IPI SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA KATI YA USIMAMIZI, SOKO NA UENDESHAJI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IPI SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA KATI YA USIMAMIZI, SOKO NA UENDESHAJI?

SOKO,UTAWALA & UENDESHAJI

Sri ya mafanikio ya kila biashara hutegemea sana usimamizi, uendeshaji na soko lako. Kila biashara ni lazima iwe na idara mbalimbali zinazofanya kazi pamoja kusudi biashara iweze kutimiza malengo yake kama mmiliki wake alivyokusudia ni sawa na ilivyo kwa mwili wa binadamu kila kiungo na umuhimu wake. 

Idara hizi kwenye biashara zipo nyingi zaidi ya soko, uendeshaji na usimamizi na unaweza ukazitaja zote au kuzijua kwa urahisi kwenye vipengele mbalimbali katika mpango wa biashara lakini idara zinazotajwa mara kwa mara zaidi ni hizi, USIMAMIZI, SOKO na UENDESHAJI.

Naziita idara lakini unaweza ukaziita jina lolote kulingana na mazingira ya biashara yako kwani kwa mfano ukitaka kuanzisha biashara ya mtu mmoja unaweza usiseme idara ukasema tu ni shughuli za usimamizi, masoko na uendeshaji.

Kwa kweli kama ilivyo kwa viungo vya mwili wa mwanadamu vitu vyote 3 pamoja na hivyo vingine nilivyosema kwenye biashara ni muhimu lakini hapa tunatakiwa tulenge zaidi kile kinachohusika moja kwa moja na kazi ya kusababisha fedha ziingie kwenye biashara kwa kuwa lengo letu ni kutafuta hasa mbinu za kuongeza mzunguko wa fedha kwenye biashara zetu

 SOMA: Njia ya mafanikio ni nyeupe kwa mjasiriamali mdogo anayeweza kuvikwepa vidakizi hivi.

Hebu fanya zoezi lifuatalo, chukua vitu vyote hivi vitatu, viweke mahali kisha kila kimoja kipe mazingira yote sawa na mwenzake, kama ni bajeti kila moja ipe bajeti sawa na mwenzake, kama ni muda hivyohivyo. Kisha baada ya hapo biashara yako izalishe bidhaa au huduma nyingi lakini wateja wawe wachache sana kiasi cha kutisha.

Hebu niambie ukiwa kama meneja au mmiliki wa biashara  ni hatua gani za kwanza utakazoanza kuzichukua kabla ya nyingine?

Bila shaka yeyote utanijibu kwamba utaanza kutafuta soko la bidhaa au huduma hizo kwa udi na uvumba kusudi zisizidi kukudodea. Sidhani kama utaniambia eti utaongeza uzalishaji wa bidhaa huku zikiendelea kuoza, wala kuajiri wasimamizi zaidi wakati bidhaa zimejaa stoo hazina wanunuzi.

Tunapojiuliza swali, ni ipi siri ya mafanikio ya biashara kati ya usimamizi, soko na uendeshaji, Soko au kwa maneno mengine wateja ndiyo kiini cha mafanikio ya biashara yeyote ile. Sisemi idara nyingine hazina umuhimu hapana, ila soko ndiyo kitu muhimu zaidi katika kuhakikisha biashara inafanya vizuri na kuleta mafanikio yaliyokusudiwa na mwanzilishi wake au waanzilishi.

SOMA: Je, wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?

Biashara zetu huwa zinashindwa kutengeneza mzunguko chanya wa fedha au kwa maneno mengi kutengeneza utajiri haraka kutokana na sababu hii kuliko sababu nyingine zozote zile na hii hutokana na sababu kwamba tunashindwa kuelewa ni nini hasa maana ya utafutaji wa masoko ya biashara zetu tukidhani kuwa utafutaji wa soko ni kile kitendo cha kutangaza biashara tu peke yake kama vile kutangaza redioni, mtandaoni au kwenye magazeti na vipeperushi kumbe siyo, ni zaidi ya hivyo.

Ukichunguza kwa umakini tabia za watu waliofanikiwa maishani ni pamoja na hulka yao ya kujitangaza sokoni, kujijengea majina makubwa yanayodumu akilini mwa wateja ambao hatimaye wanafanya kazi ya kuwatangaza kwa watu wengine bure bila ya wao kuingia gharama zozote zile za ziada.

Dhana ya kutafuta soko ni pana kidogo, utafutaji wa soko ni mchakato unaoanzia pale unapopata wazo la biashara unayotaka kuifanya, unapoanza kutengeneza bidha zako au huduma mpaka dakika ya mwisho unapokuwa ukimkabidhi mteja na yeye kukupa fedha yake. Ukikosea hata hatua moja kwenye mchakato huo mzima na ujue umeharibu au kupunguza ufanisi wa shughuli za kimasoko za biashara yako na hivyo kuidumaza isikuletee faida haraka.

SOMA: Umuhimu wa kuligawa soko la biashara yako katika makundi/vipande tofauti 

Mchakato huo wa kimasoko ninaouzungumzia maarufu kwa kimombo kama 4ps, unajumuisha; BIDHAA, BEI, MATANGAZO na ENEO (MAHALI), Product, Price, Promotion and Place. Hii inamaanisha, kutoa huduma au bidhaa sahihi, katika eneo sahihi, kwa bei sahihi na kwa wakati sahihi.

Ikiwa kimoja kati ya hivi kitakosekana basi biashara au kampuni italazimika kuingia hasara kubwa na wakati mwingine kufa kabisa. Biashara nyingi hukosa mzunguko mzuri wa fedha kwa sababu tu ya kukosa mpangilio mzuri wa shughuli hizi 4 za kimasoko. Ukitaka kuanza biashara au unaendesha biashara ya zamani siri kubwa ya kufanikiwa ni kuhakikisha unatengeneza mpango wako wa masoko mapema hata kabla hujaanza biashara yenyewe. 

Kumbuka mteja ndiyo kiini cha soko na thamani ya bidhaa au huduma hutegemea mtazamo wa mteja na lengo lake ni kumfanya huyu mteja aridhike na kuendelea kumfanya kuwa mteja mtiifu kwako au biashara yako.

SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu-1

Hebu tuone mchakato mzima wa kimasoko ulivyo na jinsi unavyoweza kuutumia katika biashara yako kuifanya yenye kutiririsha fedha zaidi ndani kuliko kuzitoa nje. 

1. Tafuta kiini cha bidhaa/huduma zako,

kiini hiki ni ile faida atakayoipata mteja, jiulize ikiwa kama faida hiyo itawashawishi wateja kununua. Dalili ya utajiri huanzia pale unapoona umebuni bidhaa ama huduma inayohitajika mno na wateja, wateja hawawezi kuishi bila huduma/bidhaa hiyo.

Na hata kama ikiwa ni anasa mtu wa kawaida anayoweza kukwepa kuinunua basi matajiri au wanaomudu kuinunua hiyo bidhaa/huduma hakikisha hawapati kabisa sababu ya kuacha kuinunua. Usiishie tu kuhangaika kutangaza kila mahali bidhaa au huduma  utapoteza fedha na muda wako bure ikiwa kama huna sababu nzito ya wateja kununua toka kwako.

2. Wajue wateja wako.

Ni nani atakayenunua bidhaa yako, anahitaji nini, thamani ya bidhaa/huduma yako kwake ni kitu gani. Ukivifahamu vitu hivyo bayana utakuwa na uhakika kwamba bidhaa/huduma zako ni sahihi kwake na malengo yako pia ni sahihi

SOMA: Jinsi ya kupata wateja wengi kwenye biashara yako kwa kufanya kile wajasiriamali wengi wanachosahau kukifanya

3. Tambua washindani wako.

Fahamu bei zao, huduma na bidhaa zao na ulinganishe na zile zakwako ili uweze kupanga bei muafaka.

4. Fanya Tathmini ya Eneo utakalouzia bidhaa/huduma zako.

Ukizingatia ikiwa kama wateja wako watakuwa tayari kufika eneo hilo bila vikwazo vyovyote, zingatia pia gharama zake na ukubwa wa biashara. Je lina faida zipi zinazolandana na biashara yako?

 5. Tengeneza Mkakati wa Mawasiliano/Matangazo

Njia yeyote ile ya matangazo utakayotumia unatakiwa uhakikishe unawafikia wateja wako watarajiwa na kuhakikisha kwamba faida za bidhaa au huduma ulizoainisha zinaeleweka vyema na kupewa kipaumbele cha kwanza.

6. Hakikisha vipengele vyote vinne, BIDHAA, BEI, MATANGAZO na ENEO vinahusiana na kutegemeana na havipingani mahali popote pale. Kuwekeza pesa zako kwenye biashara bila ya kulizingatia hili hauna tofauti na mtu anayeendesha gari angali amefumba macho.

Unapoanzisha biashara yako au bidhaa mpya sokono ni lazima uhakikishe unazingatia vipengele vyote vinne kwa usawa ijapokuwa unaweza ukafika mahali ukaamua uzingatie kimoja au viwili zaidi ya vingine kulingana na utakavyoona umuhimu wake katika kufanikisha zaidi biashara yako.

SOMA: Kukuza biashara yake haraka, mjasiriamali mdogo anapaswa ajue vitu hivi 10 

Nahitimisha somo hili la leo kwa kusema kwamba, SOKO au utafutaji wa soko la biashara yako ni kitu cha kuangalia kwa umakini wa hali ya juu hata kama ikiwa biashara ni ndogo kiasi gani, tenga muda wa kutosha na fedha kwa shughuli zako za masoko angalao hata asilimia 10% ya mauzo yako yote iende kwenye masoko kwani soko ndilo linalohusika na uletaji wa fedha katika biashara moja kwa moja kuliko shughuli nyinginezo zozote katika biashara yako. Ndiyo siri kubwa zaidi ya kufanikiwa biashara yako kuzidi hata usimamizi, uendeshaji, fedha, mauzo na idara nyingine zote katika biashara yako

 

......................................................

TAARIFA MUHIMU!

1.   Nikukumbushe kuhusiana na ile OFFA ya vitu 12 bado ipo ingawa inakaribia kufika mwisho wake. Offa hii unalipa ada ya mwaka kujiunga na group la masomo sh. Elfu 10 kisha nakutumia vitabu na michanganuo ya biashara kamili, jumla vitu 12 papo hapo kama uonavyo katika orodha pale chini mwisho.

2.   Nakutumia pia masomo mbalimbali yenye maudhui ya fedha tuliyokwishajifunza tangu group linaanza mpaka sasa hivi.

3.   Nakuunganisha na group la masomo ya fedha & semina za Michanganuo ya biashara ikiwa unapenda kama hupendi nakutumia tu offa zako.

Semina za jinsi ya kuandika hatua kwa hatua Michanganuo ya biashara bunifu zenye fursa kubwa ni kila wiki na zinaaza wiki hii. Tutachanganua biashara zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo. Ni fursa nzuri ya kujifunza kuandika mpango wowote ule wa biashara kwa gharama nafuu kabisa.

Siyo lazima ziwe ni biashara za mtaji kidogo ama zinazolipa haraka lakini tutajitahidi kuonyesha ubunifu wa hali ya juu mjasiriamali anaoweza kuutumia katika kuigeuza biashara hata isiyokuwa na fursa kubwa ikawa biashara inayolipa sana.

Ikiwa unahangaika kutafuta wazo bora la biashara inayolipa unakaribishwa kwani katika mawazo mengi tutakayochanganua huwezi ukakosa wazo hata moja utakalofanyia kazi likakupa matokeo makubwa. Au hata ukapata mbinu mbalimbali za kiubunifu utakazoweza ‘kuapply’ kwenye biashara yako unayoifanya sasa hivi.

Kulipa ada tumia namba zangu hizi, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na baada ya malipo tuma ujumbe kwa meseji au watsap usemao, “NATAKA OFFA INAYOKARIBIA MWISHO”

 

ORODHA YA VITU 12 VYA OFFA INAYOKARIBIA MWISHO WAKE NI HII HAPA CHINI;

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Imeandaliwa na:

Peter Augustino Tarimo

0712202244

0765553030

0 Response to "IPI SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA KATI YA USIMAMIZI, SOKO NA UENDESHAJI?"

Post a Comment