Mwazo tuliweka
ratiba ya usomaji iliyoelekeza kila siku kusoma kurasa 10 kwa nakala ya kitabu
ya kiingereza lakini kurasa 21 kwenye nakala ya kitabu kwa Kiswahili, Hata
hivyo kutokana na changamoto ya kuchelewa kumaliza kusoma kwa wengi wetu,
tumeamua sasa hivu kuvunja uratatibu wa kurasa 10 kwa siku na badala yake sasa
tutaendelea kusoma kurasa 10 mpaka karibu kila mmoja anapokuwa amemaliza ndipo
tunaanza tena nyingine 10
Kwa mfano mpaka
leo hii bado hatujaanza kurasa 10 za session ya tatu bado tupo session ya 2
mpaka wadau wote waweze kumaliza. Tumeamua hivi kutokana na ukweli kwamba lengo
letu la kuanzisha utaratibu huu wa kusoma hiki kitabu cha Think and Grow Rich
ni ili kila mdau aweze kunufaika vilivyo na maarifa ya kipekee yaliyomo ndani
ya hiki kitabu ambapo anaweza kwenda kuyafanyia kazi maisha yake yakabadilika
na kuwa mtu mkuu - anayethaminika katika
jamii (To become Great).
Taratibu taratibu
kila mtu akizoea na sote tukiwa na kasi inayolingana au kupishana kidogo kwenye
usomaji basi tunaweza tukarejea kwenye ratiba yetu siku za mbele.
Leo tayari nimemaliza
kuandaa ripoti yangu ya usomaji kurasa 10 za session ya pili (pg. 9 – 18 for English version) na (uk.17 – 37 kwa nakala ya Kiswahili). Na
nitaipost hapa kwenye group jioni baada ya kila mmoja wetu kukamilisha session
hiyo.
Hivyo naomba
sana tujitahidi kutafuta muda wa kupitia hizo kurasa 10 no matter what.
Leo hii unaweza
kuona ugumu lakini kesho na keshokutwa itakuwa vigumu zaidi, haujawahi
kupatikana muda muafaka kwa ajili ya kusoma kitabuchochote kile nadhani
mwenyewe ni shahidi na unakumbuka jinsi hata mashuleni tulivyokuwa tukihaha na
kukikimbizana misimu ya mitihani, hivyo jisukume itawezekana tu!
Nategemea pia
mirejesho kwa namna ya ripoti fupifupi au hata ikiwezekana unaandaakabisa
ripoti yako ya Sura, sura ikiisha unashea hapa si mbaya.
Majedwali 2
hapo chini yanaonyesha tathmini ya ratiba yetu tuliyopanga mwanzo ‘A’ na ile
inayojitokeza kwenye usomaji halisi ‘B’
A B
SESSION 1 |
29/07/2025 |
|
SESSION1 |
29/07/2025 |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
SESSION 2 |
30/07/2025 |
SESSION 2 |
30/07/2025 |
|
|
|
|
31/07/2025 |
|
|
|
|
|
|
SESSION 3 |
31/07/2025 |
SESSION 3 |
01/08/2025 |
Soma kilichopita kwenye Usomaji huu
Soma kifuatacho kwenye Usomaji huu
0 Response to "SABABU YA KUVUNJA RATIBA YETU YA USOMAJI WA KITABU CHA THINK & GROW RICH"
Post a Comment