NJIA YA KUTENGENEZA PESA ZA ZIADA ISIYOJULIKANA NA WATU WENGI BADO (PASSIVE INCOME) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NJIA YA KUTENGENEZA PESA ZA ZIADA ISIYOJULIKANA NA WATU WENGI BADO (PASSIVE INCOME)

kutengeneza pesa za ziada ukiwa umelala usiku

Tunapozungumzia njia ya kutengeneza kipato cha ziada (Passive income) maana yake hasa ni pesa au kipato kile mtu anachoingiza iwe anafanya kazi au hafanyi. Mara nyingi kipato cha ziada huhusishwa na uhuru wa kifedha ingawa siyo lazima mtu unapoingiza kipato cha ziada basi pia uwe huru kifedha. Siri ya utajiri ipo kwenye ujanja wa kuingiza pesa nyingi za ziada na wala mtu asikudanganye eti ipo dawa ya kupata pesa ama utajiri nje ya hiyo. 

Kwa upande mwingine uhuru wa kifedha unaweza kuwa na maana moja kati ya hizi 2 zifuatazo kulingana na mazingira na kipato cha mhusika.

1.   Maana ya kwanza mtu anajihesabu kuwa huru kifedha pale anapokuwa anaingiza kipato cha ziada kinachotosha kugharamia mahitaji yake yote ya msingi. 

 

2.   Maana ya pili ni pale mtu anapokuwa na kipato cha ziada cha kumuwezesha kulipia kitu chochote kile akitakacho maishani ikiwa ni pamoja na vitu vyote visivyokuwa muhimu hata vile vya anasa.  

Mtu aliyekuwa huru kifedha yeye afanye kazi asifanye pesa au kipato huingia kama kawaida. Watu tumezoea na tunafahamu kwamba ili mtu kupata kipato cha ziada ni lazima aanzishe au awe na moja kati ya vitegauchumi hivi vifuatavyo vinavyohusisha uwekezaji wa mara moja tu kisha kutoa mapato endelevu kwa muda wote unaofuata bila ya uwekezaji mwingine, tena bila ya kufanya kazi moja kwa moja. Vitegauchumi hivyo ni kama vile;

·      Kodi itokanayo na upangishaji wa jengo/nyumba

 

·      Riba kutoka katika akaunti ya akiba ya benki

 

·      Gawio kutokana na uwekezaji kwenye hisa za kampuni/biashara

 

·      Mirahaba kutokana na kazi za kisanii, muziki, filamu na utunzi wa vitabu nk.

Kwa kifupi hivyo ndiyo baadhi ya vitegauchumi watu wengi walivyozoea kuona kama ni vipato vya ziada (passive income). Kodi ya nyumba kwa mfano mmiliki kazi pekee atakazofanya ni kukusanya tu kodi yenyewe na labda kufanya matengenezo madogomadogo pale yatakapojitokeza, kazi ambazo huwezi ukasema zisipofanyika kipato kitakoma kuingia. 

Tukiingia kwa undani kujua zaidi maana ya kipato cha ziada (passive income) tunaambiwa ni kipato kile mtu anachoweza kuingiza hata ikiwa yeye mwenyewe hayupo pale katika eneo la tukio. Kwa lugha rahisi mtu huyu fedha zinatiririka kwake hata ikiwa ataamua kulala mchana kutwa na usiku, siku 7 za wiki na hii ndiyo njia kuu matajiri wanayoitumia kupata utajiri haraka.

Watu wengi hii huifanya pasipo kutambua kama ni kipato cha ziada. Kwa mfano hata ukiweza kununua mashine ambayo unaweza ukaiweka mahali ikahudumia wateja wakati wewe haupo pale, nayo ni njia ya kukuingizia kipato cha ziada.

Hata ukiweza kubuni jinsi ya kuingiza pesa kupitia simu yako kama vile kuingiza pesa mtandaoni kwa kutumia blog na mitandao ya kijamii nayo inahesabika kama mbinu ya kuingiza pesa za ziada.

Hata hivyo siyo kila njia ya kuingiza pesa online unaweza ukaiita ni kipato cha ziada hapana, kwa mfano huwezi kusema blogu au ukurasa wa mtandao wa kijamii unaotakiwa kupost kila siku ndipo upate wateja ni passive income hapana lakini ikiwa utapost siku moja moja huku wateja wakija hata baada ya muda mrefu kupita basi hiyo ni njia ya kukupa kipato cha ziada.

Kabla hatujaenda kuona njia hiyo ya kuingiza kipato cha ziada isiyojulikana na watu wengi bado, hebu kwanza tuone ni kipato cha ziada kiasi gani mtu anahitaji ili kuwa huru kifedha.

Unahitaji kipato cha shilingi ngapi kuwa huru kifedha?

Unaweza ukajiuliza, upate kipato cha ziada kiasi gani kusudi ujue sasa umeshakuwa huru kifedha?” hupaswi wala kuumiza kichwa kwani jibu lake ni rahisi sana. Tumesema awali kwamba, kuwa huru kifedha kunaweza kutafsiriwa katika maana 2, ya kwanza ni pale mtu utakapoweza kuyamudu mahitaji yako yote ya msingi pasipo kubabaika na ya pili ni pale utakapoweza kuingiza kipato cha ziada kinachotosha kugharamia mahitaji yako yote ya msingi hata yale yasiyokuwa ya msingi mfano anasa huku ukiwa huna haja ya kuuza muda wako ndipo uweze kulipia gharama hizo. 

Sasa kanuni au hesabu rahisi ya kujua kama umeingia kwenye uhuru wa kifedha, unaorodhesha mahitaji yako yote ya msingi mahali kisha unayajumlisha, jibu utakalopata sasa ndiyo kipimo. Kipato chako inabidi kiwe kikubwa ama juu ya mahitaji yako yote ya msingi.

UHURU KIFEDHA = KIPATO CHA ZIADA > MATUMIZI

Hiyo ni hatua ya kwanza, ukitaka sasa kuufikia ule uhuru wa kifedha namba 2, inabidi katika matumizi yako yote ujumuishe na yale matumizi yako yote yasiyokuwa na umuhimu sana kama vile matumizi ya anasa nk. Ikiwa kama bado hujamudu kufikia hatua ya uhuru namba 2 wa kifedha basi usijaribu kuweka matumizi yasiyokuwa na umuhimu kwani huo hautakuwa tena uhuru kifedha bali utakuwa ni utumwa kifedha.

Njia ya kupata kipato cha ziada watu wengi wasiyoijua

Kichwa cha somo hili pale juu ni “NJIA YA KUINGIZA PESA ZA ZIADA AU TUSEME KIPATO CHA ZIADA WATU WENGI WASIYOIJUA” sasa hebu tukaone njia hiyo ni kipi; 

Pale juu niliorodhesha baadhi ya miradi iliyozoeleka kuwa ndiyo njia kuu za kuingiza kipato cha ziada au passive income mfano biashara za uwekezaji kwenye majengo na hisa lakini inasahaulika mara nyingi kuwa ipo njia nyingine kubwa ya kuingiza pesa za ziada tofauti kabisa na hizo nilizozitaja. Sasa basi njia hiyo ni ipi na inafanyajefanyaje kazi?

Ili kujua kila kitu kuhusiana na njia hiyo, ungana namimi kwenye darasa la Michanganuo na masomo ya pesa kila siku, MICHANGANUO-ONLINE kwa kiingilio cha sh. Elfu 10 tu ada ya mwaka mzima.

Punde tu ulipiapo nakutumia vitu vifuatavyo;

1.   OFFA ya vitu 12

2.   Masomo yote ya pesa yaliyopita

3.   Kukuunga na group la masomo ya kila siku

Kulipa tumia namba zetu; 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo

Na baada ya malipo tuma ujumbe kwa sms au wasap usemao, “NATAKA OFFA YA VITU 12 NA KUUNGANISHWA NA GROUP”

 

OFFA YA VITU 12 INA VITU VIFUATAVYO;

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)


SOMA NA HIZI HAPA:

1. Njia za kuingiza kipato cha ziada nje ya kazi yako

2. Kama pesa haijawahi kuwa rahisi kupatikana kwanini uchezee pesa?

3. Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?

4. Sababu 5: Kwanini masikini wengi hawafanikiwi kirahisi (Nakosea wapi part ii)

5. Bajeti: Jinsi ya kusimamia, kutunza na kutumia vizuri fedha binafsi na za biashara yako


0 Response to "NJIA YA KUTENGENEZA PESA ZA ZIADA ISIYOJULIKANA NA WATU WENGI BADO (PASSIVE INCOME) "

Post a Comment