simu za kisasa kuokoa gharama za matumzi ya makaratasi mengi. Katika matumizi ya teknolojia pia hakikisha vitu kama baadhi ya programu ‘software’, unatumia zile zisizokuwa za gharama kubwa au zinazopatikana bure(free) mitandaoni.

SOMA: Siri 10 za utajiri wa Aliko Dangote, tajiri namba 1 Afrika

Na huo ndio mwisho wa makala yetu hii ya leo inayohusu jinsi ya kuanza biashara, au uanzishaji wa biashara mpya toka mwanzo(Startups). Kwa makala zaidi juu ya kipengele hicho angalia katika makundi ya makala pale pembeni mwa hii blog(tags) au chini(lebels) yenye jina “Kuanzisha biashara”
  
………………………………………………………………..


Ukihitaji Huduma zetu mbalimbali, bonyeza maandishi hapo chini kupata maelezo zaidi.










0 Response to "NJIA 5 ZA KUKUZA MAPATO YA BIASHARA NDOGO KWENDA HATUA YA JUU"

Post a Comment