JE WAJUA UNAWEZA KUMILIKI KIWANJA AU NYUMBA BILA KUTOA SENTI 5 MFUKONI? SOMA KITABU CHA DOLA MILIONI 5 UJUE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE WAJUA UNAWEZA KUMILIKI KIWANJA AU NYUMBA BILA KUTOA SENTI 5 MFUKONI? SOMA KITABU CHA DOLA MILIONI 5 UJUE

VITABU VYA MAFANIKIO

Katika safu yetu ya vitabu vya mafanikio 300 vilivyowahi kusomwa zaidi duniani nakala maelfu kwa melfu, leo tutakitazama kitabu kimoja  kilichoandikwa  na mwandishi Stefan Aarnio kiitwacho THE FIVE MILLION DOLLAR BOOK(Kitabu cha dola milioni tano). Kitabu hiki kinazungumzia jinsi ambavyo mtu unaweza ukatumia WATU, FEDHA na FURSA(dili) katika kufanikisha biashara ya ardhi na majengo(real estate wealth) hata kama hauna kitu chochote kile mifukoni.


Stefan anasema anawashangaa sana wawekezaji katika ardhi & majengo wanaochipukia wanavyozitumia fedha zao. Mara nyingi wawekezaji hao vijana ni wenye umri kati ya miaka 30 na 40 waliochoshwa na ajira zao lakini wanaotengeneza kipato cha wastani kilekile kisichobadilika.


Kwa kuwa wanakuwa na ajira ya uhakika watu hawa wana uwezo wa kupata mikopo kwa urahisi kutoka mabenki na taasisi mbalimbali za kifedha kwa ajili ya kukamilisha shughuli yeyote ile ya kiuchumi. Wawekezaji hawa wanakuwa wamekwisha choka na ajira za kukimbizana(rat race) na wako tayari kujiingiza katika biashara za uwekezaji katika majengo na ardhi kwa kutumia fedha zao wenyewe.

Kitu cha kusikitisha ni kwamba, aina hii ya wawekezaji wapya wamekuwa kwenye ajira tangia wakiwa na umri wa miaka 18 mpaka kufikia hatua hii kifedha na sasa wapo katika miaka yao ya 30  wakiwa tayari kuanza uwekezaji. Wawekezaji hawa wamezowea kufanya vitu kwa njia ya polepole ilioyowachukua miongo kadhaa kufikia pale walipo sasa kiuchumi. Muda ndiyo fedha ya kweli pekee maishani na ili kufanya mambo haraka, ni sharti tukubali kuelimika. Elimu ndipo mahali utajiri wote hutokea kwa sababu utajiri wote chanzo chake ni akili.


Haijalishi tumejiandaa kiasi gani au tulianza na kiasi gani cha fedha, ukweli wa mambo ni kwamba katika biashara au uwekezaji kwenye ardhi na majengo(real estate) mara nyingi tunaishiwa fedha njiani. Bila kujali ni kiasi gani cha fedha au mkopo tuliokuwa nacho mara nyingi kiasi hicho hufungwa kwenye mradi na mwishowe tunajikuta fedha zimekatika. Hili humtokea kila mwekezaji, uwe Donald Trump au Warren Buffet. Mara nyingi kuna hatua ambayo mwekezaji ni lazima atoke aende kutafuta mtaji wa kuendelea kuwekeza.

Stefan anaendelea kusema kwamba alianza kuwekeza akiwa na  umri wa miaka 22 na faida kubwa zaidi aliyoipata kwa kuwekeza akiwa na umri mdogo kiasi hicho ni kwamba hakuwa kabisa na fedha taslimu, wala mkopo, wala kuaminika alipoanza. Ilimbidi ajifunze kupata fedha, kusimamia kiasi chake kidogo cha mkopo na kuongeza zaidi kuaminika kwake. Ilimbidi ajifunze mbinu za kucheza mchezo wa “FEDHA, WATU na FURSA” pasipokuwa na fedha taslimu mfukoni tangia siku ya kwanza kabisa kwa kuwa alianza biashara akiwa hana kitu.


Alikuwa kijana ‘mtundu’ aliyepata semina ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo yenye thamani ya dolla elfu mbili na kutaka kuifanya ndoto yake kuwa kweli. Anasema shughuli zile za uwekezaji hazikunza mara moja mpaka kwanza alipojifunza sheria za kutengeneza madili(fursa) na kutafuta fedha za mtaji.

Sheria hizi zilimwezesha kutafuta fedha/mtaji kwa ajili ya fursa/mikataba(deals) zake zote isipokuwa mktaba wa kwanza peke yake ambao aliwekeza kiasi kidogo cha fedha kama dola 1200 hivi. Kwasababu alifahamu misingi ya FEDHA, WATU NA FURSA, hajawahi tena kutoa fedha  zake mfukoni kununulia biashara au ardhi na majengo tokea hapo.


Wawekezaji wengi hudhani kwamba ‘fedha ni mfalme’ na huogopa kutafuta fedha kwa ajili ya mikataba(deals). Ukweli wa mambo ni kwamba fedha ni ‘takataka’, kila mtu anazo na ni bidhaa rahisi isiyokuwa na thamani kama utaitumia pasipo akili. Fedh ni kigeugeu na ni rahisi kupatikana ikiwa tutaelewa kanuni chache muhimu za pesa.

SEHEMU KUU 3 UNAPOTAKA KUFANYA MKATABA(DEAL)
Kuna sehemu kuu 3 wakati unapotaka kuweka sawa mpango wa kupata fedha unazohitaji nazo ni hizi hapa;

1.FEDHA=Fedha zinahitajika kuanzishia biashara au kununulia nyumba/ardhi
2. WATU=Timu itakayoendesha biashara au kusimamia rasilimali
3. FURSA/MPANGO/BIASHARA(DILI)= Ni biashara au asseti yenyewe

Wawekezaji wengi wachanga hwaelewi hizi sehemu za msingi tatu katika uwekezaji kwenye ardhi na majengo na hupoteza muda mwingi wakijaribu kutafuta pesa kupitia njia zisizokuwa sahihi. Kwa kufanya hivyo huharibu kuaminika kwao na kuonekana kama wajinga katika mitandao ya wawekezaji wakubwa.

NI VITU 3 MUHIMU UNAPOANZISHA BIASHARA YA AINA YEYOTE ILE IKIWEMO HII YA ARDHI NA MAJENGO

Uimuuliza mtu yeyote swali hili atakujibu mara moja kuwa jibu ni PESA. Ni kweli asilimia 100% kuwa pesa zinahitajika unapotaka kuanzisha biashara eyote ile hata iwe ni ya kuuza juisi stendi au ya kujenga magorofa. Lakini Stefan anaposema alianzisha bishara yake bila kuwa na pesa anamaanisha kwamba alianzisha biashara yake kwa kutumia fedha za watu wengine(wawekezaji).


Pesa peke yake miongoni mwa viungo vingine 2 haina maana ikiwa hakuna sehemu nyingine 2, WATU na BIASHARA/FURSA(Deal). Pesa zipo nyingi kila mahali na zina tabia ya kutafuta mahali salama zinapoweza kuwekezwa ili zizae.

Kiungo cha pili ambacho ni WATU au TIMU ndicho kitakachoendesha na kusimamia biashara na huhusisha usimamizi na utaalamu wa kiufundi wa biashara.

Kiungo cha tatu kinachohitajika ili biashara iweze kuanza ni FURSA(DILI), unaweza pia ukakiita MPANGO au BIASHARA yenyewe. Dili laweza kuwa ni biashra ya majengo na ardhi au hata biashara tu ya kawaida lakini ile inayoweza kuleta faida. Lakini katika kitabu hiki cha THE 5 MILLION DOLLAR BOOK kimezungumzia zaidi biashara ya ardhi na majengo(Real Estate). Dili ndiyo kiungo muhimu zaidi katika biashara kwani ndicho huvutia viungo vingine vya Pesa na Watu.


Mjasiriamali mwenye uwezo wa kuviunganisha viungo hivi vyote 3 kwa weledi ndiye hufanikiwa na kupata faida kubwa katika biashara yeyote ile ikiwemo biashara ya ardhi na majengo hata kama hana fedha kabisa mfukoni huku pia akiwafanya wafadhili wake au wawekezaji aliowatumia pia kupata faida kubwa.

Ukiweza kumiliki viungo 2 peke yake kati ya 3 ni rahisi kupata kiungo cha 3 lakini ikiwa utamiliki kiungo kimoja tu peke yake itakuwa vigumu sana kuweza kuvutia viungo vingine 2 na hivyo hutaweza kufanikiwa.

Hiyo ni sehemu tu ya kitabu hicho, The Five Million Dollar Book” ambacho mwndishi wake Stefan Aarnio ameeleza hatua kwa hatua jinsi yeye mwenyewe binafsi alivyoweza kumiliki utajiri mkubwa kupitia biashara ya ardhi na majengo akiwa hana hata senti tano mfukoni. Ukikisoma kitabu hicho chote unaweza kuanza mra moja biashara hii ya majengo hata ikiwa huna mtaji wa fedha.

……………………………………….
Mpendwa msomaji zile semina na masomo yahusuyo fedha na michanganuo ya biashara ndani ya Group la whatsapp la MICHANGANUO ONLINE bado zinendelea kila siku usiku saa 3 kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu. Pia unapata offa ya masomo na semina zilizopita, vitabu na michanganuo mbalimbali ikiwemo ya kuku. Lipi kupitia namba 0712202244 au 0765553030 kisha utume anuani yako ya email na ujumbe wa “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

Somo la leo kwenye Group litakuwa na kichwa cha habari kinachosema; KWANINI NI HATARI KUKOPA AU KUWAKOPESHA NDUGU NA JAMAA WA KARIBU?
            


1 Response to "JE WAJUA UNAWEZA KUMILIKI KIWANJA AU NYUMBA BILA KUTOA SENTI 5 MFUKONI? SOMA KITABU CHA DOLA MILIONI 5 UJUE"